Uchaguzi 2020 Utata wa muungano wa kisiasa (coalition) wa CHADEMA na ACT-Wazalendo katika macho ya Sheria

Ukimsikiliza mahela, ukamsikiliza mtungi, unajiuliza maswali mengi sana lakini sawali kubwa kuliko yote, NI KWA NINI AWAMU HII WENGI WA WANAOTEULIWA KWENYE NAFASI MUHIMU NI WALE WASOMI (WALIOSOMA BILA KUELIMIKA WALA KUSTAARABIKA) WAJINGA NA WANAFIKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi huwa naiona ofisi ya msajili na msajili mwenyewe kama makada wa CCM wenye akili fulani za kiuwendawazimu. Kuanzia Jaji Liundi, Tendwa mpaka huyu Mutungi. Yaani kichwani weupe mnoo.

Hili suala la Muungano au Ushirikiano baina ya vyama liko wazi mnoo katika mambo ya kisiasa. Huhitaji hata shule ya kisheria kulidadavua.

Katika mfumo wa siasa za vyama vingi suala la ushirikiano baina ya vyama vya siasa ni jambo la kawaida sana, lipo siku zote, haliwezi kuepukika na wala halihitaji sheria yoyote ile ili kulifanya liwepo au lisiwepo. Nature ya mfumo wa siasa za vyama vingi inalifanya liwepo. Kikubwa katiba inatoa uhuru kwa mtu yoyote kuchagua chama au itikadi anayoitaka, huwezi kuzuia wagombea, wanachama au vyama kushirikiana kwenye uchaguzi.

Kuhusu muungano baina ya vyama vya siasa hilo ni suala lingine tofauti kabisa. Siku zote katika nyanja zote muungano rasmi ni suala la kisheria. Hivyo tafsiri ya kisheria ndio ingehitajika.

Tukirudi kwenye suala la Chadema-ACT, sote tunajua haliwezi kuwa suala la muungano maana muda wa kisheria ulishapita na wahusika wa hivyo vyama hawakusema kama wana mpango wa kufanya muungano bali ushirikiano. Sasa sijui msajili analitoa wapi?

Yaani Lissu kasema CHADEMA inamuunga mkono Maalim Seif na Maalim Seif kasema ACT inamuunga mkono Lissu, ghafla tu msajili anaibuka na kulikemea! Huo ni wazimu wa ofisi ya msajili.
 
Ukimsikiliza mahela, ukamsikiliza mtungi, unajiuliza maswali mengi sana lakini sawali kubwa kuliko yote, NI KWA NINI AWAMU HII WENGI WA WANAOTEULIWA KWENYE NAFASI MUHIMU NI WALE WASOMI (WALIOSOMA BILA KUELIMIKA WALA KUSTAARABIKA) WAJINGA NA WANAFIKI.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wateule wanalinda ugali.
 
UTATA WA MUUNGANO WA KISIASA (COALITION) WA CHADEMA NA ACT-WAZALENDO KATIKA MACHO YA SHERIA

Mwaka 2019 bunge liliifanyia mabadiliko Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kupitia Sheria Na. 1 ya 2019 ( the Political Parties (Amendment) Act, 2019) ambapo Kifungu cha 11 A kiliongezwa kwenye sheria hii kwa madhumuni ya kutambua rasmi Muungano wa Kisiasa (Political Coalition) wa vyama vya siasa katika uchaguzi ambapo vyama hivyo vitaweza kusimamisha mgombea mmoja katika kiti cha Rais, Mbunge na Diwani na kugawana ruzuku kwa mujibu wa makubaliano yao.

Mabadiliko haya ya sheria yanatambua Muungano Rasmi wa Kisiasa (Formal Political Coalition), hata hivyo, mabadiliko haya ya sheria hayakuzuhia na wala hayakuruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (Informal Political Coalition). Hivyo basi, Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 "iko kimya" kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (informal political coalition) wa vyama vya siasa pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa (Political Co-operation).

Sheria haijazuhia na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ikiwemo uchaguzi wa Rais pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa. Hakuna popote ambapo sheria imesema kuwa kuanzisha Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi ni kosa la jinai (criminal offense) au kosa la madai (civil wrong) au kosa la kimaadili (ethical misconduct).

Katika mazingira haya, iwapo vyama vya siasa vitaunda Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi au vitaanzisha ushirikiano wa kisiasa wa aina yoyote, changamoto kubwa ya Msajili wa Vyama vya Siasa itakuwa ni kuonesha kifungu cha sheria mahususi ambacho kimevunjwa katika Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kwa sababu sheria iko kimya kuhusu swala hili.

