Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Nenda Sido iliyo karibu nawe utapata details zote za machine na malighafi pamoja na procedure za TBS na wengineo.

Kuhusu soko inategemeana na lengo lako maana kuna soko la ndani ambalo huanzia mtaani kwako, wilaya mkoa kanda taifa na afrika mashariki.

Soko unalitafuta la jumla na rejareja kwenye maduka madogo mtaani, wanunuzi wakubwa Wale Wa jumla, supermarkets, n.k.

Ikumbukwe kuwa matumizi ya sabuni yapo kila siku katika kila familia kuanzia kuogea, kufulia, kuoshea vyombo, kudekia, n.k

Kikubwa utengeneze sabuni yenye ubora kwa maana ya povu jingi, uwezo Wa kuhimili maji magumu, ugumu Wa kuisha lakini pia manukato na rangi za kuvutia.

Karibu katika Tanzania ya viwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa, mda mwingne inabid wati waache kuwasikiliza hao wanaojihita wasomi sasa kwe upande wa sabuni inahitajika research ya nn ya soko, soko la sabuni ni pana sana na nirahisi sana mradi tu uwe na product nzuri, soko kubwa kwanza ni mtaani kwako au mji wako, anza na vile tuviduka vya kina Mangi, sambaza mzigo leo wape siku moja kakusanye ela ndio tunavyofanya biashara sasa kwa hal hii, alafu ukitaka kuwin kwa haraka ktk biashara hii hakikisha kwanza unapata malighafi kwa bei na fuu mfno kwa sabun za kipande hakikisha unapata mafuta kwa bei nafuu, pia hakikisha product ni nzur lzm utapiga hela tu na sabuni inahela sana hasa ya kipande, na ukitaka utoboe haraka nenda kwe miji au wilaya zilizo mbal na jiji la Dar, sababu weng wao hawana marifa kuhusiana na sabun ukiwambia unaweza kutengeneza ww mwenyewe wanakushangaa wanaona kitu cha ajabu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu mna roho nzuri syo hao wa ni pm hongera mkuu ku share
Nenda Sido iliyo karibu nawe utapata details zote za machine na malighafi pamoja na procedure za TBS na wengineo.

Kuhusu soko inategemeana na lengo lako maana kuna soko la ndani ambalo huanzia mtaani kwako, wilaya mkoa kanda taifa na Afrika mashariki.

Soko unalitafuta la jumla na rejareja kwenye maduka madogo mtaani, wanunuzi wakubwa Wale Wa jumla, supermarkets, n.k.

Ikumbukwe kuwa matumizi ya sabuni yapo kila siku katika kila familia kuanzia kuogea, kufulia, kuoshea vyombo, kudekia, n.k

Kikubwa utengeneze sabuni yenye ubora kwa maana ya povu jingi, uwezo Wa kuhimili maji magumu, ugumu Wa kuisha lakini pia manukato na rangi za kuvutia.

Karibu katika Tanzania ya viwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pelham,hata mimi nilikua na wazo juu ya kiwanda hiki,unaweza ni PM nikupe clue nilipofikia juu ya utafit wangu,,tunaweza chochote.
Mr tulio na project hizi tupo wengi je wote tuku PM wote?
Kwanini usi share nasi?
 
Mkuu Pelham,hata mimi nilikua na wazo juu ya kiwanda hiki,unaweza ni PM nikupe clue nilipofikia juu ya utafit wangu,,tunaweza chochote.
We uko wap ,mm nilipata mafunzo ya utengenezaji sabuni za magadi hvi nipo ktk hatua za mwisho kuna mdau wangu nasubiri apate pension tuamshe popo hvyo tungeshare utafiti wako wasoko ingependeza zaidi
 
Hongera kwa mawazo mazuri iko hivi gharama sio kubwa inategemea unaanza na production ya ukuwa gani nakushauri anza kidogo kutegemea na soko lako na pia kwakuwa unaanza kutengeneza itakusaidia kwenye improvement mana utakuta ulikosea kitu au ulizidisha materials simply unaweza anza na 50,000.

Materials ni:

Mafuta dumu la 20litre linauzwa 38,000, caustic utachukua ya kupimiwa interm of kg, blue kwa ajili ya kuipa sabuni rangi zile tunaweka kwenye mashati kipindi hicho wahenga hahhahhah zipo feki na og Ila utadadisi, perfume kwa ajili ya harufu kuna za aina tof. Mfano ya lemon ni we we tu hapo harufu isiyokera muhimu, then hydrometer vifaa unatakiwa uandae vifuatavyo jaba au beseni kubwa ya kukorogea na ubao wa kumwagia mkorogo I mean ujiuji hapa inabidi umtafute fundi seremala akudizainie kibao chenye vyumba vya bars kwa idadi yako unayotaka simple 80 to 100 bars inatosha kishkaji.

Udambwiudambi usisahau kachapa kako

Changamoto zipo sana sana soko sasa hivi watengenezaji ni wengi wakubwa kwa wadogo sabuni ni nyingi pia wapo wanaoagiza kigoma direct sababu kule materials ndo nyumbani hivyo bei imedrop na itadrop sana halo mbeleni wako wanaozalisha mzigo wa kujaza canter wengi tu sasa hivi bei maeneo mengi kwa dar ni Tsh. 25,000 kwa katon ya sabuni 20 wewe huko mnapouza 30 elfu ni wapi au kwa mangi dukani na tatizo LA soko ni pale unapozalisha mzigo mkubwa mfano wa kujaza canter so itakulazimu uuze jumla kwa watu wa jumla bei itakuwa chini so itaminya kafaida.

Halafu ujue sabuni za magadi hazitumiki kivile kama za kawaida kina white wash na ndugu yake jamaa matumizi yake ni local limited.

Changamoto nyingine wapo wanaoproduce feki wanaharibu soko hawa watu.

Muhimu ingia YouTube jifunze zaidi then ingia mzigoni tengeneza kwa ajili yako kwanza hata bar moja then angalia ubora na uimprove kabla hujaanza kuuzia watu maana kwenye mix unaweza zidisha au kupunguza vitu sabuni ikatoka zaidi ya jiwe,laini sana,iwe inaisha haraka na mwisho iwe inamuwasha mtu pindi atumiapo.

Mwisho, ujitahidi kwenye kutafuta masoko endelevu maana kuna watu walisarender kwenye hii ishu. Asante
 
Hongera kwa mawazo mazuri iko hivi gharama sio kubwa inategemea unaanza na production ya ukuwa gani nakushauri anza kidogo kutegemea na soko lako na pia kwakuwa unaanza kutengeneza itakusaidia kwenye improvement mana utakuta ulikosea kitu au ulizidisha materials simply unaweza anza na 50,000.

Materials ni:

Mafuta dumu la 20litre linauzwa 38,000,caustic utachukua ya kupimiwa interm of kg,blue kwa ajili ya kuipa sabuni rangi zile tunaweka kwenye mashati kipindi hicho wahenga hahhahhah zipo feki na og Ila utadadisi,perfume kwa ajili ya harufu kuna za aina tof. Mfano ya lemon ni we we tu hapo harufu isiyokera muhimu, then hydrometer vifaa unatakiwa uandae vifuatavyo jaba au beseni kubwa ya kukorogea na ubao wa kumwagia mkorogo I mean ujiuji hapa inabidi umtafute fundi seremala akudizainie kibao chenye vyumba vya bars kwa idadi yako unayotaka simple 80 to 100 bars inatosha kishkaji.

Udambwiudambi usisahau kachapa kako

Changamoto zipo sanasana soko sasa hivi watengenezaji ni wengi wakubwa kwa wadogo sabuni ni nyingi pia wapo wanaoagiza kigoma direct sababu kule materials ndo nyumbani hivyo bei imedrop na itadrop sana halo mbeleni wako wanaozalisha mzigo wa kujaza canter wengi tu sasa hivi bei maeneo mengi kwa dar ni Tsh. 25,000 kwa katon ya sabuni 20 wewe huko mnapouza 30 elfu ni wapi au kwa mangi dukani na tatizo la soko ni pale unapozalisha mzigo mkubwa mfano wa kujaza canter so itakulazimu uuze jumla kwa watu wa jumla bei itakuwa chini so itaminya kafaida.
Halafu ujue sabuni za magadi hazitumiki kivile kama za kawaida kina white wash na ndugu yake jamaa matumizi yake ni local limited.

Changamoto nyingine wapo wanaoproduce feki wanaharibu soko hawa watu.

Muhimu ingia YouTube jifunze zaidi then ingia mzigoni tengeneza kwa ajili yako kwanza hata bar moja then angalia ubora na uimprove kabla hujaanza kuuzia watu maana kwenye mix unaweza zidisha au kupunguza vitu sabuni ikatoka zaidi ya jiwe,laini sana,iwe inaisha haraka na mwisho iwe inamuwasha mtu pindi atumiapo.

Mwisho ujitahidi kwenye kutafuta masoko endelevu maana kuna watu walisarender kwenye hii ishu. Asante
Vipi sabuni za kuogea zina changamoto pia? Na mafuta ya kupaka?
 
Unatengeneza mwenyewe au?
Vipi sabuni za kuogea zina changamoto pia? Na mafuta ya kupaka?
Sabuni za kuogea ni deal ukiwa na products zenye ubora na ukiwin Penetration ya soko. Kuna Dada mmoja nilimuona YouTube anatengeneza hela balaa anadeal na sabuni za kuogea na mafuta ya nywele.

Mafuta yakupakaa sina idea ila kuna kuna binti fulani wa chuo alikuwa anatengeneza under sido aliwahi niletea nilinunua nikamuuliza vip biashara akasema ngumu sana
 
Wakuu habari za leo, heri ya siku kuu ya Eid. Natumaini mu wazima, buheri wa afya.

Lengo la uzi huu ni kupeana elimu juu ya utengenezaji wa sabuni, kwa ajili ya matumizi mbalimbali (ya nyumbani na maofisini) kama vile kufuria, kuoshea vyomba na mengineyo sambamba na hayo.

Kwa wale wenye ujuzi juu ya suala hilii mnakaribishwa ili tupeane idea ili tuweze kujikwamua kwa namna moja au nyingine.

Elimu itakayotolewa hapa izingatie:

1. Aina ya sabuni (ya dawa/kawaida/unga)
2. Mahitaji kwa ajili ya kuanza kutengeneza
3. Hatua za utengenezaji
4. Soko (walengwa wa ununuzi/watumiaji )

Usisite kuchangiaa Kama unafahamu lolote juu ya utengenezaji, toa elimu hapaa pia maswali yanakarbishwa.

Tuwezeshanee wakuu. Pamoja tunajenga taifa letu.

Asantenii, naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom