Utendaji wa Rais Magufuli: Chama cha Mapinduzi chamjibu Lowassa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.

Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.

Ndugu Christopher Ole Sendeka,
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016
 
Lowasa amechanganyikiwa, mirija yake aloitegemea kufisidi nji hii imekatwa.

Imagine Lowassa huyu huyu leo hii anashindwa kumsaidia mkwewe unyapalani.....

Mifumo taratibu inaanza kufanya kazi, nafasi ya mtu na kujuana sasa havina nafasi.
 
Vipi kuhusu Raisi kufanya kazi ya Bunge ya kupanga matumizi ya fedha za serikali?
Umeliwa Doroooh!! kama ulikuwa na kikampuni chako kilichokuwa kinavuta hela ya ngua za halaiki na tshit kwa ajili ya matukio ya sikukuu za kitaifa utazisoma namba mwaka huu....ni bara bara na madawati.... Kwenye bunge kuna group la manyumbu wasio na mapenzi mema na nchii.... MAGUFULI na MAJALIWA wanatosha kufanya kila kitu!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.
Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016
 
Vipi kuhusu Raisi kufanya kazi ya Bunge ya kupanga matumizi ya fedha za serikali?
Bunge hili ovyo kabisa. Unapangaje fedha kwa ajili ya sherehe wakati hospitali hakuna vitanda, vifaa tiba nk. Bunge lijifunze kutoka kwa Magu matumizi mazuri ya fedha za umma. Watz tunamuunga mikono, wewe piga kelele,
 
Lowassa mbona na yeye aliwasimamisha Wakurugenzi wengi tu wa Halmashauri alipokuwa Waziri mkuu? sasa analalamika nini?

Kwa hiyo yeye LOWASA alitakaje? wasisimashwe kupisha uchunguzi au?

Mifumo inajengwa, ingekuwa ni enzi zao, Mkwe wake angepewa Dhamana na mahakama kwa ki-note, lakini hayo kwa sasa hayana nafasi, hiyo ndiyo mifumo.

Magufuli usimsikilize huyu jamaa kabisa, kama unataka kufanikiwa basi endelea na hatua unazochukua.
 
Lazima abwabwaje tu, Lowwasa alimnyima Ubunge.... Wamasai wote walikuwa nyuma ya Lwaigwanan Lowasa... Sendeka tupa kule....
 
Bunge hili ovyo kabisa. Unapangaje fedha kwa ajili ya sherehe wakati hospitali hakuna vitanda, vifaa tiba nk. Bunge lijifunze kutoka kwa Magu matumizi mazuri ya fedha za umma.
Yeye alipokuwa mbunge aliwahi kupinga bajeti hiyo?Hakuwa miongoni mwa wale wa kusema ndioooo?

Mkawadanganye wajingawajinga.
 
Ni kweli hatuna tatizo la mfumo? Naona kama ni personal attack kuliko majibu ya maoni ya anayejibiwa. Katika taarifa iliyoandikwa na gazeti sijaona uzito wa kauli za Mh Lowassa kuzungumzia wanaochishwa kazi kwa ufisadi bali hatua zinazochukuliwa kusababisha makampuni kuounguza au kufunga shughuli na kuachisha au kupunguza wafanyakazi. Pengine kauli hiyo aliitoa lakini iliyoandikwa ni tofauti na iliyojibiwa.
 
Back
Top Bottom