Utendaji wa Rais Magufuli: Chama cha Mapinduzi chamjibu Lowassa

Utendaji wa Rais Magufuli: Chama cha Mapinduzi chamjibu Lowassa

Hata nyumbu(chadema) wanaona alichokiongea nyumbu mwenzao ni ujinga ndio maana wamejikalia kimya pale unapotegemea mtu unaempenda na kumwamini kuwa ana upeo mkubwa harafu anaongea pumba kama mzee wetu ni shida sana aisee ndio huyu mlitaka awe rais au mliongelea rais wa mafisadi na majizi
Hapo mi mwenyewe mamvi kanichosha kweli..
 
BARCLAYS
AU VODACOM LEAGUE
 
Km si ukichaaaa basi Ole kachanganyikiwa, taarifa yanini kwa vyombo vya habari ili rais wa mioyo ya watu alikuwa akiongea na watu wake, hayo ni mawazo yake anatakiwa ayaheshimu, asitake kiki kupitia rais wetu
 
Nafurahi kuona kuna watanzania bado wanataka mabadiliko ya kimfumo, mizizi ya ccm lazima itoke na itupiliwe mbali ili tz ipate mwanga mpya. CCM walifikiri Pombe atawaokoa kumbe sivyo. Mawazo yangu haya yanatokana na michango ninayo iiona ktk mitandao ya kijamii mbalimbali.
 
Ni kweli hatuna tatizo la mfumo? Naona kama ni personal attack kuliko majibu ya maoni ya anayejibiwa. Katika taarifa iliyoandikwa na gazeti sijaona uzito wa kauli za Mh Lowassa kuzungumzia wanaochishwa kazi kwa ufisadi bali hatua zinazochukuliwa kusababisha makampuni kuounguza au kufunga shughuli na kuachisha au kupunguza wafanyakazi. Pengine kauli hiyo aliitoa lakini iliyoandikwa ni tofauti na iliyojibiwa.
Hatua ipi mbaya inayofanya watu kupunguza wafanyakazi? Hebu tuache siasa tuseme ukweli. Kwahiyo hata HSC wamo? Maana wafanyakazi walipigwa chini pia ...mabadiliko hayaji kirahisi ndugu ...
 
Vipi kuhusu Raisi kufanya kazi ya Bunge ya kupanga matumizi ya fedha za serikali?
Rais hajawahi kupanga matumizi ya fedha labda mtupe mfano. Rais anachofanya ni kubadilisha matumizi ya pesa ambazo zinatolewa kwa shughuli anazoona yeye ni za anasa au zisizokuwa na umuhimu kwenda kusaidia kumaliza matatizo yanaogusa jamii.

Mfano badala ya kurusha ndege za vita, kuandaa magwaride na kugida katika nyadhifa za sherehe za kitaifa, fedha kutumika ktk ujenzi wa barabara. Badala ya kula na kunywa sherehe za siku ya ukimwi, pesa kusaidia kununua madawa kwa ajili ya waathirika n.k.

Hii ni sawa na mtu kupewa pesa za tuzo ya mfanyakazi bora. halafu mtunzwani akaamua pesa aliyopewa wasaidiwe wafanyazi waliopata ulemavu wakiwa kazini. Hapo hujapanga matumizi bali umebadilisha matumizi ya pesa zilizopangwa kwa ajili ya shughuli nyingine.
 
Awamu iliyopita wapinzani walikuwa mbele chama tawala nyuma.
Awamu hii chama tawala mbele upinzani nyuma.
 
fisadi liende kuchunga ng,ombe uko limuache raisi afanye kazi yake,,, kila mtu ataguswa
 
Nu kweli Lowassa kasahau kuwa akiwa PM alifukuza sana watu kwa kutaka sifa. Zilikuwa mbwembwe za kwenye media. Wengi aliowafukuza waliendelea na kazi.
 
Mabadiliko Lowassa
Hahaha huu wimbo ulibamba sana
Haya sasa ona anavyopinga Mabadiliko ya kiutendaji
 
Chama cha mapinduzi CCM kimekanusha kauli iliyotolewa na aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema EDWARD LOWASSA kuwa utaratibu wa kutumbua majipu na kuwachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali imetokana na tatizo la mfumo nchini.

Ole Sendeka
Msemaji wa CCM
Ofisi Ndogo Ya CCM- Lumumba
 
Mzee Sendeka siyo tatizo hapa. Amemkumbusha tu mzee mwenzake Lowassa tabia zake wakati akiwa Waziri Mkuu. kama hujui, waulize wale waliopata kali yake. Kwa kumbukumbu moja, alikuwepo Mkuu wa Wilaya ambaye kijeshi alikuwa na cheo kikubwa kuliko cha Lowassa ambaye hakumtolea uvivu kwa kumweleza kuwa alikuwa amefanya kazi ya Ukuu wa Wilaya kwa miaka mingi na kwamba Lowassa asingeweza kumfundisha namna ya kufanya kazi hiyo. Hakuna kama tuko hilo lilisaidia kupunguza swaga swaga zake, bahati mbaya richmond ikatokea muda mfupi baadaye. Yaliyobakia ni historia.
 
Vipi kuhusu Raisi kufanya kazi ya Bunge ya kupanga matumizi ya fedha za serikali?

Usipotoshwe na Lowassa, Kazi ya kupanga matumizi ni ya serikali kazi ya Bunge ni kuidhinisha Matumizi yaliyopangwa na serikali.

Bunge linahitaji kuidhinisha matumizi mapya ikiwa yatazidi kiwango cha bajeti iliyopitishwa lakini realocation between Ministry ni kazi ya Kamishna Mkuu wa Bajeti. Mf kuhamisha fedha za kununulia Makreti ya bia ya sherehe za uhuru na kupeleka kutokomeza kipindupindu yanahitaji ruhusa ya Kamishna wa Bajeti peke yake. Lowassa anapinga kuhamisha fedha za Sherehe za Muungano kwenda kujengea barabara.
Hizi hizo siku 100 za Lowassa kutokomeza Umaskini angetumia bajeti hii hii ya Jk au angeitisha bunge kuifuta bajet hii na kuileta mpya ndan ya hizo siku 100 na kuanza ufutaji wa umaskini?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
​
Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.

Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.


Ndugu Christopher Ole Sendeka,
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

08/04/2016

Kuteuliwa kua msemaji wa chama haimanishi kupinga kila challange inayoelekezwa kwa mtu wa chama chako... Kukosolewa ni kunzuri sana. Ninaimani kua hata rais anafrahia zaid Kukosolewa ili aweze kutenda kazi zake vinzur zaidi.
 
Maendeleo gani maisha ndio yamezidi kua magumu vitu vinaongezeka bei kwa namna ya kutisha kisa magufuli na bandari yetu
 
Back
Top Bottom