Utengenezaji wa sabuni za maji

The Tai

Member
Dec 9, 2019
6
14
JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI ZA MAJI

Katika harakati zetu za utafutaji wa pesa leo ninaomba tuzungumzie kuhusu utengenezaji wa sabuni.Sabuni hizi unaweza kuzitumia katika kufulia,kuogea,kuoshea vyombo na kusafishia chooni.Sabuni hizi unaweza kutumia kwa matumizi yako ya nyumbani au kuuza maeneo mbalimbali.Sasa tuangalie namna tunaweza tengeneza sabuni za maji

MAHITAJI:(Materials)

SULPHONIC ACID LITA 1

SODA ASH ROBO KILO

SLESS/UNGAROL LITA 1

GRYCELINE VIJIKO 5 VYA CHAKULA

RANGI KIJIKO 1

CHUMVI KILO 1

TIGNA GRAM 250 ( inategemea Aina ya tigna Kama ya hapo kwa hapo au ya kulaza ktk maji)

PERFUME ROSE

CDE MILS 200

MAJI SAFI LITA 30

--------------------------
KUTENGENEZA

Hatua 1

Chukua maji lira 30 gawa mara 2 kwa ulingano ulio sawa.Katika chombo kimoja weka tigna yote koroga hadi kupata uji mzito kisha weka kando.

Hatua 2

Weka sulphonic acid katika chombo kisha Tia Soda ash.Koroga vyema hadi kupata kitu kama ugali.Hakikisha unakoroga vyema kwa muda usiopungua dakika 15 bila kupumzika.

Hatua 3

Ongeza sless na kisha koroga vyema kwa dakika kumi kisha weka maji lita 15 ya kwenye chombo kingine ambayo hukuyaweka tiga kisha koroga hadi ugali wote uishe.
Hatua 4

Weka maji yenye tigna,koroga vyema kisha ongeza rangi, glycerin,cde na kisha weka chumvi.Baada ya kuweka chumvi koroga kuelekea upande mmoja mpaka iyeyuke yote kabisa maana ukikoroga kwa kuchanganya upande sabuni yako haitakuwa laini na povu la kutosha.

Hatua 5

Weka perfume na koroga kwa dakika tano kisha iache kwa muda fulani kutokana na aina ya tiga ukiyotumia baada ya hapo sabuni yako ipo tayari kwa ajili ya matumizi.

NOTA BENE:
1.Kama unataka kutengenza kwa ajili ya biashara nakushauri amza kutengeneza sample( sampuli) kidogo jaribu kutumia wewe nyumbani kwako,wape marafiki au hata jamaa zako watumie bure halafu wakupe mrejesho.

2.Perfume ya sabuni sio lazima iwe na harufu ya rose unaweza kuchagua harufu uipendayo wewe.

3.Unaweza tengeneza sabuni za rangi mbalimbali uzipendazo.

4.Sikuwahi kufanya biashara ya kutengeneza sabuni za maji maana tulikuwa tunatengeneza kwa ajili ya matumizi ya shule basi hivyo sijui sijui gharama za kununua vitu vinayohitajika wala mchanganuo wa faida.Ninakuomba mpwendwa msomaji kama utapenda kufanya biashara ya uuazaji wa sabuni nakushauri ufanye utafiti kwa wauzaji waliokutangulia ili na wese uweze kuanza biashara hii japo nimejaribu kuuliza nimeambiwa gharama za kununua mahitaji ya kutengeneza sabuni sio ghali na wanasema ukifata vipimo vinavyotakiwa unaweza tengeneza angalau faida nusu ya mtaji wako.

5.Utakapoanza uuzaji wa sabuni basi anza na mtaani kwako,majirani,marafiki na wafanyakazi wenzako hao ndio watakuwa wateja wako wa kwanza halafu tafuta mahali kwenye duka pana wateja wengi ongea na mwenye duka uweke bidhaa zako.

6.Hata kama biashara ni ndogo lakini ifanye kiuweledi ili kuvutia wateja zaidi, nakushauri utengeneze brand yaani logo na label ya kubandika kwenye bidhaa zako za sabuni.

7.Wateja wako pia watukuwa ni taasisi mbalimbali za binafsi na serikali kama vike shule,vyuo,taasisi za dini au hata hospitali mbalimbali hivyo nakushauri ili uweze wapata wateja kama hawa ni lazima uwe umesajiliwa na serikali.

#We_all_gonna_make_it (WAGMI) ✊✊
 
Chumvi haipunguzi povu? na je nikiongeza sulfuric acid haiwezi kuwa dawa ya kusafishia vyoo vyenye uchafu sugu?
 
Ukiongeza hiyo Sulphuric acid inaondoa madoa sugu yoote. Ila uwe na kipimo maalumu maana huwa ona tabia ya kuondoa grout (kwa vyoo vya tiles) kama ukiweka nyingi sana.
 
Mi umenichanganya kidogo katika hatua ya uchanganyaji!

Hapa unatoa formula ya utengenezani sabuni ya maji, lakini katika hatua ya utengenezaji nimeona tunasonga kama ugali na kitu kinaenda kuwa "solid".

Je ni hatua gani inayotupeleka kurejea kwenye liquid?

Maelezo ya step 3 yanachanganya sana pia kwa wafuatiliaji.
 
Back
Top Bottom