Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Wakauu,

Kuna changamoto moja nakumbana nayo katika utengenezaji wa sabuni ya mche nayo maji kujitenga chini na mafuta kuwa juu

Mara ya kwanza nilitumia mawese na mara ya pili nilitumia mise hali ikawa ni ileile
Naomba msaada nifanyeje ili maji yasijitenge na mafuta?

Na swali la pili niongeze nini ili sabuni iwe na mapovu mengi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF

Naomba msaada kwa mwenye ufahamu au uzoefu wa kutengeneza sabuni za kigoma maatufu kama gwanji au sabuni za magadi maana nataraji kufungua kiwanda kidogo nyumbani kwangu hapa jijini Dar, maana kwa utafiti wangu sabuni miche 20 = sh 30,000 hivyo nataka kujua gharama ya uzalishaji na changamoto zake, natanguliza shukrani kwa wote mtakao toa michango ya mawazo na mtabarikiwa.

Amen
 
Mkuu chakwanza uwe Na mafuta ya mise sio mawese baada ya hapo blue hii yanguo +sodium bicarbonate nahisi kama sio calcium bicarbonate kati ya hizi chemical mbili unachemsha mafuta yako maana hua yanaganda then unayamwagia kwenye jaba yakianza kupoa unaongeza Kwa juu hio calcium carbonate kama si sodium bicarbonate mpaka ianze kuwa ya uji uji then unaimwagia sehem yako yakutengenezea mpaka itakapo kua solidified
 
Mkuu chakwanza uwe Na mafuta ya mise sio mawese baada ya hapo blue hii yanguo +sodium bicarbonate nahisi kama sio calcium bicarbonate kati ya hizi chemical mbili unachemsha mafuta yako maana hua yanaganda then unayamwagia kwenye jaba yakianza kupoa unaongeza Kwa juu hio calcium carbonate kama si sodium bicarbonate mpaka ianze kuwa ya uji uji then unaimwagia sehem yako yakutengenezea mpaka itakapo kua solidified
Asante kaka
 
MAHITAJI
1. Sulphonic(LABSA)
2. Slec
3. Pafyumu (lemon)
4.Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
5. Chumvi nzuri ya mawe.
6.Glycerin
7.Soda ash light.
8 .Formalin na alka.
9. Maji yaliyokuwa safi .
10. Chombo zaidi ya lita 25.

JINSI YA KUTENGENEZA

1. Chukua sulphonic 1 lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea (lita 25)

2. Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.

3. Chukua soda ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni, kisha chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wasulphonic na sles weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.

4. Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi kutokana na rangi unayoitaka lakini angalia isizidi sana koroga tena vizuri.

5. Kisha chukua glycerin vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana.

6. Kisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.

7. Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai kisha mimina katika mchanganyiko wako naKisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri

NB: Chumvi ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.

8. Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka formalin kisha koroga tena vizuri (alka na formalin sio lazima sana hata kama hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).

ANGALIZO

1. Mchanganyiko wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.

2. Kuna baadhi ya malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama Maski na Gloves.
 
Sulphonic, alka, soda ash, slec na formalin znapatkana kwa maduka ya namna gan? Msaada tafadhali, nataka niifanyie kazi
 
Asante mkuu,

Ila hapo kwenye vijiko viwili mpk vitatu vya rangi ni vingi sanaa, mimi natengeza lita arobaini lakini rangi hata kijiko hakijai ishakolea, ile rangi inakolea haraka sana ukiweka nyingi inakuwa km uchafu.
 
Ndio maana huwa nanunua sabuni za waturuki au viwanda vikubwa vya hapa Tz. Wajasiliamali wa Tz wanaangalia hela tu kuliko afya ya mtumiaji.
 
Ndio maana huwa nanunua sabuni za waturuki au viwanda vikubwa vya hapa Tz. Wajasiliamali wa Tz wanaangalia hela tu kuliko afya ya mtumiaji.
Mkuu mi nadhani hujamuelewa kamaanisha vifaa ambavyo ni sumu ni zile materials ambazo hutumika kutengeneza sabubni ila ikiwa tayari kwenda kwa mtumiaji sio sumu tena.
 
Pelham 1,

Bila shaka tangu 2014 utakuwa umeshatekeleza project yako kwa kiasi kikubwa.

Sio vibaya ukatupa uzoefu wako ikawa kama mrejesho na wengine wajifunze kitu japo ni kama hukupa majibu hapa ila naamini project hii haikuishia njiani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pelham,hata mimi nilikua na wazo juu ya kiwanda hiki,unaweza ni PM nikupe clue nilipofikia juu ya utafit wangu,,tunaweza chochote.
Nenda Sido iliyo karibu nawe utapata details zote za machine na malighafi pamoja na procedure za TBS na wengineo.

Kuhusu soko inategemeana na lengo lako maana kuna soko la ndani ambalo huanzia mtaani kwako, wilaya mkoa kanda taifa na afrika mashariki.

Soko unalitafuta la jumla na rejareja kwenye maduka madogo mtaani, wanunuzi wakubwa Wale Wa jumla, supermarkets, n.k.

Ikumbukwe kuwa matumizi ya sabuni yapo kila siku katika kila familia kuanzia kuogea, kufulia, kuoshea vyombo, kudekia, n.k

Kikubwa utengeneze sabuni yenye ubora kwa maana ya povu jingi, uwezo Wa kuhimili maji magumu, ugumu Wa kuisha lakini pia manukato na rangi za kuvutia.

Karibu katika Tanzania ya viwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom