Utaratibu wa kufuatwa baada ya kulingana kwa kura za wagombea walioongoza katika Uchaguzi

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
70DEAB7D-2D84-4788-B71C-3C396BDD1E84.png


Kwa mujibu wa kifungu cha 77 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 78 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, pale ambapo kutakuwa na wagombea waliopata idadi ya kura inayolingana na ikashindikana kupata mshindi baada ya kujumlisha kura zote, Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi anatakiwa kufungua masanduku yote ya kura katika jimbo au kata na kuhesabu kura upya.

Baada ya kuhesabu kura zote upya na matokeo ya uchaguzi kulingana tena atatakiwa kuitaarifu Tume.

Tume itapanga siku nyingine ya uchaguzi ambayo haitakuwa zaidi ya siku thelathini (30) tangu Siku ya Uchaguzi wa awali.

Wakati upigaji kura utakaporudiwa, watakaopigiwa kura ni wale tu ambao katika uchaguzi wa awali walipata kura nyingi kuliko wagombea wengine na kura zao zililingana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom