Utata katika matumizi ya lugha

Umuzukuru

JF-Expert Member
May 30, 2019
609
540
Kwa fasili ya harakaharaka
Utata katika maneno au katika matumizi ya lugha ni ile hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja
Mfano:maneno kama vile
đź“ŚUa
đź“ŚMbuzi
đź“ŚChezewa

Mfano wa sentensi:
đź“ŚMwenye kazi yeyote halali

Hapa maana ya kwanza ni kuwa mtu yeyote mwenye kazi huwa halali usingizi

Maana ya pili ni mtu yeyote mwenye kazi inayotambulika kisheria na isiyokiuka kanuni na taratibu zilizowekwa na aidha serikali au jamii fulani mahsusi
⚠️Neno lenye utata ni halali

đź“ŚAmempigia mpira
đź“ŚAnalima barabara
đź“ŚWanajf ambao hawatachangia mada watapigwa ban
đź“ŚKufanya kazi hataki
đź“ŚNini analilia.....nk

Sababu za utata katika lugha:
⚠️Kutumia maneno yenye lugha ya picha
⚠️Kutumia maneno yenye mzizi -amba-
⚠️Kutumia maneno yenye maana zaidi ya moja
⚠️Kutofuata taratibu bora za uandishi kama vile kutotumia mpangilio mzuri wa meneno
⚠️Kutotumia alama za uandishi inavyotakiwa mfano alama za mkato,nukta,kiulizo,mabano,nk
⚠️Kutumia baadhi ya viambishi vya kauli ya kutendea mfano limia,chumia,pigia,chezea nk.

Hebu ongezea maneno au sentesi zenye utata hasa kama wewe ni mtumiaji wa lugha adhimu ya kiswahili
 
Back
Top Bottom