Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu katika PDF

Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu katika PDF

Nakubaliana kabis ana hoja ya msingi kuwa TUSIWE WEPESI WA KUONDOLEWA KIMAWAZO KWENYE HOJA YA MSINGI.....Fine, Mwakyembe ana conflict of interest (if that will make all of us feel better), je hii inabadilisha chochote kwenye maamuzi ya kipuuzi yaliyopelekea uzazi wa RICHMOND na mkwe wake DOWANS? Come on people, tuamke jamani....I wish ningekuwa above the law, shughuli ingekuwa moja tu kuezeka watu vibao na mikwaju....
And the issue is, almost watu wote tunajua who is behind the scum(s), lakini eti hakuna jinsi yoyote ya kum-link mtu na hayo ma-scum yenyewe..what is the point of having people kwenye nafasi tulizowapa?
 
Mzee Mwanakijiji,

Mbona haukumtetea marehemu chacha Wangwe wakti akiwa na matatatizo kipindi kile wa matatizo yake na wakulu?

Mbona haukumtetea Mengi wakati wa picha zile za kashfa ya yeye kuoa baada ya yeye kutoa Press Conference?

Wewe unatetea tu wale unao ona wana maslahi na wewe siyo?

MR GEMBE!......hapa swala ni kusimama kwenye HAKI tena katika maswala yanayohusu maslahi ya taifa.Sio kila kitu.mwanakijiji ANA POINT HAPA.tene kubwa tu.narudia tena TUNAANGALIA ZAIDI MAMBO YANAYOIATHIRI TANZANIA NA UCHUMI WAKE.who is mengi bwana???migongano ya kina wangwe ni ya kimaslahi binafsi..........OPEN YOUR EYES BWANA

Kwani huyu Mwanakijiji ndio mtetezi wa watu??? thehee utetezi mwingine bwana ooooh mbona jirani naye hamkumkamata wakati na yeye alijisaidia barabarani? hatutaki umengism/wamgweism suala ni FACTS KWENYE HOJA.
 
Nakubaliana kabis ana hoja ya msingi kuwa TUSIWE WEPESI WA KUONDOLEWA KIMAWAZO KWENYE HOJA YA MSINGI.....Fine, Mwakyembe ana conflict of interest (if that will make all of us feel better), je hii inabadilisha chochote kwenye maamuzi ya kipuuzi yaliyopelekea uzazi wa RICHMOND na mkwe wake DOWANS? Come on people, tuamke jamani....I wish ningekuwa above the law, shughuli ingekuwa moja tu kuezeka watu vibao na mikwaju....
And the issue is, almost watu wote tunajua who is behind the scum(s), lakini eti hakuna jinsi yoyote ya kum-link mtu na hayo ma-scum yenyewe..what is the point of having people kwenye nafasi tulizowapa?

Dina,

Hapo ndio kwenye tatizo. Kama umefuatilia huu mjadala watu wengi tumeandika clearly kwamba walichoandika Mtanzania kwa asilimia zaidi ya 90 hakikuwa sahihi. Hawakuwa na facts za kutosha kupata conclusion waliyofikia. KUna asilimia kama kumi iliyohusu umuhimu wa Dr ku declare interests zake naamini walikuwa sahihi.

Lakini pia tukaandika Dr alikuwa na uwezo wa kuchunguza mikataba yote ikiwemo documents za siri za Tanesco pamoja na wote wanaofanya biashara na Tanesco. Kwa mtu ambaye ana kampuni inayotegemea kufanya kazi karibu na hizo alitakiwa aeleze wazi interests zake kwenye hiyo sector ili kuwatendea haki makampuni mengine yote.

Je hili jambo linaondoa umuhimu wa ile report ya Dr? Mimi naamini hapana, ile ilikuwa ni kazi nzuri na ambayo huenda imeweka mfano wa kuigwa kwenye chunguzi zote za baadaye. Mimi pia naamini hata hiyo kamati angefanya mtu mwingine yeyote ambaye hana interests zake kwenye nishati, yale madudu ya Richmond yangejulikana tu. Madudu yenyewe si tuliyaandika hapa miaka na miaka?

Je kwasababu Dr. kafanya hiyo kazi nzuri, akikosea tusiseme, hapana, kama tulivyompongeza wakati ule, kama sasa kuna jambo ambalo tunaona amefanya kosa tuna wajibu wa kuandika kama ambavyo tuliandika watu kama akina mzee Warioba kule mwananchi Gold.

Huu mjadala sio about Either Dr. Mwakyembe or DOWANS. Huu mjadala ni mpana zaidi, unaenda zaidi kwenye maadili ya uongozi na umuhimu wa kufuata sheria. Tusianze mambo ya akina Bush, you are either with us or the terrorists. Unaweza ukachukia ma terrorists kwa nguvu zote na bado ukachukia serikali kupiga piga tu watu hata wasio na hatia.

Hii ya kuamini amini sana watu, mtakuja kutengeneza majambazi. Angalia akina Lamwai wako wapi? Akina Kaborou wako wapi? JK, ambaye mpaka watu wakasemwa ni chaguo la mungu, yuko wapi? Amini sheria, haki na principles, hizo huwa hazibadili, utakuwa salama muda wote.
 
Mzee Mwanakijiji,

Naomba unipe sababu kubwa tano za kitaalam na siyo za kisiasa ,Kwanini TANESCO isnunue mitambo ya DOWANS?

Maana tumekalia kuzungumzia Rostama matra Lowassa ila hakuna sababu za msingi za kuikataza TANESCO wasinunue hiyo mitambo.

Kwa kifupi tumetawalilwa na hisa zetu binafsi kuwa kila jambo linalofanyika ni la kifisadi.Tuankoelekea ni kubaya sana kwasabbu sasa hivi tunaongoza nchi kwa hisia!

Sitaki kuingia kwenye dhambi hii.Jambo la muhimu ambalo Mwakyembe na watu weystaha kama yake ni kuwa wafanye uchambuzi pembunifu kujua gharam halisi ya mitambo hiyo kama ya DOWANS ni shilingi ngapi huko nje na siyo kuhisi ni ya ghali bila kuwa na vithibitisho

Nimewasoma sana kwa wiki mbili sas ana hakuan aliyensihawashi kuwa mitambo ya dowans isinunuliwe na TANESCO.Mwakyembe ni one side minded Politician na kwa hili anatafuta umaarufu usiyo na maana.

Tabia ya kukomoana ilianaz zamani na to make it clear,Lowassa ni mchafu ila kwa suala la RIchmond tulimuoenea and i know the truth about that issue!

Heshima yako mkuu!

Kamati ya Shelukindo ilitoa ushauri (unaweza kuuita wa kisiasa!) kwa Tanesco(serikali) kutonunua mitambo ya Dowans. Kamati haikuwalazimisha Tanesco kufuata ushauri huo.

Kama Tanesco(na serikali) wanaamini zipo sababu za kitaalamu za kwa nini ni lazima tununue mitambo ya Dowans, ni kwa nini wanaogopa kufanya maamuzi ya kuinunua? Kama maamuzi hayo ni kwa manufaa ya taifa, kwa nini wanaogopa? Si wana wajibu wa kuhakikisha maslahi ya taifa yanazingatiwa?

Kwa kifupi wao (wataalamu- tanesco,serikali) wanajua ni dili chafu na kwa kuzingatia hizo sababu za 'kitaalamu' hawawezi kuonesha without doubt kwamba Dowans was/is the only option!

Ngeleja hataweza kudefend maamuzi ya kununua mitambo chakavu ya Dowans bungeni ndio maana anaogopa! Nadhani bado anakumbukumbu nzuri ya kilichowapata kina Msabaha na Karamagi.
 
Kwa hiyo waandishi wa habari wameamua kuwa mabaamedi wa mafisadi? Nionavyo mimi ni kwamba kama ilivyo kwa baadhi ya dada zetu wanavyokubali kudhalilishwa na walevi ili wapate mlo, ndivyo baadhi ya waandishi wa habari walivyoamua kudhailisha taaluma zao ili mafisadi wajaze matumbo yao!
Wasiwasi wangu ni juu ya hao nafisadi kuwa na uraia wa nchi zaidi ya mbili. wana pa kukimbilia wakati nchi itakapoporomoka kiuchumi na kisia! Je wataondoka na hao waandishi wa habari mabaamed?
 
Mwanaharakati/Mwandishi MKK huwa anachagua upande. Akiwa na urafiki na mtu atamtetea kwa kila jinsi. Akimchukia mtu utaona jinsi atakavyomkandamiza. Simshangai sana kuwa ni NDUMILAKUWILI.
 
Je hili jambo linaondoa umuhimu wa ile report ya Dr? Mimi naamini hapana, ile ilikuwa ni kazi nzuri na ambayo huenda imeweka mfano wa kuigwa kwenye chunguzi zote za baadaye. Mimi pia naamini hata hiyo kamati angefanya mtu mwingine yeyote ambaye hana interests zake kwenye nishati, yale madudu ya Richmond yangejulikana tu. Madudu yenyewe si tuliyaandika hapa miaka na miaka?

Hapa nipo mguu kwa mguu na wewe. Kinachofanya hii habari ionekane ina mrengo mwingine ni hisia kuwa imetolewa kwa lengo la kudiscredit kazi ya kamati teule ya Bunge. Na ndio maana katika mjadala, kwa kiasi kikubwa inashindikakna kwa wengi kutenganisha masuala haya mawili
 
Suala la conflict of interest ni kubwa sana kwa viongozi wetu, mtu kama Abdallah Kigoda alikuwa waziri wa madini na wakati huo huo alikuwa na migodi ya Tanzanite and the list continues kwa viongozi wetu kibao hata mkulu pia na hile hotel ya ngurdoto
 
Mzee Mwanakijiji,

Spinning! ungekuwa unajali ukweli, ungeweka na arguments za watu wengine zilizotelewa hapa JF kuhusu vifungu mbalimbali ulivyoongelea.

Haki itatendeka Tanzania pale tutakapokuwa fair na sio kujadili issue kwa kuangalia sura ya mhusika.

Mtanzania umelonga,
Unajua watu hapa wanaweka issue kuwa Mwakyembe vs Rostam. Lakini suala siyo hao sura za hao wawili, suala ni matendo yao ambayo yamekiuka maadili.

Sasa kama Rostam akikiuka tunamjadili, akikiuka Mwakyembe tukimjadili eti tunatumiwa na Rostam. Lengo ni kwamba watu wanataka wawatoe watu (kutoka kwa maana ya muziki wa bongo flava) ili wawe viongozi. Ni lazima tuwaambie mambo ya kutuuzia mbuzi kwenye gunia sasa hivi lazima yaishe. Maana 2005 JK mlimkimbiza hata kwenye mdahalo ili asipate maswali magumu, sasa hivi mnawatetea akina Mwakyembe wanapo flip flop sasa watakuwa viongozi gani wasipokoselewa wakajifunza?
 
Hapa nipo mguu kwa mguu na wewe. Kinachofanya hii habari ionekane ina mrengo mwingine ni hisia kuwa imetolewa kwa lengo la kudiscredit kazi ya kamati teule ya Bunge. Na ndio maana katika mjadala, kwa kiasi kikubwa inashindikakna kwa wengi kutenganisha masuala haya mawili

Mkuu,

Kwa bahati mbaya gazeti la Mtanzania liliandika habari ile likiwa na lengo hilo...ukianzia kwa headline yenyewe tu tayari ilikuwa imekaa kishabiki zaidi. Huweze kutenganisha masuala hayo mawili.
 
Hapa nipo mguu kwa mguu na wewe. Kinachofanya hii habari ionekane ina mrengo mwingine ni hisia kuwa imetolewa kwa lengo la kudiscredit kazi ya kamati teule ya Bunge. Na ndio maana katika mjadala, kwa kiasi kikubwa inashindikakna kwa wengi kutenganisha masuala haya mawili

Hapo ndipo tatizo linapoanzia. Watu walipobanwa kuhusiana na DOwans na wakashindwa, sasa wanasema wenyewe, "Wanamwaga mboga".

Rostam aliwahi kujitetea, Lowassa alijitetea pia. Wakati wanajitetea wote waliijua sana kampuni ya Dk. Mwakyembe (Nina hakika 100%) lakini hawakuitaja hata chembe kwa kuwa walijua haikuwa na madhara na waliona itawaharibia na wao hapo baadaye maana na wao wana kampuni inayoshindana na wananchi wa kule Singida (kisasida) na huko wanawakilishwa na RC, Kone.

Jamani sasa wanakuja eti kusema "kulikua na conflict of interest" baada ya Dowans kutupwa. Walijua baada ya Richmond scandal, watanzania watasahau na yale makubaliano yao ya kuiuzia Gov Dowans yatakamilika. Tujue kwamba, hata kabla ya Kamati ya Mwakyembe iliripotiwa kwamba hatimaye serikali itainunua Dowans ThisDay

Kwa ufupi, Watanzania tunachezewa na hawa jamaa waliwekeza sana kila sehemu na kama si ugumu wa Watanzania wachache, basi saa hizi tungekuwa tunaliwa tu bila hata kelele. Lakini kwa sasa angalao kuna kelele za mwizi!!! Mwizi!!!! hata kama anakuwa amekwiba na kukimbia atakuwa ametoka jasho na si kupora na kutembea.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hapa Uk kuna mtu anitwa LORD SAINSBURY, Kuna kipindi alikuwa kamati ya viwanda na bishara na yeye ni mwana hisa mkubwa wa sainsbury supermarket.

Je mwakyembe kujihusisha na biashara ya nishati kumeisaidia bunge kuwa na mtaalamu wa biashara hiyo?
Je mwakyembe kujisisha na nishati kumesaida hata kujulikana hiyo mitambo inauzwa kwa kiasi gani?
Huwezi ukawa na tume nzima hamna hata mtu mmoja mwenye ujuzi wa hiyo biashara. Fikirieni advantage za mfanyabishara wa nishati kuwa kwenye tume ya nishati.

Je Masha kuwa waziri wa Mambo ya Ndani na kuwa mwanahisa wa IMMA ADVOCATES ni wrong?

Kuweni waangalifu serikali inataka wafanyabiashara wasiwe wanasiasa ili kupunguza ushindani, sasa hivi hawataki wagombea binafsi. Wafanyabiashara ni moja ya watu mahiri sana kwa hiyo kuwakataza wasiwe wanasiasa ni disadvantage kwa TZ.
Sheria ya bunge inasema kila mtu ataje mali zake hii ni pamoja shares na kadhalika lakini kwa ajili bunge ni butu kwa hiyo hata mtu asipotaja alimfanyi chochote.Hii sheria ikifuatwa kikamilifu hayo mambo ya conflict of interest ya tatokomea.

Kwa hiyo sheria mpya itakua ni kwa mazumuni ya kuwazui wafanyabishara wakubwa ambao chama kinawaogopa na sio ufisadi.
 
kutoka gazeti la mwananchi - "Baregu alisema inaonekana wazi kuwa Dk Mwakyembe alizuia ununuzi wa mitambo ya Dowans kwa sababu ya mgongano wa maslahi alionao katika sekta hiyo.
Naye mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema mbunge huyo wa Kyela hakupaswa kushiriki katika hoja yoyote ya sekta ya umeme kutokana na kumiliki kampuni hiyo."

Jamani hapa kuna DR na Prof kweli au ndio vyeti vya kwenye internet au ndio wamenunuliwa.
hawaoni advantage za mwakyembe kuwa ndani ya kamati kwa ajili ya uwelewa wake wa mambo ya nishati.
mbona hawasemi masha na IMMA advocates, hawaoni kwamba waendesha mashitaka wanaweza wakawa wanaunganisha na IMMA advocates kupitia masha na kufanya wawe wanashinda kila kesi. this serious (wafanyakazi wa imma RIDHIWANI KIKWETE, fatuma karume(mwanahisa)) ndio maana baadhi ya kesi zao wanashinda kimaajabu
 
Hapa Uk kuna mtu anitwa LORD SAINSBURY, Kuna kipindi alikuwa kamati ya viwanda na bishara na yeye ni mwana hisa mkubwa wa sainsbury supermarket.

Je mwakyembe kujihusisha na biashara ya nishati kumeisaidia bunge kuwa na mtaalamu wa biashara hiyo?
Je mwakyembe kujisisha na nishati kumesaida hata kujulikana hiyo mitambo inauzwa kwa kiasi gani?
Huwezi ukawa na tume nzima hamna hata mtu mmoja mwenye ujuzi wa hiyo biashara. Fikirieni advantage za mfanyabishara wa nishati kuwa kwenye tume ya nishati.

Je Masha kuwa waziri wa Mambo ya Ndani na kuwa mwanahisa wa IMMA ADVOCATES ni wrong?

Kuweni waangalifu serikali inataka wafanyabiashara wasiwe wanasiasa ili kupunguza ushindani, sasa hivi hawataki wagombea binafsi. Wafanyabiashara ni moja ya watu mahiri sana kwa hiyo kuwakataza wasiwe wanasiasa ni disadvantage kwa TZ.
Sheria ya bunge inasema kila mtu ataje mali zake hii ni pamoja shares na kadhalika lakini kwa ajili bunge ni butu kwa hiyo hata mtu asipotaja alimfanyi chochote.Hii sheria ikifuatwa kikamilifu hayo mambo ya conflict of interest ya tatokomea.

Kwa hiyo sheria mpya itakua ni kwa mazumuni ya kuwazui wafanyabishara wakubwa ambao chama kinawaogopa na sio ufisadi.

Semilong,

Usiwe unatoa mifano ambayo huna uhakika nayo, fuatilia ushiriki wa Sainsbury kujua ukweli.
Hapa sheria ziko wazi mno. Hukatazwi kuwa kwenye cheo chochote, unachokatazwa ni kujadili jambo ambalo una interest bila kuzisema.

Wanachofanya UK ni kwamba kama kuna maslahi yako, basi hushiriki kwenye mjadala husika au ukiamua kushiriki ni lazima useme.

Pia standards za hapa ziko juu mno maana huwezi kusajiri kampuni bila kutoa taarifa bungeni. Ukifanya hivyo utakuwa kwenye matatizo makubwa sana.

Msichanganye mambo bure, sheria ya conflict of interest haikukatazi, wala haikuzuii wewe kufanya/kushiriki kwenye kazi yoyote.
 
Mnazungushana maneno tu, I know I am right and you guys are wrong. Mengine ya kuitana majina, kurushiana maneno ni kulazimisha hoja tu. "shame on you, ndumilakuwili, mvuta bangi" n.k is part of the same.

As far as all the evidence has been laid down, Mwakyembe hajavunja sheria yoyote, hajakiuka taratibu yoyote; na hakuwa na pecuniary interests yoyote ya kudeclare wakati wa sakata la Richmond na hata kwenye Dowans sasa hakuna interests yoyote anayoweza kuvuna wakati huu.

Watu wanajaribu kutafuta standard tofauti na iliyowekwa na wabunge wenyewe. Bunge limesema wakati spika anateua wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge anaweza kuangalia uzoefu na ujuzi wa wajumbe katika kamati fulani. Kwa maneno mengine, Daktari anaweza kuwa kwenye kamati ya Afya na Jamaii (wakati pia ana kliniki) na mfanyabiashara (Dr. Kigoda, Dr. Diallo kwa mfano) wanaweza kuwa kwenye kamati ya Fedha na Uchumi.

Jambo jingine ni kuwa watu hawataki kukubali kuwa taarifa anazozipata Mwakyembe kutoka kwenye kamati ya Madini ni public record na mtu yeyote anaweza kuzipata akiwemo Lowassa, Selelii, Serukamba na Kikwete. Siyo siri hivyo Mwakyembe au mjumbe yoyote wa kamati ya Madini hana taarifa kwa kamati ambazo mtu mwingine hawezi kuzipata. As a matter of fact, hata mtanzania mwingine yoyote akitaka kupata taarifa zinazoletwa Bungeni anaweza kuzipata kwa kuwasiliana na Katibu wa Bunge.

Kuna watu wanataka kuwaaminisha watu kuwa nimeshauriana na Dr. kuhusu majibu yake. Wakiulizwa ushahidi hapa watajiuma uma maneno. Kusiwe na utata kwenye hilo. SIJAZUNGUMZA NA DR.MWAKYEMBE kuhusu suala hili hata mara moja tangu lianze. Sijamshauri (kwani sina uwezo wa kumshauri na si mshauri wake). Ukweli ni kuwa hoja zake na za kwangu zinafanana na hilo siyo jambo la kulionea haya au kuogopa kuonekana namtetea.

Ndio maana nimesema Hoja za wazi kwani sina sababu ya kujiuma maneno. I am right and you guys are wrong. Na mna makosa si kwa sababu ni watu wabaya, au mna mchuki au vitu vingine bali kwa sababu hoja zenu zina makosa. It is nothing personal kama watu wanavyotaka kuzigeuza. You arguments are flawed, the premises wrong, the evidence weak, and conclusions illogical.

It is purely that. Call it the supremacy of reason and the arrogance of boldness.
 
What make you to be right each time when you say something?are you so special than anybody can be?Maana aliyotoa mtanzania kuhusiana na pecuniary interests siyo sahihi?

Maneno ya kusema kuwa flani anahisia na kujihisi kuwa wewe umeonga na Dr ,inabaki kuwa siri yako na yeye mwenyewe na hatuna shida ya kujua mlizungumza nini?kumbuka uliongea naye kwenye simu kwa mahojiano na inawezekana kabisa kuna mambo mengine uliyaweka of-record.

Inawezekana na yeye alilia kama Ngeleja kuwa umsaidie kufunika funika,ila kwa kuwa yeye ana staha tofauti na wengine hauwezi kusema alichomkkwambia kuhsusu kumeteta.

Kimsingi haujajibu hoja zaidi ya kupanga maneno tu kwa kuchanga vitu ili hadhira ione umejibu vyema .Bado haujajibu hoja zetu na tusubiri taarifa ya Bunge kwa kuwa Katibu wabunge alishasema kuwa Dr. Alikosea kwa kuwa kuna mgongano wa kimaslahi kutoka na tafsiri halisi ya pecuniary interests!

Mie nimeuliza ,Ni sababu gani ambazo wewe unafikiri ni za msingi kuikataz aTANESCO isinunue mitambo ya DOWANS?

Lets be smart na tuache KUSPIN mambo !

ukifikiria mambo ya kuwezekana kuna watu wanafikiri inawezekana mwezi umetengenezwa kwa jibini.

Kuhusu swali lako la mwisho ni kuwa: Sifikiri sababu za msingi.. NAJUA SABABU YA MSINGI YA KUIKATAZA TANESCO isinunue mitambo ya DOWANS ni kwa sababu kama mama yake Dowans ni kampuni ya kitapeli iliyoingia nchi kwa ulaghai ikiletwa na Kikwete na Rostam wakishirikiana na rafiki yao BRIG. GEN SULEIMAN AL ADAWI. TANESCO isitumie fedha za walipa kodi wa Tanzania kumlipa TAPELI.

Sasa wewe uniambie kwanini fedha za walipa kodi zimlipe tapeli wetu wakati tunajua ni tapeli?
 
Wabunge: Mwakyembe amekiuka maadili, sheria za Bunge
Halima Mlacha
Daily News; Thursday,March 19, 2009 @21:15

Habari nyingine
Matangazo ya Channel Ten hewani
Hakimu mpya wa Liyumba leo
MCT yamruhusu RC kulishtaki gazeti
Sheria ya Maafa kufanyiwa marekebisho
Pinda: Vyama vya wafanyakazi unganeni
TLP yamwengua Mutungirehi TCD
Ajali barabarani zaua watu
Wabunge: Mwakyembe amekiuka maadili, sheria za Bunge
Kondomu ‘zamkaanga’ Papa
Ngongoro yaboresha barabara

Baadhi ya wabunge wameibuka na kudai kuwa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, amekiuka maadili na sheria za Bunge, kwa kuwa mmoja wa wamiliki katika kampuni ya Power Pool East Africa ya kuzalisha umeme wa upepo, wakati yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Wabunge hao wamedai kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na za Maadili ya chombo hicho, mbunge mwenye kampuni au biashara inayohusiana na kamati yoyote ya Bunge, haruhusiwi kuwa hata mjumbe katika kamati hiyo.

Kanuni hiyo ya 61 (1) katika toleo la mwaka 2007 inasema, “wakati wa majadiliano bungeni au kwenye kamati yoyote ya Bunge, mbunge hataruhusiwa kuzungumzia jambo lolote ambalo yeye mwenyewe ana maslahi binafsi nalo ya kifedha.”

Kanuni hiyo inaendelea kueleza, kuwa “isipokuwa maslahi hayo, na kwa sababu hiyo, itakuwa ni lazima kwa mbunge ye yote anayetaka kuzungumzia jambo hilo bungeni au kwenye kamati yoyote ya Bunge, kusema kwanza jinsi anavyohusika na jambo hilo na kutaja kiwango cha maslahi ya kifedha aliyonayo kuhusiana na jambo hilo kabla ya kuanza kuzungumzia jambo hilo.”

Aidha, kanuni hiyo katika kifungu cha (2) inaeleza kuwa mtu yeyote au mbunge, anaweza kumweleza Spika kwa maandishi na kutoa ushahidi kuwa mbunge amezungumzia jambo ambalo ana maslahi nalo binafsi ya kifedha bila kusema jinsi anavyohusika.