Katika nchi za Jumuiya ya Madola ambazo zinafuata Mfumo wa Sheria za Kawaida (Common Law Legal System) ikiwemo Tanzania kuna Kunga ya Kisheria (Legal Principle) ambayo imekubalika kikamilifu (settled principle of law) kwamba "jambo lolote ambalo sheria iko kimya basi jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanyika". Kwa maneno mengine, kila mtu anaruhusiwa kufanya jambo lolote ambalo sheria iko kimya yaani iwapo sheria haijazuhia jambo fulani kufanywa na watu na wala haijaruhusu jambo hilo kufanywa na watu basi kisheria jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanywa na watu. Pamoja na kesi zingine, msimamo huu wa sheria uliwekwa na Mahakama kupitia kwa Mtukufu Jaji Laws katika kesi ya R Vs Somerset County Council, Experte Fewings [1995] 1 All ER 513 na mtukufu Jaji Robert Meggary katika kesi ya Malone Vs Commissioner for the Metropolitan Police [1979] Ch 344.

Kwa lugha ya Kiingereza, msimamo huu wa sheria ninaweza kuuleza kwa ufasaha kama ifuatavyo;

"It is impregnable legal principle of ages in all common law jurisdictions that “Everything is permitted except what is forbidden by the law”, in other words, we as citizens, we are permitted or entitled to do things not only which the law expressly or impliedly permits or entitles us to do but also citizens are permitted or entitled to do even those "things which the law is silent".

Kwa kuwa sheria iko kimya kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi na sheria haijakataza na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi katika uchaguzi basi msimamo sahihi wa sheria ni kwamba Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ni halali kisheria na umeruhusiwa kutokana na ukimya wa sheria.

Pia, ni muhimu sana kutofautisha dhana hizi mbili yaani dhana ya "Muungano wa Kisiasa" (Political Coalition) kwa upande mmoja na dhana ya "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-operation) kwa upande mwingine. Hizi ni dhana mbili tofauti kisheria na kisiasa.

Msajili wa Vyama vya Siasa ana mamlaka ya udhibiti (regulatory powers) wa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (Formal Political Coalition) na ambao Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa (Political Coalition Agreement) imesajiliwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Muungano wa Kisiasa unakuwa Muungano Rasmi wa Kisiasa iwapo Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa wa vyama vya siasa viwili au zaidi yameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa kila chama cha siasa ambacho ni mdaawa (party) katika makubaliano hayo na makubaliano hayo yamesainiwa na viongozi ambao wameruhusiwa na vyama vya siasa husika kufanya hivyo na nakala ya makubaliano hayo imesajiliwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa miezi 3 kabla ya uchaguzi au siku 14 baada ya kuingia makubaliano hayo iwapo yamefanyika baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya udhibiti wa "Muungano wa Kisiasa" ambao sio rasmi (informal coalition) na ambao Makubaliano yake hayakusajiriwa katika ofisi yake. Pia, Msajili wa Vyama vya Siasa hana kabisa mamlaka ya udhibiti wa "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-Operation) wowote isipokuwa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (official) tu ndo uko ndani ya mamlaka ya udhibiti wa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Swala la "Ushirikiano wa Kisiasa" wa vyama vya siasa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi liko nje ya mamlaka ya udhibiti ya Msajili wa Vyama vya Siasa isipokuwa ushirikiano wa kisiasa ambao huko katika umbo (form) la "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi. Ushirikiano wa Kisiasa sio lazima uwe katika Uchaguzi tu bali unaweza kuwa kwenye mambo mengine zaidi ya Uchaguzi kama vile katika eneo la kujengea uwezo viongozi (leadership capacity building), sera, misimamo ya pamoja katika maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi etc. Wakati Muungano wa Kisiasa kwa kawaida huwa na lengo kuu moja la kushirikiana katika uchaguzi kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi zote za kisiasa zinazogombewa kwenye uchaguzi au katika baadhi ya nafasi.

Kwa msingi wa uchambuzi huu mfupi wa kisheria, ninamkaribisha kila mtu afanye hitimisho lake mwenyewe, mimi sitafanya hitimisho ili kumpa huru kila msomaji kufanya hitimisho lake mwenyewe.

Makala hii imeandaliwa na Matojo M. Cosatta, (Senior JF Member).
Your talking tooooo much
 
Back
Top Bottom