UTENGUZI: Rais Samia awatumbua Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TASAC, Posta na Posta Masta. Avunja Bodi ya Wakurugenzi Posta

Website ya TASAC mpaka leo tarehe 4 May 2021 inaonesha kuwa hao ni wajumbe wa bodi. Rejea linki Wajumbe wa Bodi |Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania na kama ni wastaafu inaonesha jinsi TASAC ilivyo na uzembe katika ku update taarifa zao za mtandaoni na kutia shaka kama kampuni hii ya umma inaweza kuwasiliana na wateja wao ki- dijitali kuendesha shughuli zao kwa ufanishi na kiushindani.

Soma zaidi.

Wasiliana Nasi​

Kurasa za Karibu​

Tovuti Mashuhuri​

Ungana nasi kupitia​

2021 TASAC . Haki zote zimehifadhiwa.
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Inaendeshwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
Source : Wajumbe wa Bodi |Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
Tarehe 04 May?,mwenzetu unaishi sayari gani?
 
14 Julai 2016

Msuguano wa Fikra Ni Muhimu asema Kanali Mstaafu:

Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo


Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Ramadhani Kondo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo amewaasa watanzania kuchukua tahadhari na watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwa kuwaaminisha wananchi kuwa maandamano na vurugu ndio demokkrasia na ukombozi wa umaskini wetu.

Kanali Kondo alisema kuwa watu wa aina hiyo ni wakuogopwa kama ukoma kwani ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu ambapo tunashuhudia vurugu, vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali duniani na madhara yake.

“watanzania tuchukue taadhari ya watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwani kumekuwa na watu wanaotuhamasisha ya kuwa maandamano na vurugu ndiyo ukombozi wa umaskini wetu hivyo tunapaswa kuchukua taadhari na kukataa hadaa hizo” alisema Kanali Kondo.

Vilevile aliongeza kuwa, roho mbaya imechangia taifa letu kudumaa kimaendeleo kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wetu wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa umma, wasomi na wananchi wa kawaida.

Aidha,alifafanua kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais John Pombe Magufuli amechukua hatua ngumu ya kupambana na vitendo vya rushwa, ubadhilifu na ufisadi kwani kitendo hicho kimewaudhi mafisadi na mawakala wanaopotosha ukweli na kuendesha propaganda chafu dhidi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano
 
Toka maktaba
6 November 2016

Ufisadi wagubika Shirika la Posta​


Luteni Kanali mstaafu, Dk. Haroun Kondo

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Luteni Kanali mstaafu, Dk. Haroun Kondo ameamuru mikataba yote iliyoingiwa na shirika hilo ipitiwe upya, baada ya kubaini baadhi ni mibovu.

Mbali na hayo, watumishi wote wa shirika hilo watahakikiwa upya ili kubaini wafanyakazi hewa na waliofanya udanganyifu katika uhakiki wa kwanza.

Dk. Kondo, alisema hayo jana alipokutana na bodi ya wakurugenzi kupitia majukumu waliyopewa baada ya bodi hiyo kuzinduliwa Oktoba, mwaka huu.

“Mashirika ya umma yamejiingiza katika mambo ambayo huwezi kuamini, yamesababisha mashirika kukwama, wazawa wanafanya mambo kama nchi si yao, yanayofanywa na Watanzania yanaogopesha.

“Kitu cha Sh milioni 25 watu wanaandika bilioni, kuna watu wezi Posta, wabadhirifu wanakula fedha, wakubwa waliopewa dhamana ndio tatizo wameifikisha nchi pabaya kazi kulalamika tu.

“Watanzania hawana uoga wanaingia mikataba ya ovyo kila sehemu wanaingiza siasa, waliozoea kufanya mambo ya ovyo, sasa tunasema basi, mashirika yamejaa rushwa na watumishi hewa.

“Ninazo taarifa za Posta tukae tujiangalie tuko wasafi kiasi gani, mashirika yameathiriwa zaidi na watendaji,wengine baada ya kufanya kazi wanazungumza tu hawajulikani wanafanya kazi gani,”alisema.

Dk. Kondo, aliitaka bodi kushirikiana kila mmoja kwa sehemu yake kuhakikisha wako wasafi, yasiwapo mazingira ya kulindana.

“Kuna mikataba mingi mibovu, watu hawana aibu wanasaini, kuna mkataba uliingiwa na TPC Plot namba 416, jengo la ghorofa tatu lililopo jirani na jengo la mawasiliano, kuna kipengele kinaeleza mkataba huo ni wa milele.

“Mikataba mingi wanayoingia hawana uchungu na nchi, mikataba mibovu ipo mingi, naagiza mikataba yote mipya na ya zamani iangaliwe upya, tukibaini ina upungufu tunaikataa,”alisema.

Alisema jengo hilo la ghorofa tatu lina vyumba sita, mpangaji analipa pango kwa mwezi Sh 1,800,000 ambapo kila ghorofa kwa mwezi Sh 600,000.

Alisema pango hilo kwa miaka mitatu mpangaji atakuwa kalipa Sh milioni 64.8, lakini yeye kawasilisha taarifa ukarabati aliofanya katika jengo hilo umegharimu Sh milioni 398.7.

“Kodi ya Sh milioni 1.8 kwa mwaka katika gharama hizo za ukarabati, mteja atakaa miaka 20 bila kulipa kodi ya pango,” alisema na kuongeza kwamba lazima mikataba iangaliwe upya.

Akizungumzia wafanyakazi hewa, alisema katika uhakiki wa awamu wale wenye vyeti feki inadaiwa waliviondoa ili wanusurike.

“Tutaanza kuwafanyia uhakiki upya wafanyakazi wa Posta, Hazina inatoa fedha wafanyakazi hawapo,”alisema.

Alisema kutokana na kukua kwa teknolojia lazima wajifunze kutoka kwa wenzao ambapo wao walikwenda nchini Kenya
 

Toka maktaba :​

DK.KONDO APONGEZA JITIHADA ZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA KUJENGA UMOJA.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Kondo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya<endela bofya kichwa cha habari hii juu> harakati ya Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, katika jitihada alizofanya za kujenga nchi na kuleta maendeleo kwa watanzania bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, rangi na jinsia watanzania hivyo tumuombe Mungu ampe afya nguvu ujasiri hekima na busara katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Waandishi wa habari wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Kondo leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka
 
Hivi Mzee Mkinga hayupo kwenye hizi bodi? Yule mzee alikuwa mwanaharakati mzuri sijui kilimkuta nini akaufyata enzi za Magufuli baada ya kupewa ujumbe wa bodi kama zawadi
 
17 June 2020

TPC) LATOA TAARIFA YA MAFANIKO NA MATARAJIO YA SHIRIKA KWA MWAKA 2019/ 2020​



Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mafanikio na matarajio ya shirika hilo, kwa mwaka 2019/2020, mara baada ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka, (2nd Annual General Meeting), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akisisitiza jambo

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya mkutano huo. Kulia waliokaa ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bibi Kitolina Kippa na Mwakilishi wa Msajili wa Hazina, Bw. Elikana Mtumweni. Aliyesimama kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TCRA), Bw. Wilfred Maro.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, katika picha ya pamoja na menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania.

Habari kwa hisani kubwa ya: https://hakipensheni.blogspot.com/2020/06/shirika-la-posta-tanzania-tpc-latoa
Usitarajie mafanikio hapo
 
Nchi hii hata ateuliwe malaika, ataiba tu......kinachofanyika ni kubadilisha muonekano wa chupa tu ila mvinyo ni uleule tu
Unawaza kama mimi. Kinachobadilishwa mafisadi tu. Badala ya fisadi A anawekwa fisadi B. Mfumo wa uteuzi na utendaji kazi Tanzania unaacha loopholes nyingi sana za upigaji. Bila kufumua system yote na kuifanya ''ufusadi proof'' kwa kadiri inavyowezekana ni kazi bure. Sehemu kama mashirika na taasisi za umma tubadilishe mfumo kabisa. Kwa mfano hawa wanaoitwa mwenyekiti na wajumbe wa bodi ni wa kuondoa na kuweka mfumo wa aina nyingine kwani wao ni moja ya machaka ya upigaji.
 
Back
Top Bottom