Utawajengea wakwe zako nyumba?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kwa wengine ni kama mwiko kuwajengea wakwe nyumba.

Lakini mimi sioni kama kuna ubaya wo wote ule kufanya hivyo, hasa kama hali ya kifedha inaruhusu. Kutaonekana na kasoro tu ikiwa utawajengea wakwe huku wazazi wako wa kukuzaa hujawatendea hilo.

Kimsingi, wakwe zako ni wazazi wako, na wa kwako ni wa mkeo vile vile!

Kama wewe na mkeo ni mwili mmoja, inamaanisha hata na wazazi wenu ni wenu sote.

Wewe una mtazamo gani? Utawajengea wakwe zako nyumba?
 
jambo lolote unalofanya kwa ajili ya mkeo halina lawama nyingi ila sio mchepuko,mchumba,demu.

kujengea wazazi wake hasa kama mfuko unaruhusu sio jambo baya.

ila iwe ni katika ziada ya kipato chako,sio mke anazingua unakwenda na kijiko kuvunja.
 
One man down.

You are not the true son of your father
Kwa wengine ni kama mwiko kuwajengea wakwe nyumba.

Lakini mimi sioni kama kuna ubaya wo wote ule kufanya hivyo, hasa kama hali ya kifedha inaruhusu. Kutaonekana na kasoro tu ikiwa utawajengea wakwe huku wazazi wako wa kukuzaa hujawatendea hilo.

Kimsingi, wakwe zako ni wazazi wako, na wa kwako ni wa mkeo vile vile!

Kama wewe na mkeo ni mwili mmoja, inamaanisha hata na wazazi wenu ni wenu sote.

Wewe una mtazamo gani? Utawajengea wakwe zako nyumba?
 
mbona poa tu, sadaka hyo chief, ila wawe na uhitaji wa nyumba, sio ujenge tu kwa sifa ili na wewe uonekane umewajengea wakwe.
 
Kwa wengine ni kama mwiko kuwajengea wakwe nyumba.

Lakini mimi sioni kama kuna ubaya wo wote ule kufanya hivyo, hasa kama hali ya kifedha inaruhusu. Kutaonekana na kasoro tu ikiwa utawajengea wakwe huku wazazi wako wa kukuzaa hujawatendea hilo.

Kimsingi, wakwe zako ni wazazi wako, na wa kwako ni wa mkeo vile vile!

Kama wewe na mkeo ni mwili mmoja, inamaanisha hata na wazazi wenu ni wenu sote.

Wewe una mtazamo gani? Utawajengea wakwe zako nyumba?
Kaka LIKUD njoo kuna mtu anataka kunitoa kwenye mstari

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mpaka nimecheka!

Mkuu, wakwe zako ni wazazi wako pia. Wajengee tu kama unao huo uwezo.

Ujue na wewe ni mkwe mtarajiwa. Golden rule inasema uwatendee wengine kile unachotaka utendewe.

Ukiwafanyia wakwe zako jambo la kuwafurahisha, na wanao watakuja kukutendea ya kukufurahisha.

Matendo ni mbegu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom