Uchaguzi 2020 Utata wa muungano wa kisiasa (coalition) wa CHADEMA na ACT-Wazalendo katika macho ya Sheria

Matojo Cosatta

Senior Member
Jul 28, 2017
193
500
UTATA WA MUUNGANO WA KISIASA (COALITION) WA CHADEMA NA ACT-WAZALENDO KATIKA MACHO YA SHERIA

Mwaka 2019 bunge liliifanyia mabadiliko Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kupitia Sheria Na. 1 ya 2019 ( the Political Parties (Amendment) Act, 2019) ambapo Kifungu cha 11 A kiliongezwa kwenye sheria hii kwa madhumuni ya kutambua rasmi Muungano wa Kisiasa (Political Coalition) wa vyama vya siasa katika uchaguzi ambapo vyama hivyo vitaweza kusimamisha mgombea mmoja katika kiti cha Rais, Mbunge na Diwani na kugawana ruzuku kwa mujibu wa makubaliano yao.

Mabadiliko haya ya sheria yanatambua Muungano Rasmi wa Kisiasa (Formal Political Coalition), hata hivyo, mabadiliko haya ya sheria hayakuzuhia na wala hayakuruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (Informal Political Coalition). Hivyo basi, Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 "iko kimya" kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (informal political coalition) wa vyama vya siasa pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa (Political Co-operation).

Sheria haijazuhia na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ikiwemo uchaguzi wa Rais pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa. Hakuna popote ambapo sheria imesema kuwa kuanzisha Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi ni kosa la jinai (criminal offense) au kosa la madai (civil wrong) au kosa la kimaadili (ethical misconduct).

Katika mazingira haya, iwapo vyama vya siasa vitaunda Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi au vitaanzisha ushirikiano wa kisiasa wa aina yoyote, changamoto kubwa ya Msajili wa Vyama vya Siasa itakuwa ni kuonesha kifungu cha sheria mahususi ambacho kimevunjwa katika Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kwa sababu sheria iko kimya kuhusu swala hili.

Katika nchi za Jumuiya ya Madola ambazo zinafuata Mfumo wa Sheria za Kawaida (Common Law Legal System) ikiwemo Tanzania kuna Kunga ya Kisheria (Legal Principle) ambayo imekubalika kikamilifu (settled principle of law) kwamba "jambo lolote ambalo sheria iko kimya basi jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanyika". Kwa maneno mengine, kila mtu anaruhusiwa kufanya jambo lolote ambalo sheria iko kimya yaani iwapo sheria haijazuhia jambo fulani kufanywa na watu na wala haijaruhusu jambo hilo kufanywa na watu basi kisheria jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanywa na watu. Pamoja na kesi zingine, msimamo huu wa sheria uliwekwa na Mahakama kupitia kwa Mtukufu Jaji Laws katika kesi ya R Vs Somerset County Council, Experte Fewings [1995] 1 All ER 513 na mtukufu Jaji Robert Meggary katika kesi ya Malone Vs Commissioner for the Metropolitan Police [1979] Ch 344.

Kwa lugha ya Kiingereza, msimamo huu wa sheria ninaweza kuuleza kwa ufasaha kama ifuatavyo;

"It is impregnable legal principle of ages in all common law jurisdictions that “Everything is permitted except what is forbidden by the law”, in other words, we as citizens, we are permitted or entitled to do things not only which the law expressly or impliedly permits or entitles us to do but also citizens are permitted or entitled to do even those "things which the law is silent".

Kwa kuwa sheria iko kimya kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi na sheria haijakataza na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi katika uchaguzi basi msimamo sahihi wa sheria ni kwamba Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ni halali kisheria na umeruhusiwa kutokana na ukimya wa sheria.

Pia, ni muhimu sana kutofautisha dhana hizi mbili yaani dhana ya "Muungano wa Kisiasa" (Political Coalition) kwa upande mmoja na dhana ya "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-operation) kwa upande mwingine. Hizi ni dhana mbili tofauti kisheria na kisiasa.

