Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu katika PDF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu katika PDF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 20, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Tangu nilipoanza utetezi wangu wa Dr. Harrison Mwakyembe, nimetoa majibu kwa watu wengi na kutoa hoja nyingine katika kurasa mbalimbali. Vile vile kuna mambo mengine ambayo ningeweza kuyaonesha lakini kwa kuendelea kujibizana na mtu mmoja mmoja, inanichukua muda mrefu kujenga hoja. Hivyo nimeamua kujipa jukumu hili la kutoa utetezi wangu wa wazi na usio na utata wa Dr. Harrison Mwakyembe: M. M.

  [​IMG]

  UTANGULIZI
  Ndani ya siku hizi chache tumeshuhudia hoja ambazo zina hisia nyingi na ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya yale yale mapambano ya kifikra. Hoja hizi zimejengwa hasa dhidi ya Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond ambayo ripoti yake Bungeni ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu kufuatia kashfa ya kampuni feki ya Richmond.

  Kuanzia matukio yale ya kihistoria ya mwaka jana hadi leo hii kumekuwepo na majaribio ya kila aina ya kumdhalilisha na kumbomoa Dr. Mwakyembe na ninaamini hili la sasa hivi limedhaniwa kuwa ndilo linaloweza kufanikiwa. Kuanzia suala la kukatiwa maji na DAWASCO mwezi wa nne mwaka jana. Wakati ule kama ilivyo sasa walioathirika na ripoti ya Mwakyembe Bungeni walionesha kufurahia kuwa hatimaye kumbe na Dr. Mwakyembe naye ni fisadi.

  Katika jaribio jingine la sasa kuna imani ya kwamba hatimaye safari hii wamempata. Hata hivyo hilo ni kundi moja tu.

  Kuna kundi la pili la wale ambao wanaamini katika maadili ya uongozi ambao wanaamini kuwa kwa jinsi walivyosoma na kutambua kuwa Dr. Mwakyembe naye ni mmiliki wa kampuni ya kufua umeme basi alitakiwa kutangaza maslahi hayo katika Kamati Teule (wakati wa kuzungumza Bungeni mwaka jana) na pia katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo yeye ni mjumbe. Hawa wanaamini Dr. Mwakyembe amevunja maadili na amekiuka miiko fulani.

  Hawa naweza kusema wanaongozwa na kanuni.

  Ni makusudio yangu kumtetea Dr. Mwakyembe dhidi ya makundi yote mawili na kuonesha kuwa hoja zao ni za kuvutia masikio lakini hazina msingi, ni dhaifu na tukiziangalia kwa karibu tutaona zina makosa mengi. Kwamba, makundi yote mawili yamekosea kwa hoja zao na kwa ushahidi wanaotoa. Tafadhali fuatana nami katika utetezi huu wa wazi wa Dr. Harrison Mwakyembe.

  Unapofuatana nami hakikisha unaangalia sana matumizi ya maneno yangu kwani najitahidi kuchagua maneno vizuri kutaka kumaanisha kile ninachokisema na kusema ninachomaanisha. Ukikosea stepu usisite kurudi nyuma kunipata vizuri.

  Kwa wale wageni na makala zangu za utetezi hii siyo makala ya kwanza au hoja ya kwanza ya utetezi. Huko nyuma nilisimama kumtetea marehemu Amina Chifupa baada ya "kunyamazishwa", nimemtetea Waziri Sofia Simba, na nimewatetea mabinti wa Nyegezi kina Nsia Swai. Na huu utetezi hautakuwa wa mwisho kwa mtu yeyote ambaye dhamira yangu inanituma kuamini kuwa aidha anaonewa au kutokana na nguvu zaidi anawekwa mahali ambapo hawezi kushinda.

  karibu....
   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Mar 20, 2009
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naona mkuu mwkjj umeamua uweke ''zege'' kabisa kuimarisha hoja ambayo watu wanataka kuipindisha ama makusudi au kwa kutoelewa dhana nzima ya CONFLICT OF INTEREST!

  Pengine baada ya hili zege watu wataelewa (kama wanapenda), turudi kwenye kipolo cha Dowans na mradi wa vitambulisho!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hata kama ikithibitika kuwa Dr Mwakyembe amekiuka maadili, hiy haitoondoa dhambi ya damu ya Richmond na Dowans
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Unajua uzuri kuwa suala hili limetufanya tuzungumzie maadili ya viongozi. Tatizo ni kuwa tulipoanza kuzungumzia hayo tukaruka kuangalia hoja yenyewe ya msingi hasa nini. Ikabakia watu wanahamisha magoli na kujaribu kuyaweka mahali ambapo badala ya mpira ufuate goli, sasa goli linafuata mpira!

  Bahati mbaya katika kufanya hivyo wamejikuta wametoka nje ya uwanja, lakini wanataka tuendelee kushangilia kuwa tumewafunga!

  Hoja hapa ilikuwa very simple: a. Mwakyembe alikuwa na maslahi ya kifedha ambayo yalikuwa yanatishiwa na ujio wa dowans/Richmond na kuwa kuwa mjumbe wa kamati ya madini na nishati wakati ana umiliki wa kampuni ya nishati ni makosa. Yote mawili katika upanuzi wa hoja yangu nimeyaonesha kuwa hayana msingi on facts, evidence, and logic. None whatsover.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Mpita Njia, haiwezekeni kwenye mahakama ya sheria kukuta amekiuka maadili. Kwenye mahakama ya public opinion inawezekana (kama ninavyoona humu) in a court of law ambapo kinachoangaliwa ni ushahidi na sheria, hakuna jaji anayeweza kumconvict.. except of course..na yeye ana conflict of interests!
   
 6. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nashindwa kuamini macho yangu kama zito kweli atacha kuwashambulia mafisadi na kuanza kutafunanawenyewe kwa wenyewe. Yaani mnamfukuza mwizi halafu analusha fedha nyuma mnaanza kuzigombania na kutoana macho mwenzenu anatokomea

  Mimi bado naamini kuwa hawa watu wawili bado watetezi wa wananchi ila tu bwana hawa mafisadi kwa kweli ni wanjanja sana
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mhhhh just wonderinmg, hivi mbona Mwambalaswa, ambaye naye ni mwanahisa wa hiyo kampuni na mjumbe wa kamati ya nishati na madini aandamwi kama Mwakyembe? Au yeye hana maslahi?
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Mafisadi wajanja sana wanatafuta njia zote ili kuonyesha kuwa RICHIMOND/DOWANS ni safi!sasa naona wanaelekea kushinda maana nimesoma michango mingi humu inamtuhumu Mwakyembe il hali sioni sababu kama uwepo wa campuni yake ndo umesababisha RICHIMOND/DOWANS kuonekana ni za kifisadi!
  Jamani watanzania tuamke vinginevyo mafisadi watashinda!
  Hongera sana MKJJ nimekusoma!
   
 9. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji,

  Mbona haukumtetea marehemu chacha Wangwe wakti akiwa na matatatizo kipindi kile wa matatizo yake na wakulu?

  Mbona haukumtetea Mengi wakati wa picha zile za kashfa ya yeye kuoa baada ya yeye kutoa Press Conference?

  Wewe unatetea tu wale unao ona wana maslahi na wewe siyo?
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MR GEMBE!......hapa swala ni kusimama kwenye HAKI tena katika maswala yanayohusu maslahi ya taifa.Sio kila kitu.mwanakijiji ANA POINT HAPA.tene kubwa tu.narudia tena TUNAANGALIA ZAIDI MAMBO YANAYOIATHIRI TANZANIA NA UCHUMI WAKE.who is mengi bwana???migongano ya kina wangwe ni ya kimaslahi binafsi..........OPEN YOUR EYES BWANA
   
 11. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji,

  Naomba unipe sababu kubwa tano za kitaalam na siyo za kisiasa ,Kwanini TANESCO isnunue mitambo ya DOWANS?

  Maana tumekalia kuzungumzia Rostama matra Lowassa ila hakuna sababu za msingi za kuikataza TANESCO wasinunue hiyo mitambo.

  Kwa kifupi tumetawalilwa na hisa zetu binafsi kuwa kila jambo linalofanyika ni la kifisadi.Tuankoelekea ni kubaya sana kwasabbu sasa hivi tunaongoza nchi kwa hisia!

  Sitaki kuingia kwenye dhambi hii.Jambo la muhimu ambalo Mwakyembe na watu weystaha kama yake ni kuwa wafanye uchambuzi pembunifu kujua gharam halisi ya mitambo hiyo kama ya DOWANS ni shilingi ngapi huko nje na siyo kuhisi ni ya ghali bila kuwa na vithibitisho

  Nimewasoma sana kwa wiki mbili sas ana hakuan aliyensihawashi kuwa mitambo ya dowans isinunuliwe na TANESCO.Mwakyembe ni one side minded Politician na kwa hili anatafuta umaarufu usiyo na maana.

  Tabia ya kukomoana ilianaz zamani na to make it clear,Lowassa ni mchafu ila kwa suala la RIchmond tulimuoenea and i know the truth about that issue!

   
 12. M

  Mama JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  FL,

  ukisoma vizuri mawazo mbalimbali utaona nia sio kuonyesha kwamba Richmond na Dowans ni safi. Mwakyembe anaandamwa kwa sababu ni 'mzalendo na shujaa', watu wanaquestion kwa nini huyo mzalendo na shujaa wao anafanya mambo ndivyo sivyo? Hatakiwi hata kuonekana karibu na tuhuma licha ya kutokutuhumiwa kabisa.

  Kumbuka mzalendo na shujaa huyu ana uzoefu katika fani mbali mbali zikiwemo uandishi wa habari, uanasheria, uhadhiri, uwakilishi wa wananchi bungeni n.k. ambazo kupitia kwazo alitakiwa ajue kabisa kwamba kuingia kwenye kamati ya kuchunguza Richmond, aliingia kwa kuonekana ni msafi, hana doa la kifisadi wala muingiliano wa kimaslahi! Alivaa ngozi ya kondoo akiwa na roho ya chui?

  Kumbuka alisema kuna mambo mengi anayatamani, hayo mambo ndiyo yanatilisha wasiwasi.

  Kwa hiyo FL, Mwakyembe sio kwamba anaandamwa kuliko Mwambalaswa au zaidi ya mafisadi wengine kwa ajili ya kumuonea au kuwapa credit mafisadi, hapana. Wananchi humu wanataka kumwona shujaa wao akiwa msafi, na usafi huo uonekane transparently. Asiweke viwingu viwingu visivyoeleweka.
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa nini sababu tano tu? kwa nini asikupe 100 au moja.....akupe tano za kukuridhisha wewe au zitakozomridhisha kila mmoja ya watz more than 40mil?....ulivyouliza swali hili inonyesha tayari unalojibu sahihi '''SABABU TANO"kama ndivyo haina haja kutegana!

  Kama utaka for real kuelimisha omba hivyo sio kulimit au kumpangia mtu eti akupe sababu tano!
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji,

  Spinning! ungekuwa unajali ukweli, ungeweka na arguments za watu wengine zilizotelewa hapa JF kuhusu vifungu mbalimbali ulivyoongelea.

  Kwa mfano hapa imejadiliwa vya kutosha nini maana ya maslahi kifedha, kwenye makala yako unarudia yale yale ambayo baadhi ya wana JF hapa wameweza kukuonyesha wazi kwamba maslahi ya kifedha hayaji pale tu unapopata faida au kupewa cash. Yanaanza toka unapoaanza ku take risk risk yoyote for expectation of future returns.

  Umeambiwa ushindani wa kibiashara hauanzi pale unapoanza kuzalisha, unaweza kuanza hata unapokuwa na mawazo tu. Unapoandaa proposal ya kampuni inakuwa pamoja na market research. Info ambazo Dr. alikuwa na access nazo kutoka kwa washindani wake kama IPTL, DOWANS na makampuni mengine zilikuwa zinampa unfair advantage ya kujua soko la nishati likoje. Kama huelewi hiyo ndio conflict of interest yenyewe.


  Private company yoyote ina lengo la future returns. Kama hutaki future returns, kama hutaki faida unaanzisha NGO.

  I challenge you Mwanakijiji kama mtetezi wa mawazo huru, kuweka pia maoni ya upande wa pili.

  Hapa unaonekana huna tofauiti na akina Ballile, unaongozwa na interests za mapenzi yako kwa mtu kuliko facts.

  Pamoja na kuelemishwa kwamba ile kamati ya Mwakyembe ilipewa uwezo wa kuangalia mikataba yote ya makampuni ambayo yanafanya biashara na Tanesco, wewe umeona ujikite kwenye DOWANS tu kwasababu unatumia chuki ya Watanzania juu ya DOWANS kama njia ya kupotosha ukweli, hiyo ndio inaitwa SPINNING!

