NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Hizi ndoa za kikristo zimefikia mahala sasa tunaweza kuziita ndoa za kisheria kwasababu watu wanaona mahakamani kuna unafuu kuliko kufata sheria za ndoa za kikristo.
Usijidanganye kizazi hiki kwamba mke mwema anashushwa na Bwana, mwanamke unaweza kumchunguza mwaka mzima mkiwa kwenye uchumba na ukaona ndiyo hapa nimepata "Wife material".
Muoe sasa uone timbwili lake na makucha aliyoficha, hutakosa kuona rangi yoyote. Kiburi kitaanza kwa jeuri ya ndoa akiona kwamba wote mpo sawa, maana sheria za viongozi wa kanisa zimekubana ugandane naye mpaka kifo na huruhusiwi kuoa mke mwengine.
Maandiko yapo wazi kabisa huwezi kumuacha mpaka kifo ama afanye uashareti nje ya ndoa, lakini hakuna sehemu wamekataza kuongeza mke! Kuhusu kuoa wake wawili hapa ndipo tulipoingizwa cha kike hasa kwetu Waafrika.
Watu wanakuja na utetezi wa mistari ile ya kila mwanaume awe na "Mke wake", hivi nitoe mfano tu mtu ana wake watatu;
~ Mke wa kwanza sio "Mke wake"?
~ Mke wa pili sio "Mke wake"?
~ Mke wa tatu sio "Mke wake"?
Hata kwa mwanaume mwenye mke moja, naye huyo moja ni mke wake.
Yesu pia aliongelea tu kuhusu kutoa talaka hakuzungumzia chochote kuhusu kukataza kuongeza mke. Wakati huo aliokuwepo kulikuwa na wa Israel wengi tu wenye mke zaidi ya mmoja kama mababu zao akina Musa walioleta Amri 10 za Mungu.
Kuna hii hoja nyingine ya "Mwili moja" inatafsiriwa vibaya ili kuendana na sheria za viongozi wa makanisa wanaobana mwanaume asioe mke wa ziada.
Mwanaume ni mwili moja na kila mwanamke ataekutana nae kimwili, iwe ni kwenye ndoa yenye baraka zake Mungu ama nje ya ndoa akiwa na malaya. Kwahiyo pale mwanaume anapokuwa mwili moja na mke wake bado haiondoi kwake kuwa mwili moja na wake wengine.
Hata sisi wanadamu tupo zaidi ya bilioni lakini Mungu yupo moja ila kila anaeungana roho yake, Mungu hutengeneza roho moja. Ndivyo ilivyo hivi kwa wanawake wengi wakiolewa na mwanaume moja, kila mmoja wao huwa ni mwili mmoja na mme moja. Siongei maneno matupu bila maandiko ya biblia 1-wakorintho 6:16;
"Au hamjui ya kuwa hata yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja, Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye."
Madhara yake siku hizi wakristo wengi hawana muda na sheria za viongozi wa makanisa wanakimbilia kuyamaliza mahakamani ili kuoa mke mwengine.
kumbana mwanaume kuwa na mke moja matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona michepuko imekuwa kawaida sana siku hizi.