Uteuzi Mkurugenzi wa TBC, Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi Mkurugenzi wa TBC, Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mike Mushi, Apr 27, 2011.

 1. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

  Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011.

  Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).

  Bwana Mshana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Dunstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake


  ------------


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja wa Wizara, na Naibu Makatibu Wakuu 10 wa Wizara mbalimbali.

  Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Naibu Katibu Mkuu mmoja kutoka Wizara moja kwenda nyingine.

  Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo wa maofisa hao waandamizi wa Serikali unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011, na wataapishwa Jumamosi wiki hii, Aprili 30, saa sita mchana.

  Taarifa hiyo inasema kuwa katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bwana Job D. Masima kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

  Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemhamisha Injinia Mbogo Futakamba aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji kwenda Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Taarifa hiyo inasema kuwa Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni kama ifuatavyo:

  • Bwana Aphayo Kidata ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kidata alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  • Bwana Hab Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri.

  • Bwana Charles Amos Pallangyo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Pallangyo alikuwa Mkurugenzi wa Uratibu – Ofisi ya Waziri Mkuu.

  • Bibi Mwamini Juma Malemi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya hapo alikuwa Msaidizi wa Makamu wa Rais katika masuala ya Maendeleo ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Wananchi.

  • Injinia Mussa Ibrahim Iyombe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi na JKT. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Usafiri katika Wizara ya Ujenzi.

  • Injinia Dkt. John Stanslaus Ndunguru ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi katika wizara hiyo hiyo ya Ujenzi.

  • Bwana John Thomas James Mngodo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi. Kabla ya uteuzi wake alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula.

  • Bibi Anna T. Maembe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Kabla ya uteuzi wake, Bibi Maembe alikuwa Mkurugenzi wa Mazingira na Habari wa NEMC.

  • Bibi Sihaba Nkinga ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Uchukuzi.

  • Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.
   
 2. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  source:times FM muhtasari wa habari saa kumi jioni leo.
  na makatibu wengine wameteuliwa leo na muungwana.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,315
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.

  huu uteuzi kichwa mafuta?? maji akafanye nini injinia huyu maskini???
   
 4. K

  Kana Amuchi Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kamtosa mnyalukolo?? au amestaafu maana umri pia umesonga!!
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  It will never change anything. we are still living in difficulties. He is going to change here and there but their brain are already damaged by ufidadi and MAGAMBA. We are expecting nothing.
   
 6. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naimani atakuwa amestaafu, maana alitoka nae mambo ya Nje mpaka leo...!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,315
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  hiyo sio breaking mkulu soma jf kwa umakini ahsante kwa unaniino afadhali kamwondoa yule kilema wa mawazo
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Saafi big up mr prezident
   
 9. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Unajuaje mkuu?inawezekana huyo ni Injinia wa Rasilimali Maji.
   
 10. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  mkulu asante kwa ufafanuzi maana nimechanganywa na hiyo taarifa na sikuwa kwenye net kwa muda hivyo nimejikuta nimeitumbukiza kama hivyo ilivyokuja!
  kama imekukwaza pole!
   
 11. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante sana Mkuu kwa kutujuza.

  Ninawapongeza sana kwa wote walioteuliwa.

  Wito wangu kwao: Tanzania tunahitaji tutoke hapa tulipo kwa kuwaletea watu wetu maendeleo. Uadilifu, Uaminifu, Ukweli, Uwazi na Uchapakazi (5U) ziwe nguzo imara kwa viongozi wetu waliopo na wanaoteuliwa sasa.
   
 12. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  'Bwana Hab Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri.'

  wakuu ukiwa karani baraza la mawaziri unakuwa na majukumu gani? je ni tofauti na makarani wengine nimepata utata kidogo ,kutoka ukarani hadi unaibu katibu mkuu
   
 13. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Operesheni vua gamba INAENDELEA...
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ina maana Luhanjo ndio kaondoka iwapo huyo jamaa Yambesi anakaimu? Maana Luhanjo nae umri ndio umemtupa mkono unless alisign affidavit ya kupunguza miaka ili asistaafu mapema!!
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Karani wa Baraza la Mawaziri siyo kama makarani wa kikoloni au makarani wa kwenye mashamba ya chai huyu ni Clerk kama Clerk of National Assembly kwa maana nyingine ni katibu
   
 16. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  zote hizo ni mbwe mbwe tu!, tunataka kunufaika na madini na rasilimali nyingine tumechoshwa na wizi!, maisha magumu yamepanda kwa 100% anatuletea story hizo!,
   
 17. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  bashiri Mrindoko alitajwa kwenye ripoti ya mwakyembe kuhusu richmond na azimio Na. 14 lilisema:

  AZIMIO NAMBA 14:

  "Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), na Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni. Aidha, Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza."

  tusiwe warahisi kusahau jamani!!
   
 18. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  JF nawaaminia sana.
  Ebu wenye habari za ziada za hawa wateuliwa watuwekee hapa ili tuone kama hawa nao si katika waliotiwa mifukoni na mafisadi.
  Naona wengi walioteuliwa walikuwa wakurugenzi katika wizara/idara fulani fulani nk; je yawezekana hawa ikawa walinisurika na fedha za mafisadi? na je wanaweza kunusurika nazo?
   
 19. k

  kuruti Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Clement Mshana ni mtu makini sana. Hajui na hana siasa za maji taka. ataipeleka TBC na Nchi mbali sana. Mungu amjalie afya njema. nawapongeza wengine ingawa sina UHAKIKA sana na utendaji wao ila naamini sio "mashemeji".
   
 20. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hongera Bwana Clement Senzota Mwete Mshana, Nenda kafanye alichokutuma aliyekuteua usije ukafuata ya Tido yeye huenda alikuwa hajajua vizuri TBC ni mali ya nani ndiyo maama akaruhusu mijadala nchi nzima japo wamiliki hawakushiriki.
   
Loading...