Utata waingia muda wa kutibiwa Dk Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata waingia muda wa kutibiwa Dk Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jul 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  KIZA kimetanda juu ya siku rasmi ya kurejea kwa Dk Stephen Ulimboka nchini baada ya kuelezwa kuwa licha ya hali yake ya afya kuimarika matibabu yake yanatarajia kuwa ya muda mrefu.

  Hivi karibuni ulitokea uvumi kuwa Dk Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari angerejea nchini siku yoyote ya mwezi ujao baada ya afya yake kuimarika.

  Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage aliliambia gazeti hili jana kuwa habari za kuwa Dk Ulimboka angerejea nchini hivi karibuni hazina ukweli wowote kwakuwa matatizo yake yanahitaji matibabu ya muda mrefu.

  “Dk Ulimboka anaendelea vizuri, lakini anahitaji kuendelea na matibabu zaidi nchini Afrika ya kusini, habari ya kuwa anaweza kurejea nchini kwa siku za hivi karibuni hazina ukweli wowote, kwani kwa sisi tunaoelewa taratibu za matibabu anayopatiwa hilo haliwezekani kwa sasa”, alisema Dk Chitage.

  Alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba suala la matibabu yake si la muda mfupi,” alisema.

  Dk Chitage alisisitiza kuwa DK Ulimboka ambaye alisafirishwa nje ya nchi kutokana na hali yake kubadilika ghafla baada ya figo kushindwa kufanya kazi anasitahili kuendelea na matibabu kwa muda zaidi ya hapo alipofikia.

  Kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, aliyekuwa kiongozi wa jopo la madaktari lililokuwa likimtibia Dar es Salaam, Profesa Joseph Kahamba alikaririwa na gazeti hili alisema mwenyekiti huyo alipata maumivu makali katika sehemu zote za mwili.

  Katika hatua nyingine mmoja ya vyanzo vya habari vya kuaminika vilieleza kuwa afya ya Dk Ulimboka inaimarika, lakini kwa sasa suala la kurejea nchini bado kwa kuwa anaendelea na matibabu.


  “Katika shambulio lile alipata matatizo makubwa katika sehemu za figo na macho, ingawa hali yake imezidi kuimarika bado matibabu yake hayawezi kuwa ya muda mfupi na yenye kumwezesha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa siku za hivi karibuni”kilisema chanzo hicho cha habari..

  Dk Ulimboka alisafirishwa nje ya nchi baada ya Jopo la Madaktari Bingwa lililokuwa likimtibu likiongozwa na Profesa Joseph Kahamba kutoa ripoti kuwa hali yake imebadilika ghafla na kwamba angehitaji kusafirishwa nje kutokana na baadhi ya vipimo na matibabu kutokuwapo nchini.

  Pia Profesa Kahamba aliwahi kukaririwa na gazeti hili akisema Dk Ulimboka katika shambulio lile alipata majeraha katika sehemu zote za mwili huku aking’olewa meno mawili na kucha za vidole vyake kunyofolewa.

  Madaktari kushitaki serikali (MCT)

  Wakati hali ikiwa hivyo kwa Dk Ulimboka, viongoziwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Jumuiya ya Madaktari na Madaktari waliofukuzwa kazi na wengine kusitishiwa usajili wa leseni zao za muda walikutana jijini Dar es Salaam jana na kupitisha azimio la kuishtaki Serikali na Baraza la Madaktari mahakamani.

  Umuzi huo ni matokeo ya ushauri uliotolewa na wanasheria kwa madaktari hao waliopendekeza hatua mojawapo ya kuchukua kuwa ni kulifikisha suala hilo mahakamani.
  Mwakilishi wa Madaktari hao, Dk Frank Kagoro, alilimbia gazeti hili kuwa wamefikia hatua ya kwenda mahakamani kudai haki baada ya kugundua kuwa hatua waliyochukuliwa haikuwatendea haki.

  “Tumekubaliana kutekeleza usahuri wa wanasheria wetu, tunafikiria kufungua kesi mahakamani kupinga kitendo kilichofanywa na Serikali cha kufukuza baadhi ya madaktari kutokana na mgomo na (MCT) kusitisha leseni za muda kwa baadhi yetu”, alisema Dk Kagoro.
  Utata waingia muda wa kutibiwa Dk Ulimboka
   
 2. Robati

  Robati JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  We nilikuwa nakuheshimu sana! Naona utakuwa ACP Msangi bila shaka
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Serikali ili husika asilimia 100% na kipigo kwa Dr ulimboka
   
 4. M

  Magesi JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wap RAMADHAN IGHUNDO
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kwanza ange-seek political asylum tu. anarudije mahali Kama hapa?
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Aende uhamishone then afyatue makombora akiwa huko.
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa kuna utata gani hapo kama sio kurembaremba hadithi?
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,783
  Likes Received: 36,779
  Trophy Points: 280
  Magazeti mengi ya tz yako tayari kujizalilisha ili mradi yauzike,
  Sasa hapo kuna habari gani ya msingi??

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 9. Gajungi

  Gajungi Senior Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Umenikumbusha ,kuna habari facebook,kuna mwanafaunzi senior wa MD MUHAS ameandika "TANZANIA IS NOT A SAFE PLACE TO LIVE." imagine
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  makole Dodoma,,,,,nadhan karibu na club laaziz
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kama Dalai lama wa tibeti
   
 12. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Source:Gazeti la Uhuru
   
 13. M

  Magesi JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nataka nikamuue vp anapatikana
   
 14. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  tehe tehe...
   
 15. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,068
  Likes Received: 6,528
  Trophy Points: 280
  No comment.
   
Loading...