mourisous
JF-Expert Member
- Jan 19, 2016
- 443
- 270
Pengine umesahau kuwa wadhifa wa RC ni mkubwa sana kuliko utangazaji au ukurugenzi wa media.Niende moja kwa moja kwenye mada,
Kuna habari chungu nzima zinazoelezea jinsi RC wa Dar es Salaam alivovamia Clouds Media lakini habari hii ina ushahidi kidogo sana, ushahidi mkubwa ni mahojiano ya Bw Ruge na waandishi wake wa habari, na clip fupi inayomuonyesha RC akiingia na kutoka ofisin kwao.
Kila mtu anayemjua Ruge anamjua ni mtu wa maslahi, ni mwepesi sana kumgeuka yoyote kunapo maslahi. Hili linaweza elezewa vzr na Mr II (Sugu) kuliko yoyote. Asingeweza kuacha maslahi makubwa aliyenayo kwa RC huyo na kugombana naye unless anamaslahi mengine makubwa zaidi, na kwa maana hiyo maneno yake siyo ya kuzingatiwa saana labda kama yana ushahidi mwingine wa ziada.
Kwa hilo, ingekuwa vyema Clouds Media wakatoa ushahidi huo wa ziada kwa kuonyesha mkanda mzima ukionyesha uvamizi ule ili ndugu RC ashtakiwe kwa hilo na kwa sababu ushahidi wa video ni mkubwa zaidi ya ushahidi mwingine wowote ndugu makonda hawezi kukwepa kamwe huko mahakan au kokote ushahidi utakapoonyeshwa.
Swali la kujiuliza why haujatolewa ushahidi woote huo either kwenye TV yao au mahakan na badala yake zimeanza kuwekwa hadithi moja baada ya nyingine (vyeti,uvamizi,utakaji....) mpaka mwishowe verse zitaisha na hakuna lililobadilika.
Naamini haki ya RC na Clouds Media ziko kwenye hiyo video. Clouds Media watuweke wazi ili tumjue mkuu wa mkoa vzr na tumhukum kwa hilo na si maneno yao.
Kwa video hiyo hatutahitaji vyeti wala tuhuma za yeye kumteka ROMA, ila bila video hiyo itakuwa ni hadithi tu kama hadithi nyingine zozote, baada ya utamu na uwongo wa hadithi kila mtu anakung'uta matako yake na kwenda kukojoa then kulala kesho tukisubiria hadithi nyingine.
katika andishi lako unadai kupata video ili ushahidi ukamilike. Je Ile clip haimuoneshi RC akiwa na askari wenye mtutu wakiingia studio za clouse? Pengine unaweza ukajitetea kuwa ni walinzi wake OK. Je RC analindwa zaidi hapa nchini kuliko mkuu wa nchi? Na wapi ulishaona mkuu WA nchi kaongozana na walinzi wenye silaha za dhahiri shahir?
Kwa majibu ya maswali ayo ni wazi utapata kujua adhma ya RC kufika Na mtutu pale haikuwa njema. Na ikiwa RC hakuhusika Na tulio zima (maybe picha za kutengeneza) mbn hakutoa kauli yeyote au kukichukulia hatua xhombo hicho kwa kumchafua yeye Na KITI chake??
Tusitetee maovu kisa kafanya mzazi wako.