Utendaji wa Rais Magufuli: Chama cha Mapinduzi chamjibu Lowassa

Utendaji wa Rais Magufuli: Chama cha Mapinduzi chamjibu Lowassa

Sendeka nae viti maalumu anana ufahali? Mshukuru mungu kuna viti maalumu
 
Juzi 7/04/2016 wanazuoni wa ndani na nje yanchi wanaofanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, utawala bora na ushindani wa kisiasa kwa kuzungumza na watu kutoka vyama mbalimbali na Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) walimtembelea nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam,

Waziri Mkuu wa zamani aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND na aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) baada ya kukatwa na CCM kutokana na taswira yake ya UADILIFU kwa Wananchi kuwa mbaya, EDWARD LOWASSA na kufanya naye mahojiano.

Katika Mahojiano hayo, LOWASSA aliyataja mambo matano yanayomfanya autilie shaka mustakabali wa Taifa chini ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Dr. John Pombe Magufuli. Ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na Rais kugawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo, watumishi kuachishwa kazi, upitishaji mizigo Bandari ya Dar es Salaam kushuka, nchi kunyimwa misaada, na ugumu wa maisha unaowakabili wanachi kwa sasa.

HAYA NI MANENO YA MFA MAJI. Mawazo kugawa pesa hayawezi kuisha kichwani mwa LOWASSA, alizoea kufanya hivyo ili kujipatia makundi ya kumuunga mkono kwenye harakati zake za klsiasa. ALIGAWA PESA sana kwenye taasisis za dini, baadhi ya watumishi wa Umma n,k. Anafikiri na Rais naye anafanya aliyoyafanya yeye.

LOWASSA atambue kuwa fedha kwa ajili ya sherehe za Bunge, Uhuru, Muungano zipo kisheria, zilipitishwa na Bunge. Rais alichokifanya ni kubadilisha matumizi ya pesa hizo kutoka matumizi yasiyo na tija kwenda kwenye matumizi yenye tija. Lowassa anataka kutuambia hizo sherere ni muhimu kuliko vitanda mahospitalini na ujenzi wa barabara?

Lowassa hakuwahi kufanya biashara yoyote zaidi ya kuwa mtumishi ndani ya CCM na Serikalini. utajiri wake alionao na anaojivunia unatokana na UFISADI wake ndani ya chama na SERIKALI(KWA MANENO MENGINE , HAKUWA MWADILIFU KATIKA UTUMISHI WAKE).

Ingeshangaza sana kuona anafurahia watumishi wazembe, Mafisadi na wala Rushwa kama alivyokuwa yeye wakiwajibishwa na Serikali yoyote ile acha hii ya JOHN POMBE MAGUFULI. Mafisadi lazima watamuunga mkono kwa kauli yake kuhusu watumishi wabadhilifu kuchukuliwa hatua lakini Watanzania tulio wengi tunamuona kama anadhihirisha kuwa HAKIKA HAKUWA MUADILIFU.

Lipi bora? Upitisahaji mizigo Bandari ya Dar es Salaam kuongezeka mara dufu lakini tukakosa kodi au ukapungua mara dufu lakini kodi itokanayo na mizigo hiyo michache ikazidi ile mizigo mingi? Huku kote ni kutapatapa tu, ni kudhihirisha kuwa NI MUUMINI WA UFISADI.

Namna ya uzuiaji wa misaada uliofanywa na Marekani umejadiliwa sana. LOWASSA anataka kutudhihirishia yale yaliyosemwa na wengi sana kuwa YEYE ni KIBARAKA katika sakata hili.

Rais Magufuli Mungu akimuweka hai ataiongoza Tanzania kwa zaidi ya siku 1825. Ndiyo kwanza ameshaongoza siku 157 tu. maisha gani magumu wanayo wananchi kwa kipindi hicho cha siku 155 ukilinganisha na siku zilizotangulia?

Hapana shaka thamani ya sarafu yetu imeimarika, kwa kipindi hicho, bei ya vyakula imeendelea kuwa pale pale na mahali pengine kushuka, Umeme na mafuta vimeshuka bei , n.k. LOWASSA anaishi wapi asiyaone haya?

KWA KASI YA MAGUFULI, MIAKA 5 NI MICHACHE SANA. LOWASSA NI LAZIMA AONGEE ANGALAU AONEKANE YUPO LA SIVYO ANAWEZA KUPOTEA GHAFLA ILA KWA KAULI ZAKE NI DHAHIRI NI MFA MAJI, ANATAPATAPA TU.
 
Mzee wa Monduli anapenda sana mashindano, anaamini kwamba yeye tu ndiye anayeweza kufanikisha mambo. Sio vibaya akatulia akaendelea kula maisha, kufurahi na wajukuu zake. Kama haikuandikwa kuwa wewe utakuja kuwa rais basi tulia ule maisha.

Kinyongo husababisha magonjwa mengi sana. Lowassa anaishi na kinyongo, na kitamtesa kweli. Akubali tu kwamba kama haipo basi haipo, atulie amwachie JPM apige kazi, apambane na majizi pamoja na majambazi yenye elimu.

Lowassa afurahie siku zake za kuishi, awe mnyenyekevu, kutafuta kupendwa na watu siku zote hakufanani na ule upendo ambao unakuja naturally.

Washauri wake waifanye kazi yao vizuri ili Mzee wa Monduli abakie kuwa mstaafu mwenye heshima yake. Kuendelea kukosoa na kukejeli kila kinachofanywa na awamu ya tano hakuwezi kumsaidia. JPM ameshika kisu, na anao uwezo wa kukitumia kadri anavyotaka mpaka 2020.
 
Akili ya form six failure
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
​
Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.

Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.

Ndugu Christopher Ole Sendeka,
MSEMAJI WA CCM ​
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016​
 
Mkuu olesendeka ukiona watu waplay na mfumo ujue huu mfumo umekufa au ni legelege sana unahitajika kufanyiwa overhaul.mfumo imara na madhubuti ni kama bahari ,hujisafisha wenyewe, mtu asiyeendana na huko mfumo no way anaweza kufiti,hata akiingia humor kwa bahati mbaya atajitoa mwenyewe. Tuache kuposha watanzania kwa ujinga wetu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.
Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.


Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016
 
Watanzania msiwe Na haraka Na magufuli mawaziri wake wana hemea juu Juu walianza Kwa mkwara mzito nchi sio mchezo Mh.magufuli kaona dar tu akienda mikoani wilayani Na vijijini atashangaa kuona watanzania wanapelekewa Hela za Tasaaf lakini wanalala Na ng'ombe , Mashule no mapagala watoto Na walimu wanajisaidia vichakani
 
Lowassa hana lolote na yeye ndiye fisadi maana alijiuzulu nyadhifa aliyokuwa nayo ya waziri mkuu kwa shinikizo toka kwa wabunge wapinzani ndani ya bunge. Kwa sasa mh. Rais Magufuli anachapa Kazi halafu anaanza mambo yasiyo na tija. Yana
 
Watanzania Buana ni shida kweli!!
Mmewekewa mpaka vifungu vya katiba vinavyoelezea ni namna gani pesa za umma zinavyotakiwa zitumike kwa kuidhinishwa na Bunge wakati wote. Ile hela sio ya Magufuli aliyoingia nayo Madarakani toka mfukoni kwake ni hela ya umma .

Wana CCM wanashangilia uvunjwaji wa katiba kana kwamba nchi sasa inaongozwa kama enzi za machiefu. Ikumbukwe kuwa hili taifa lina Makabila zaidi ya mia ishirini na kila kabila lina historia ya watawala wake kwa hiyo kuna watawala wenye uwezo 120 ndani ya taifa hili. Ndio maana tukaamua kuwa na taifa moja lililounganishwa na himaya zilizokuwa na utawala zaidi ya 120.
Tukiacha mtu mmoja akatawala kwa maoni yake tutakua tunasimika udikteta kwenye taifa hili.
Nchi hii ni lazima iongozwe na mtu mwenye kabila au dini lakini ni lazima afuate katiba hata kama kuna kasoro kwenye katiba. Katiba yetu ina mapungufu mengi lakini isivunjwe. Bunge lipewe heshma yake. Kwa sasa bunge limekuwa kama tawi la vyama vya siasa ndio maana mwenyekiti wa chama au mjumbe wa chama anapoamua huko serikalini basi bunge nalo linapitisha ili kulinda maamuzi ya kichama.

Tunataka lowasa ajibiwe kwa na msemaji wa Ikulu na sio msemaji wa chama cha mapinduzi.
Ole sendeka hakushauriana na Rais wakati anatoa maamuzi ya matumizi ya fedha za sherehe za uhuru na za Muungano.
 
Back
Top Bottom