Wabunge hao ambao baadhi wamekataa kutaja majina yao wakikataa kuhusishwa na sakata hilo, pia walimwomba Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kupitia upya orodha ya majina ya wabunge walio kwenye kamati mbalimbali za Bunge ili kuwabaini walio kwenye Kamati ambazo zinaweza kuwasababishia mgongano kimaslahi.

Akizungumza na gazeti hili, kwa masharti ya kutozungumzia chochote kuhusu Dk. Mwakyembe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alikiri kuwapo kwa sheria hiyo ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa wajumbe wanakuwa hawana mgongano wowote kimaslahi ili kutoingilia katika uamuzi wa kamati hiyo.

“Sheria iko wazi, kitendo cha Mwakyembe kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Madini, ambayo inatunga sera na ambayo inakutana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa mujibu wa sheria hii kinaleta mgongano wa kimaslahi,” alisema Kabwe.

Alisema hiyo ni kutokana na ukweli kuwa si rahisi kwa Watanzania kutenganisha maslahi ya mjumbe wa kamati au kiongozi wa kamati, mwenye kampuni yenye kuhusiana na kamati na uamuzi halisi wa kamati husika au taasisi ya Serikali husika akitolea mfano wa Tanesco.

Naye mmoja wa wabunge ambaye alikataa katakata jina lake kutajwa gazetini, alisema kwa mujibu wa taarifa zilizopo kampuni hiyo ilisajiliwa mwaka 2004 na kuna taarifa kuwa mwaka juzi ilianza mazungumzo na Tanesco ili kuanza kusambaza umeme.

“Katika hali ya kawaida, huwezi kuwa mjumbe wa kamati licha ya Makamu Mwenyekiti, ikiwa tayari una kampuni iliyofikia hatua hiyo ya kusajiliwa na mazungumzo tayari kuanza. Huku ni kwenda kinyume na maadili,” alisema mbunge huyo.

Alisema ndiyo maana imewekwa sheria ya wabunge kuorodhesha mali zao, ili kumrahisishia Spika kupanga kamati ili kuepuka matatizo kama hayo, ambayo yanaweza kusababisha baadhi ya wajumbe wenye migongano ya kimaslahi, kuingiza maslahi yao katika uamuzi wa kamati.

Gazeti hili lilizungumza na Naibu Spika Anne Makinda, ili kupata undani wa sheria hiyo, hata hivyo alisema yuko njiani anasafiri hivyo hawezi kuzungumza chochote kuhusu suala hilo. Mnadhimu wa Bunge kwa upande wa Serikali, Philip Marmo, alisema hana taarifa za tukio hilo kwa kuwa yuko kijijini kwao, ambako hakuna hata redio, hivyo hawezi kulizungumzia. Spika wa Bunge Sitta na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, hawakuweza kupatikana kutokana na simu zao kutopatikana.

Juzi, Dk Mwakyembe alipozungumza na waandishi wa habari, alikanusha kwamba kuwa kwake na hisa katika kampuni hiyo ya kuzalisha umeme wa upepo, kunamsababishia mgongano wa kimaslahi kwa kuwa bado kampuni hiyo iko katika mradi na haijaanza kuzalisha nishati hiyo. Alisema iwapo mradi huo utaanza kuzalisha umeme, atachagua aende wapi, kwenye ubunge au kuwa mfanyabiashara. “Lakini naamini kuwa ubunge si kazi ya kudumu japo kwa upande wangu sina ukomo na kazi hii, ila ifahamike kuwa sina mkataba na Bunge,” alisema.
 
Mhhhh just wonderinmg, hivi mbona Mwambalaswa, ambaye naye ni mwanahisa wa hiyo kampuni na mjumbe wa kamati ya nishati na madini aandamwi kama Mwakyembe? Au yeye hana maslahi?

Mwambalaswa akiwa kama mwanahisa wa kampuni ya kufua umeme kwa upepo hastahili kuwa mjumbe wa board ya Tanesco ; nadhani baada ya sokomoko hili hatangoja kufukuzwa ujumbe bali atajiuzuli mwenyewe!!
 
Mwanakijiji,

Hivi umeshawahi kumpinga Dr. Mwakyembe? Ni swali tu la kutaka ku establish neutrality yako. Tusije kuwa tunabishana na campaign manager wa Mwakyembe bure.
 
Back
Top Bottom