Msajili wa Vyama vya Siasa ana mamlaka ya udhibiti (regulatory powers) wa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (Formal Political Coalition) na ambao Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa (Political Coalition Agreement) imesajiliwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Muungano wa Kisiasa unakuwa Muungano Rasmi wa Kisiasa iwapo Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa wa vyama vya siasa viwili au zaidi yameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa kila chama cha siasa ambacho ni mdaawa (party) katika makubaliano hayo na makubaliano hayo yamesainiwa na viongozi ambao wameruhusiwa na vyama vya siasa husika kufanya hivyo na nakala ya makubaliano hayo imesajiliwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa miezi 3 kabla ya uchaguzi au siku 14 baada ya kuingia makubaliano hayo iwapo yamefanyika baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya udhibiti wa "Muungano wa Kisiasa" ambao sio rasmi (informal coalition) na ambao Makubaliano yake hayakusajiriwa katika ofisi yake. Pia, Msajili wa Vyama vya Siasa hana kabisa mamlaka ya udhibiti wa "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-Operation) wowote isipokuwa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (official) tu ndo uko ndani ya mamlaka ya udhibiti wa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Swala la "Ushirikiano wa Kisiasa" wa vyama vya siasa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi liko nje ya mamlaka ya udhibiti ya Msajili wa Vyama vya Siasa isipokuwa ushirikiano wa kisiasa ambao huko katika umbo (form) la "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi. Ushirikiano wa Kisiasa sio lazima uwe katika Uchaguzi tu bali unaweza kuwa kwenye mambo mengine zaidi ya Uchaguzi kama vile katika eneo la kujengea uwezo viongozi (leadership capacity building), sera, misimamo ya pamoja katika maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi etc. Wakati Muungano wa Kisiasa kwa kawaida huwa na lengo kuu moja la kushirikiana katika uchaguzi kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi zote za kisiasa zinazogombewa kwenye uchaguzi au katika baadhi ya nafasi.

Kwa msingi wa uchambuzi huu mfupi wa kisheria, ninamkaribisha kila mtu afanye hitimisho lake mwenyewe, mimi sitafanya hitimisho ili kumpa huru kila msomaji kufanya hitimisho lake mwenyewe.

Makala hii imeandaliwa na Matojo M. Cosatta, (Senior JF Member).
 
Da Gladiator

JF-Expert Member
Aug 3, 2020
816
1,000
Acha kuruka ruka, hakuna chenye utata kinachohusu sheria, kinaweza kumshinda Tundu AM Lissu. Rejea kwenye kipindi cha Dk45, Lissu v Middle, ITV. aliongelea kuhusu mtego juu ya muungano, hivo mpaka kutoka hadharani ACT-Wazalendo NA CHADEMA wanajua wakifanyachO.

NiYeyE2020. 'in TID voice'
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,428
2,000
Kwahiyo Muungano wa CCM na TLP, ama Mrema kumuunga mkono Magufuli ni sahihi?

Hizi ni sheria kandamizi za awamu ya tano. Kama sheria ya Takwimu. Sheria ya habari nk.

Jiwe out.
Baada ya MaCCM kusumbuliwa na UKAWA mwaka 2015 yakaona yatunge sheria ya kuzuia vyama vya upinzani kuungana .

Yaani badala ya kutatua challenges za wananchi, yako busy kutunga sheria mbovu na kandamizi kujilinda.
 
tathmini

Senior Member
Feb 10, 2011
196
250
Kwa mtizamo wangu, ushirikiano wa kisiasa wa TLP na CCM ni sahihi kisheria, pia ushirikiano wa Chadema na ACT-Wazalendo ni sahihi kisheria.
Sisi na vyama vyote tusimfuate Msajili ambaye amepitiliza katika uoga wake wa nguvu ya CHADEMA na ACT. Jambo liko wazi. Sheria ilitungwa ili iratibu Muungano wa vyama, siyo kuzuia bali kuratibu. Muungano ni kitu kikubwa kwa sababu ama uhai wote au sehemu ya uhai wa mwanzo wa vyama vinavyoungana huondolewa, na uhai mpya hutengenezwa. Huo unahitaji kuelezewa haki na wajibu wake. Ndiyo sababu unahitaji sheria (regulation). Ushirikiano ni jambo tofauti, rahisi na la kila siku.

Halitengenezi uhai mpya au kuondoa wa zamani kwa namna yoyote. Hufanyika muda wote kwa hiari na namna mbalimbali. Hauhitaji makubaliano ya kimaandishi. Hauzuiliki wala kushitakika. Kuutungia sheria ni kichekesho. Wote tumekuwa tukijua kuwa, kwa vile vyama HAVIKUUNGANA katika muda wa kisheria, VITASHIRIKIANA tu vikipenda.

Ndivyo wanavyofanya. TLP na CCM walikuwa sahihi na Msajili alijua hivyo, ndiyo sababu alinyamaza. Ni ushabiki na uoga wake tu ndio uliomfanya kujaribu kukataza jambo hili - pale vyama asivyovitaka navyo vilipoonyesha ushirikiano. Tuendelee. Ushirikiano hoyee!
 
Matojo Cosatta

Senior Member
Jul 28, 2017
193
500
Baada ya MaCCM kusumbuliwa na UKAWA mwaka 2015 yakaona yatunge sheria ya kuzuia vyama vya upinzani kuungana .

Yaani badala ya kutatua challenges za wananchi, yako busy kutunga sheria mbovu na kandamizi kujilinda.

Pia, nchi hii ina changamoto moto ya draftmen wa sheria, wanaandika sheria bila weledi na mwishowe sheria inatengeneza matatizo mengi na mazito kuliko inayotatua.
 
Jankoliko

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
434
500
UTATA WA MUUNGANO WA KISIASA (COALITION) WA CHADEMA NA ACT-WAZALENDO KATIKA MACHO YA SHERIA

Mwaka 2019 bunge liliifanyia mabadiliko Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 2058 kupitia Sheria Na. 1 ya 2019 ( the Political Parties (Amendment) Act, 2019) ambapo Kifungu cha 11 A kiliongezwa kwenye sheria hii kwa madhumuni ya kutambua rasmi Muungano wa Kisiasa (Political Coalition) wa vyama vya siasa katika uchaguzi ambapo vyama hivyo vitaweza kusimamisha mgombea mmoja katika kiti cha Rais, Mbunge na Diwani na kugawana ruzuku kwa mujibu wa makubaliano yao.

Mabadiliko haya ya sheria yanatambua Muungano Rasmi wa Kisiasa (Formal Political Coalition), hata hivyo, mabadiliko haya ya sheria hayakuzuhi na wala hayakuruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (Informal Political Coalition). Hivyo basi, Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 "iko kimya" kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (informal political coalition) wa vyama vya siasa pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa (Political Co-operation).

Sheria haijazuhia na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ikiwemo uchaguzi wa Rais pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa. Hakuna popote ambapo sheria imesema kuwa kuanzisha Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi ni kosa la jinai (criminal offense) au kosa la madai (civil wrong) au kosa la kimaadili (ethical misconduct).

Katika mazingira haya, iwapo vyama vya siasa vitaunda Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi au vitaanzisha ushirikiano wa kisiasa wa aina yoyote, changamoto kubwa ya Msajili wa Vyama vya Siasa itakuwa ni kuonesha kifungu cha sheria mahususi ambacho kimevunjwa katika Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kwa sababu sheria iko kimya kuhusu swala hili.

Katika nchi za Jumuiya ya Madola ambazo zinafuata Mfumo wa Sheria za Kawaida (Common Law Legal System) ikiwemo Tanzania kuna Kunga ya Kisheria (Legal Principle) ambayo imekubalika kikamilifu (settled principle of law) kwamba "jambo lolote ambalo sheria iko kimya basi jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanyika". Kwa maneno mengine, kila mtu anaruhusiwa kufanya jambo lolote ambalo sheria iko kimya yaani iwapo sheria haijazuhia jambo fulani kufanywa na watu na wala haijaruhusu jambo hilo kufanywa na watu basi kisheria jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanywa na watu. Pamoja na kesi zingine, msimamo huu wa sheria uliwekwa na Mahakama kupitia kwa Mtukufu Jaji Laws katika kesi ya R Vs Somerset County Council, Experte Fewings [1995] 1 All ER 513 na mtukufu Jaji Robert Meggary katika kesi ya Malone Vs Commissioner for the Metropolitan Police [1979] Ch 344.

