Utaratibu wa kuachana katika ndoa za kikristo

Duke Tachez

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
5,441
4,093
Katika kupita mitandaoni nimeona taarifa inasema bahati bukuku ameachana na mumewe, pia juzi tu niliona video florah mbasha anasema kwamba kuna vifungu kwenye biblia vinaruhusu mwanamke kuolewa mara mbili na kwa bahati mbaya Sana hakuvitaja vifungu hivyo, akasema huyo mume wake mpya amemzidi kwa mwezi mmoja wakati amemzidi miaka mingi tu, Sasa kuna mstari kwenye biblia unasema alichokiunganisha Mungu mwana damu asikitenganishe, jamani wataalam wa maandiko binafsi nahitaji elimu hapa maana navyojua ndoa za kikristo marufuku kuachana au sijaelewa
 
Ndoa ni agano la kimwili yaan nafsi mbili zinafanya agano la kuishi pamoja.Na Mungu anaheshimu sanaaa hili agano. Na tukumbuke kwamba ndo ni lile tendo yaan unaapa kwamba sitafanya na mwingine isipo kua huyu!! So ikitokea ukaenda kufanya mapenzi na mtu mwingine automatic ndoa yenu imeshafunjika, ndio maana Bwana wetu Yesu kristo alisema, haturuhusiwi kuwaacha wake au waume zetu ISIPOKUA kwa zinaa,. Yaan ukibaini kua mkeo au mumeo anatoka na mwanamke mwingine au mkeo anatoka na mwanamume mwingine, achana nae haraka!!
 
Ukiashaachana nae unaruhusiwa kuolewa Tena Au kuoa??
 
Hauruhusiwi kuachana ukishafunga ndoa mkuu. Ni mauti tu ndio inapaswa kuwaachanisha. Na hiki ni kiapo mnachoweka bila kulazimishwa wakati wa kufunga ndoa.
 
Hahaa florah mbasha amefanya maamuzi magumu
 
Back
Top Bottom