'Bwana Hab Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri.'
wakuu ukiwa karani baraza la mawaziri unakuwa na majukumu gani? je ni tofauti na makarani wengine nimepata utata kidogo ,kutoka ukarani hadi unaibu katibu mkuu
Clement Mshana ni mtu makini sana. Hajui na hana siasa za maji taka. ataipeleka TBC na Nchi mbali sana. Mungu amjalie afya njema. nawapongeza wengine ingawa sina UHAKIKA sana na utendaji wao ila naamini sio "mashemeji".
Ukiwa gamba utang'angania magamba wenzako.Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza tusiwe warahisi kusahau !
Akawarudishie wenye magamba TVT yao.Hongera Bwana Clement Senzota Mwete Mshana, Nenda kafanye alichokutuma aliyekuteua usije ukafuata ya Tido yeye huenda alikuwa hajajua vizuri TBC ni mali ya nani ndiyo maama akaruhusu mijadala nchi nzima japo wamiliki hawakushiriki.
Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.
huu uteuzi kichwa mafuta?? maji akafanye nini injinia huyu maskini???