  SHAME ON YOU MWANAKIJIJI!

  Kama msomi ulitakiwa uanze kwanza kwa kutoa maana ya hilo neno pecuniary in a legal sense kabla ya kuanza ku SPIN!

  Naambatanisha maana ya pecuniary hapa in a legal sense:

  Pecuniary refers to a something related to money, such as a monetary interest or award. he received thanks but no pecuniary compensation for his services" Pecuniary comes from Latin pecuniarius, "of money, pecuniary," from pecunia, "property in cattle, hence money," from pecu, "livestock, one's flocks and herds." If a statute provides for pecuniary punishment for violators, they are subject to being fined rather than face jail time. Non-pecuniary damages in a lawsuit refers to injuries like pain and suffering, that are not subject to a precise quantifiable amount in dollars.

  Kusema unaanza kampuni kwa lengo la kupata faida eti huna pecuniary interest is very shallow na naamini hata wewe unajua hilo. Angalia hata sheria ya renumeration. Ndio maana sehemu mbalimbali duniani, hata kampuni ikikulipia medical insurance, wewe unalipa tax kwenye hiyo amount. Ndio maana hizo shares za hiyo kampuni kama Dr. anampa mtu mwingine lazima alipe tax kwasababu hizo shares have monetary interest.

  Hata kwenye sheria za kazi kuna kitu kama percuniary loss, kwa mfano mtu akiumia na asiweze kufanya kazi tena, analipwa fidia kwa kutegemea pesa ambazo angeweza kupata siku za mbele. Haina maana ni kweli angepata hizo pesa lakini wakati huo inaamuliwa kunakuwa na probability kwamba angeweza kupata.

  Pia sio kweli kwamba kila mbunge ana uwezo wa kuona taarifa za siri ambazo ile kamati iliweza kuziangalia. Na sio kweli kwamba ile report iliweka taarifa za siri zote ambazo iliweza kuziona. Yeye Dr. mwenyewe alieleza kuna mambo mengi hawakuyatoa kwa faida ya serikali. Kamati yoyote ya uchunguzi hapa duniani, huona siri lakini wanapoandika report ambayo inatolewa kwa wananchi, zile siri ambazo zina madhara kwa kila mtu akiona huwa hawaziweki. Kuona kwao kunawasaidia kupata ukweli ili watoe judgement sahihi.

  Haki itatendeka Tanzania pale tutakapokuwa fair na sio kujadili issue kwa kuangalia sura ya mhusika.
   
 15. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  :mad:
  Gembe inaonekana wewe hufuatliii mambo sana kama viongozi wezi wa tanzania. Nimewahi kuweka fedha zinazotakiwa kununua hazizidi dola milioni hamsini na unaweza kuipata, GE, TAS, RESAR RAND, nk na warranty pamoja na installation hizo ni kampuni chache tu ndani ya USA hujaenda Japan, Canada, korea, uk, france, germany. generator hizo sio aghali hivyo ila kokodi ni bei nyingine.

  Mitambo ya akina rostam ni mizee na huwezi kununua kwani haina warranty na bei yake ni mbaya kuliko mpya.
  Huwezi kununua mitambo ambayo tayari wamiliki wake umewaita matapeli na kuwafungulia kesi.
  Huwezi kununua mitambo hiyo wakati ni kuvunja sheria ulizo jiwekea za manunuzi za kutonunua vitu vichakavu.
  huwezi kununua mitambo hiyo kwa gharama kubwa kuliko mipya.
  Huwezi kumlipa lowasa na rostam kwa mgongo wa nyuma.

  Huwezi kumtenganisha lowasa na richmond/dowans kama kweli unajua hili deal otherwise kaa kimya.
   
 16. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Next level,
  Kama hauna jambo la kuandika ni bora ukae kimya.Mie ninataka sababu tano na siyo mambo ya blah blaha tu.Kata ishu mkulu na siyo kuleta viroja na kama zipo sababu mia kama unavyosema ziweke hapa.

  Tabia ya kumshabikia na kumuona Mwanakijiji kama Mungu wako itakuja kukuponza(mpo wengi akiwamo Ngeleja aliyemuomba Mwanakijiji afukie fukie)

  Mkuu Mtanzania, Tupo Mstari mmoja!

  Mwanakijiji Sham on You again na kinachoniuma ni kuwa wakati mwingine huwa unaniboa kwa kubwatuka kama mvutaji wa bangi

  I have been warnging you kwa tabia yako ya kukurupuka tu kwa kumfurahisha mtu huku vitu vingine hauvijui,siyo kwamba kwa kuwa Dr. Mwakyembe ni Maanasheria wa katiba anajua kila kitu na akisema lazima tuamini hivyo,na kwavyovyote vile siyo anachosemea Mwanakijiji ni sahihi.Hell No!

  Jipange sawa sawa,ila utetezi wako umejaa hoja dhaifu
   
 17. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kinepi,
  hauwezi kusemea tu gharama yake ni kiasi flani bila ya kuja na uthibitisho,lete Invoice za hayo makampuni tuone ukweli kuhsuiana na hiloo na siyo habari za kuhisi tu.
  Na imeandikwa wapi ni mitambo ya kina Rostam?Lete uthibitisho na acha mambo ya kuspeculate!

  Wamilili DOWANS ni matapeli?wana kesi?wapi huko!
  Mitambo hiyo ni mizee vipi wakati siye ndiyo tumeanza kuitumia hapa nchini na ilianza kutumiwa na TANESCO hao hao,Sheria inasema vipi kuhusiana na vitu vichakavu?(lete kifungu)
  Huko kumlipa Lowassa na Rostama kwa mgongo wa nyuma kukoje embu elezea?hauleweki hapa

  Siwezi kaa kimya na huna uwezo wa kuninyamazisha bila kuwa na hoja za msingi!
  Ndiyo huwezi kuleta hoja kwa kuwa siyo mjenga hoja!
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Gembe,

  Watu tumetumia siku tatu hapa kujadili hili jambo hoja kwa hoja. Leo Mzee Mwanakijiji anaandika makala yake kwa kufuata eti kilichoandikwa kwenye Mtanzania, why?

  Ameamua kujikita kwenye hoja dhaifu ya gazeti la Mtanzania kwamba kulikuwa na ushindani wa kibiashara kati ya hiyo kamapuni na DOWANS.

  Kaacha argument zote ambazo wana JF wameziandika hapa juu ya hili suala ambazo hazikubaliani na yeye. Lakini wakati anaacha hizo arguments, kachukua mawazo mbalimbali kutoka hapa JF juu ya yale wanayokubaliana naye. Hii selective journalism ni kiwango cha chini mno, JF we are better than this!

  Angeandika hiyo makala kabla ya mjadala wa hapa JF ningemwelewa lakini kuamua kuacha arguments zote zilizotolewa na kurudi kule kule kwenye gazeti la Mtanzania inasikitisha sana. Hii kweli ina tofauti gani na wale waandishi wa kununuliwa tunaowalaumu kila siku hapa JF? Wanatoka kwenye press conference moja hiyo hiyo lakini wao wanaenda kuandika kile tu ambacho mabwana zao wanataka waandike.

  Mzee Mwanakijiji anajifanya anamshauri vyema Dr kwa hili lakini huenda anampotosha mno. Dr angweza kulijibu hili swali ki ukweli mtupu kwa dakika 10 na leo hii tungelikuwa tumeanza kusahau. Lakini kwa msomi aliyebobea kisheria kusema hakuna kabisa conflict of interest kwenye hili, kweli inasikitisha na kutia wasiwasi.

  Mnakumbuka ile ya rais Clinton kujikita kwenye narror definition ya neno sex? Eti ukitumia mikono sio sex kwi kwi kwi!!! Huu mjadala hauko mbali na mfano huo.
   
 19. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kama hivyo ndivyo basi mawazo ya wana JF hayatakiwi kupotea bure bila kuwafikia Watanzania walio wengi. Ikumbukwe kwamba wenye "access" ya mtandao ni wachache sana Tanzania. Sidhani kama Mwanakijiji ndiye mwakilishi wa JF kwenye magazeti ya Tanzania (!?).

  Tunaweza kuwa na majumuisho ya kila hoja iliyo ya moto kama hii ya Mwakyembe na yakachapishwa kwenye magazeti, walau mara moja kila wiki. Magazeti yetu yana uhaba mkubwa wa habari na kwa ubora na nguvu za hoja zinazotolewa hapa JF, hakuna mhariri wa gazeti mahiri atayekataa kuchapisha majumuisho yake angalau mara moja kwa wiki!

  Tufanyeje ili hili lifanyike?
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
   
Loading...