Kwa lugha ya Kiingereza, msimamo huu wa sheria ninaweza kuuleza kwa ufasaha kama ifuatavyo;

"It is impregnable legal principle of ages in all common law jurisdictions that “Everything is permitted except what is forbidden by the law”, in other words, we as citizens, we are permitted or entitled to do things not only which the law expressly or impliedly permits or entitles us to do but also citizens are permitted or entitled to do even those "things which the law is silent".

Kwa kuwa sheria iko kimya kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi na sheria haijakataza na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi katika uchaguzi basi msimamo sahihi wa sheria ni kwamba Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ni halali kisheria na umeruhusiwa kutokana na ukimya wa sheria.

Pia, ni muhimu sana kutofautisha dhana hizi mbili yaani dhana ya "Muungano wa Kisiasa" (Political Coalition) kwa upande mmoja na dhana ya "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-operation) kwa upande mwingine. Hizi ni dhana mbili tofauti kisheria na kisiasa.

Msajili wa Vyama vya Siasa ana mamlaka ya udhibiti (regulatory powers) wa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (Formal Political Coalition) na ambao Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa (Political Coalition Agreement) imesajiliwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Muungano wa Kisiasa unakuwa Muungano Rasmi wa Kisiasa iwapo Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa wa vyama vya siasa viwili au zaidi yameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa kila chama cha siasa ambacho ni mdaawa (party) katika makubaliano hayo na makubaliano hayo yamesainiwa na viongozi ambao wameruhusiwa na vyama vya siasa husika kufanya hivyo na nakala ya makubaliano hayo imesajiliwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa miezi 3 kabla ya uchaguzi au siku 14 baada ya kuingia makubaliano hayo iwapo yamefanyika baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya udhibiti wa "Muungano wa Kisiasa" ambao sio rasmi (informal coalition) na ambao Makubaliano yake hayakusajiriwa katika ofisi yake. Pia, Msajili wa Vyama vya Siasa hana kabisa mamlaka ya udhibiti wa "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-Operation) wowote isipokuwa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (official) tu ndo uko ndani ya mamlaka ya udhibiti wa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Swala la "Ushirikiano wa Kisiasa" wa vyama vya kisiasa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi liko nje ya mamlaka ya udhibiti ya Msajili wa Vyama vya Siasa isipokuwa ushirikiano wa kisiasa ambao huko katika umbo (form) la "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi. Ushirikiano wa Kisiasa sio lazima uwe katika Uchaguzi tu bali unaweza kuwa kwenye mambo mengine zaidi ya Uchaguzi kama vile katika eneo la kujengea uwezo viongozi (leadership capacity building), sera, misimamo ya pamoja katika maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi etc. Wakati Muungano wa Kisiasa kwa kawaida huwa na lengo kuu moja la kushirikiana katika uchaguzi kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi zote za kisiasa zinazogombewa kwenye uchaguzi au katika baadhi ya nafasi.

Kwa msingi wa uchambuzi huu mfupi wa kisheria, ninamkaribisha kila mtu afanye hitimisho lake mwenyewe, mimi sitafanya hitimisho ili kumpa huru kila msomaji kufanya hitimisho lake mwenyewe.

Makala hii imeandaliwa na Matojo M. Cosatta, (Senior JF Member).
Sina ujuzi na mambo ya sheria, hivyo nilipata tabu kidogo kumuelewa Mh Zitto wakati anahojiwa na Jenerali Ulimwengu, alijibu kwamba tupo kwenye mazunguzo na muda ukifika tutashirikiana kuweka mgombea mmoja "bila kufuata sheria, na bila kuvunja sheria". Na kwa uchambuzi huu sasa ndio namuelewa Mh Zitto alimaanisha nini.
 
Matojo Cosatta

Senior Member
Jul 28, 2017
193
500
Sina ujuzi na mambo ya sheria, hivyo nilipata tabu kidogo kumuelewa Mh Zitto wakati anahojiwa na Jenerali Ulimwengu, alijibu kwamba tupo kwenye mazunguzo na muda ukifika tutashirikiana kuweka mgombea mmoja "bila kufuata sheria, na bila kuvunja sheria". Na kwa uchambuzi huu sasa ndio namuelewa Mh Zitto alimaanisha nini.

Hiyo kauli ya Zitto ambayo iko kwenye alama za kufunga na kufungua semi ni kauli ya falsafa ya sheria (jurisprudensia).
 
Malcom XX

JF-Expert Member
Sep 12, 2020
379
1,000
Jiwe alihisi tangu 2018, akaanza kutunga sheria za kubana upinzani alichosahau ni kwamba Elimu bahari huwezi kujua yote,
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,650
2,000
Pamoja na yote hayo wananchi wanataka kufaidika na nchi yao na siyo propaganda.
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,901
2,000
UTATA WA MUUNGANO WA KISIASA (COALITION) WA CHADEMA NA ACT-WAZALENDO KATIKA MACHO YA SHERIA

Mwaka 2019 bunge liliifanyia mabadiliko Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kupitia Sheria Na. 1 ya 2019 ( the Political Parties (Amendment) Act, 2019) ambapo Kifungu cha 11 A kiliongezwa kwenye sheria hii kwa madhumuni ya kutambua rasmi Muungano wa Kisiasa (Political Coalition) wa vyama vya siasa katika uchaguzi ambapo vyama hivyo vitaweza kusimamisha mgombea mmoja katika kiti cha Rais, Mbunge na Diwani na kugawana ruzuku kwa mujibu wa makubaliano yao.

Mabadiliko haya ya sheria yanatambua Muungano Rasmi wa Kisiasa (Formal Political Coalition), hata hivyo, mabadiliko haya ya sheria hayakuzuhia na wala hayakuruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (Informal Political Coalition). Hivyo basi, Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 "iko kimya" kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi (informal political coalition) wa vyama vya siasa pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa (Political Co-operation).

Sheria haijazuhia na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ikiwemo uchaguzi wa Rais pamoja na aina nyingine za ushirikiano wa kisiasa. Hakuna popote ambapo sheria imesema kuwa kuanzisha Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi ni kosa la jinai (criminal offense) au kosa la madai (civil wrong) au kosa la kimaadili (ethical misconduct).

Katika mazingira haya, iwapo vyama vya siasa vitaunda Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi au vitaanzisha ushirikiano wa kisiasa wa aina yoyote, changamoto kubwa ya Msajili wa Vyama vya Siasa itakuwa ni kuonesha kifungu cha sheria mahususi ambacho kimevunjwa katika Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kwa sababu sheria iko kimya kuhusu swala hili.

Katika nchi za Jumuiya ya Madola ambazo zinafuata Mfumo wa Sheria za Kawaida (Common Law Legal System) ikiwemo Tanzania kuna Kunga ya Kisheria (Legal Principle) ambayo imekubalika kikamilifu (settled principle of law) kwamba "jambo lolote ambalo sheria iko kimya basi jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanyika". Kwa maneno mengine, kila mtu anaruhusiwa kufanya jambo lolote ambalo sheria iko kimya yaani iwapo sheria haijazuhia jambo fulani kufanywa na watu na wala haijaruhusu jambo hilo kufanywa na watu basi kisheria jambo hilo limeruhusiwa na sheria kufanywa na watu. Pamoja na kesi zingine, msimamo huu wa sheria uliwekwa na Mahakama kupitia kwa Mtukufu Jaji Laws katika kesi ya R Vs Somerset County Council, Experte Fewings [1995] 1 All ER 513 na mtukufu Jaji Robert Meggary katika kesi ya Malone Vs Commissioner for the Metropolitan Police [1979] Ch 344.

Kwa lugha ya Kiingereza, msimamo huu wa sheria ninaweza kuuleza kwa ufasaha kama ifuatavyo;

"It is impregnable legal principle of ages in all common law jurisdictions that “Everything is permitted except what is forbidden by the law”, in other words, we as citizens, we are permitted or entitled to do things not only which the law expressly or impliedly permits or entitles us to do but also citizens are permitted or entitled to do even those "things which the law is silent".

Kwa kuwa sheria iko kimya kuhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi na sheria haijakataza na wala haijaruhusu Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi katika uchaguzi basi msimamo sahihi wa sheria ni kwamba Muungano wa Kisiasa ambao sio rasmi wa vyama vya siasa katika Uchaguzi ni halali kisheria na umeruhusiwa kutokana na ukimya wa sheria.

Pia, ni muhimu sana kutofautisha dhana hizi mbili yaani dhana ya "Muungano wa Kisiasa" (Political Coalition) kwa upande mmoja na dhana ya "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-operation) kwa upande mwingine. Hizi ni dhana mbili tofauti kisheria na kisiasa.

Msajili wa Vyama vya Siasa ana mamlaka ya udhibiti (regulatory powers) wa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (Formal Political Coalition) na ambao Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa (Political Coalition Agreement) imesajiliwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Muungano wa Kisiasa unakuwa Muungano Rasmi wa Kisiasa iwapo Makubaliano ya Muungano wa Kisiasa wa vyama vya siasa viwili au zaidi yameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa kila chama cha siasa ambacho ni mdaawa (party) katika makubaliano hayo na makubaliano hayo yamesainiwa na viongozi ambao wameruhusiwa na vyama vya siasa husika kufanya hivyo na nakala ya makubaliano hayo imesajiliwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa miezi 3 kabla ya uchaguzi au siku 14 baada ya kuingia makubaliano hayo iwapo yamefanyika baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya udhibiti wa "Muungano wa Kisiasa" ambao sio rasmi (informal coalition) na ambao Makubaliano yake hayakusajiriwa katika ofisi yake. Pia, Msajili wa Vyama vya Siasa hana kabisa mamlaka ya udhibiti wa "Ushirikiano wa Kisiasa" (Political Co-Operation) wowote isipokuwa "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi (official) tu ndo uko ndani ya mamlaka ya udhibiti wa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Swala la "Ushirikiano wa Kisiasa" wa vyama vya siasa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi liko nje ya mamlaka ya udhibiti ya Msajili wa Vyama vya Siasa isipokuwa ushirikiano wa kisiasa ambao huko katika umbo (form) la "Muungano wa Kisiasa" ambao ni rasmi. Ushirikiano wa Kisiasa sio lazima uwe katika Uchaguzi tu bali unaweza kuwa kwenye mambo mengine zaidi ya Uchaguzi kama vile katika eneo la kujengea uwezo viongozi (leadership capacity building), sera, misimamo ya pamoja katika maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi etc. Wakati Muungano wa Kisiasa kwa kawaida huwa na lengo kuu moja la kushirikiana katika uchaguzi kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi zote za kisiasa zinazogombewa kwenye uchaguzi au katika baadhi ya nafasi.

Kwa msingi wa uchambuzi huu mfupi wa kisheria, ninamkaribisha kila mtu afanye hitimisho lake mwenyewe, mimi sitafanya hitimisho ili kumpa huru kila msomaji kufanya hitimisho lake mwenyewe.

Makala hii imeandaliwa na Matojo M. Cosatta, (Senior JF Member).
msajili asilete za kuleta hapa... wakati Magufuli anamteua Mgwira kuwa RC (cheo cha kisiasa) wa Kilimanjaro alikuwa hajui kuwa huyu mama ni mwenyekiti wa ACT?
 
jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
3,376
2,000
Haisaidii kitu Mutungi na jiwe wamepigwa chenga la tobo, vyama havijaunga bali wananchi wameungana, visiwani mgombea urais ACT bara Lisu elimu inazidi tolewa. Mwaka huu chama chakavu lzm kimfate ndugu yake KANU kaburini
 
jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
3,376
2,000
msajili asilete za kuleta hapa... wakati Magufuli anamteua Mgwira kuwa RC (cheo cha kisiasa) wa Kilimanjaro alikuwa hajui kuwa huyu mama ni mwenyekiti wa ACT?
Imekula kwao kizazi cha sasa sio kile Cha miaka ya sabini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom