Utapeli uliofumbiwa macho na Serikali

Wamama sasa na hayo mafuta ya mwa mpo sijui nani,ni hatari..wako brainwashed vibaya sana.

Utapeli mtupu.
 
UTAPELI ULIOFUMBIWA MACHO NA SERIKALI.

Anaandika Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu jeusi.

Angalizo; Andiko hili laweza kuwa na Lugha Kali hasa Kwa waumini wa madhehebu ya utandawazi. Hivyo Kama ni mwepesi WA hasira, mwoga wa ukweli, na unayeongozwa na mihemko, tafadhali achia hapahapa kusoma. Kuendelea kusoma huku ukijua huwezi himili lugha Kali itahesabika Kama ukaidi na madhara ya kujitakia, nami sitahusika.

Utapeli ni kitendo cha kumlaghai mtu Kwa kumuibia Mali au haki zake Kwa kutumia maneno au ujanja usiohusisha Nguvu.
Utapeli ni Aina ya wizi usiohusisha nguvu ya Mwili. Utapeli ni kwenda kinyume na makubaliano.

Ikiwa makubaliano yatatimizwa basi hakutakuwa na utapeli, na Kama katika makubaliano kuna mmoja ameonewa Kwa ujinga au shida zake haitahesabika Kama utapeli. Mfano, mekubaliana na Mtu katika biashara ya mazao. Akakuambia Niuzie hayo mahindi Gunia moja Kwa Tsh 100,000/= mkauziana kisha yeye akaenda kuyauza hayo mahindi Gunia moja Tsh 200,000/= huo sio utapeli.

Mfano wa #2
Mmekubaliana Utalipwa laki tatu, nawe Kwa hiyari yako ukakubali licha ya Mshahara kuona haukutoshi. Huo sio utapeli. Labda akikupa chini ya hapo au asikupe kabisa, huo huitwa utapeli.
Utapeli ni Aina Fulani ya dhulma ya akili au ujanja ujanja. Wizi wa kuaminika.

Utapeli upo wa Aina nyingi lakini msingi Mkuu wa utapeli ni kuiba uaminifu wa mtu.

Aina za UTAPELI
1. Utapeli wa Mali
2. Utapeli wa fikra au wazo
3. Utapeli wa Muda.

Utapeli wa Muda unaingia sehemu karibu zote.
Mfano: Umemuachia mtu kazi Kwa kumpa Oda Fulani, akufanyie au akuandalie Jambo Fulani. Mkakubaliana siku kumi zijazo utakuja kuchukua. Inafika siku ya 9 unapiga simu kuwa umeghairi na unamuambia huwezi kulipia Kwa sababu hujachukua. Hujali mwenzako amehangaika kushughulikia Oda yako. Hapo umemtapeli mwenzako Muda wake na pia baadhi ya gharama alizotumia.

Utapeli katika masuala ya Uchumba, upo Kwenye mahusiano na binti au kijana wa watu, kumbe hauna Future naye, huo ni utapeli wa Muda.

Serikali inaweza kushughulikia utapeli karibia wote lakini utapeli wa kwenye makanisa ya siku hizi umeufumbia macho.

Sijajua Kwa nini serikali imefumbia macho utapeli unaoendelea kwenye makanisa haya ya siku hizi.

Matapeli wamejiimarisha mpaka imefikia hatua wanalipia vipindi Redioni na kwenye Luninga ili kutapeli watu. Wapo ambao wamebarikiwa mpaka kufungua Media ili wazidi kutapeli watu.

Baadhi ya matapeli ni rafiki zangu Wakubwa, wanawaita Manabii na mitume, huwaga nikiongea nao wanabakia kuniambia niokoke huku wakitabasamu.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anatibu UKIMWI Kwa maombi wakati ni uongo wa wazi Kabisa, inafumbia macho wakati msemaji Hana hata cheti cha Udaktari, Hana Uelewa wa kina wa ugonjwa huo.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anafufua wafu inakaa kimya badala ya kumpa mtu huyo karipio la kuacha kuirubuni jamii.

SERIKALI inasikia kabisa mtu akiwadanganya watu kuwa anatoa Utajiri na inajua ni uongo kabisa lakini inafumbia macho. Kama hawa manabii wangekuwa wanatoa Utajiri Kwa nini wasiisaidie Nchi kuwa Tajiri mpaka tunakopa mikopo nchi za zingine.

Hao manabii hivi wanajua nchi yetu inakopa? Hao manabii hivi wanajua kuwa nchi hii kila siku watu wanakufa? Kama sio utapeli Kwa nini washindwe kutoa Suluhu la matatizo ya nchi yetu. Hawa manabii wanajua nchi yetu kuna watu ni Watumwa wanalipwa mishahara ya laki na ishirini Kwa mwezi na wanafamilia?

Yupo mtume mmoja alinipigia siku mwaka Juzi kunitishia, nikamwambia asifikiri kila mtu ni Mpumbavu.

Pendekezo;

1. Serikali iunde sheria zinazozibana taasisi za Kidini kuhusu kutapeli wananchi hasa katika kutoa mafundisho ya uongo yanayoingilia fani na taaluma za watu wengine Kama Madaktari, waalimu n.k.
Unakuta mchungaji anaongea uongo kabisa alafu anapigiwa Makofi ukimuuliza atakuambia ni mambo ya kiroho. Hakuna mambo ya hivyo.

2. Kwa vile dini ni biashara, serikali itoze Kodi kutoka Kwa taasisi za Kidini.
Wafanyakazi wa dini husika wasajiliwe kuanzia Wachungaji, wapiga kinanda na waimba kwaya. Nilishawahi kusema, wapo watu wanatumika bure Kanisani pasipo kulipwa, kuanzia Wana kwaya mpaka mashemasi walipwe mishahara sio wadanganywe wanamtumikia Mungu Bure. Hakuna Mungu WA bure.

3. Iundwe sheria kuwa wachungaji sharti wawe wamesomea uchungaji na wanacheti. Na wahubiri kulingana na vyeti vyao. Sio mtu Hana Uelewa wowote wa Dunia na mambo ya Zama hizi anapewa kipaza sauti anahutubia taifa zima mambo ya kizamani ambayo baadhi ni irrelevant Kwa Zama hizi.

Mtu WA Darasa la Saba au Kidato cha nne azungumzie mambo ya kawaida Kwa kiwango cha elimu yake, sio aongee mambo yaliyomzidi uwezo, mambo complicated mwishowe apotoshe jamii.

4. Sheria za Miradi ya Kanisa iundwe kuwa waumini wa Kanisa husika watalipiwa Nusu ya Ada na Kanisa alafu nusu nyingine watatoa wenyewe. Sio waumini wajenge mashule na Hospitali ya Kanisa alafu bado muwaumize kwenye Ada kubwa Kwa watoto wao wajapo kusoma. Huo ni uhuni na utapeli. Kama shule au Hospital niya Kanisa Acha watoto wa waumini wafaidi Miradi Yao. Ninaongea Kwa uzoefu.

5. Mafundisho yajikite zaidi kutatua matatizo ya Zama hizi za wanajamii na sio kujikita katika ulimwengu ujao ambao hakuna mwenye ushahidi nao. Mafundisho ya ulimwengu ujao yanatengeneza kizazi cha uvivu wa fikra na kuona hapa Duniani tunapita. Hivyo kukifanya kukosa Ari ya kufanya maendeleo.

6. Mapato ya wachungaji yaendane na Hali halisi ya waumini.

7. Serikali ijihusishe na dini Kama haijihusishi ni Bora izifute zote, tuongozwe na utanzania na sheria za nchi.
Dini na madhehebu ya Dini ni Kama Club za Simba na yanga tuu, ni Kama taasisi zingine lazima ziingiliwe na kuwekewa sheria Kali.

8. Iundwe sheria ambazo zitasimamiwa na Baraza la dini litakaloundwa kuhusu vyeo vya majina ya viongozi WA dini. Rank ya juu Kama itakuwa ni Kuitwa Nabii. Ambaye atathibitishwa Kwa maajabu ayafanyayo mubashara, kutabiri na ikatokea, na kufanya mambo makubwa Kama kufufua.

Nabii atajaribiwa unabii wake mbele ya halaiki Kwa kupewa atoe miujiza kadhaa ya kumthibitisha, na sio mdomo wake umthibitishe.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM
Ndugu hongera Sana kwa kuusema ukweli ambao viongozi karibu wote wa serikali na viongozi wengi wa kisiasa hawapendi kuusema kwa kuwa;

1. Serikali yenyewe kwa muda mrefu imekuwa ikiwatumia wakuu wa dini na madhehebu kuwa uwanja mkubwa wa kuwaingiza madarakani kwa utapeli.

Kwa lugha rahisi mwasisi wa utapeli huu pia aweza kuwa ni serikali yenyewe maana hawataweza kuwanyooshea kidole kwa kuwa wanajua kuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi hata viongozi hao watakuwa sehemu ya utapeli kwa kutumia majukwaa ya matapeli hao.

2. Matapeli hao wa kidini wamekuwa wakifanikiwa Sana kutokana na elimu duni isiyeweza kumsaidia mwananchi pamoja na wingi wa matatizo ya kimaisha yanayotokana na kuendelea kukua kwa umasikini miongoni mwa Wananchi walio wengi jambo ambalo ni zao la sera dhaifu za serikali.

3. Kwa kuwa humu jf wapo wawakilishi wa serikali, na kama kweli Wanataka tupige hatua hawana budi kuchukua maoni yako haya mazuri vinginevyo madhara ya kupuuza yataligharimu taifa letu hasa katika POINT ya 5.

Na maoni yasichukiliwe kuwa ni kwenda kinyume na uhuru wa kuabudu bali iwe kama zilivyo kanuni nyingine za uratibu na udhibiti wa haki nyinginezo.

Ubarikiwe Sana mtoa madai.
 
Umeandika ukweli ulio mchungu,maana kuna mchungaji mmoja ni mkubwa tu hapa mjini dsm,anahubiri sana ila ajabu na kweli ni mlevi wa K vant balaa,alafu mkewe ni afande
 
UTAPELI ULIOFUMBIWA MACHO NA SERIKALI.

Anaandika Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu jeusi.

Angalizo; Andiko hili laweza kuwa na Lugha Kali hasa Kwa waumini wa madhehebu ya utandawazi. Hivyo Kama ni mwepesi WA hasira, mwoga wa ukweli, na unayeongozwa na mihemko, tafadhali achia hapahapa kusoma. Kuendelea kusoma huku ukijua huwezi himili lugha Kali itahesabika Kama ukaidi na madhara ya kujitakia, nami sitahusika.

Utapeli ni kitendo cha kumlaghai mtu Kwa kumuibia Mali au haki zake Kwa kutumia maneno au ujanja usiohusisha Nguvu.
Utapeli ni Aina ya wizi usiohusisha nguvu ya Mwili. Utapeli ni kwenda kinyume na makubaliano.

Ikiwa makubaliano yatatimizwa basi hakutakuwa na utapeli, na Kama katika makubaliano kuna mmoja ameonewa Kwa ujinga au shida zake haitahesabika Kama utapeli. Mfano, mekubaliana na Mtu katika biashara ya mazao. Akakuambia Niuzie hayo mahindi Gunia moja Kwa Tsh 100,000/= mkauziana kisha yeye akaenda kuyauza hayo mahindi Gunia moja Tsh 200,000/= huo sio utapeli.

Mfano wa #2
Mmekubaliana Utalipwa laki tatu, nawe Kwa hiyari yako ukakubali licha ya Mshahara kuona haukutoshi. Huo sio utapeli. Labda akikupa chini ya hapo au asikupe kabisa, huo huitwa utapeli.
Utapeli ni Aina Fulani ya dhulma ya akili au ujanja ujanja. Wizi wa kuaminika.

Utapeli upo wa Aina nyingi lakini msingi Mkuu wa utapeli ni kuiba uaminifu wa mtu.

Aina za UTAPELI
1. Utapeli wa Mali
2. Utapeli wa fikra au wazo
3. Utapeli wa Muda.

Utapeli wa Muda unaingia sehemu karibu zote.
Mfano: Umemuachia mtu kazi Kwa kumpa Oda Fulani, akufanyie au akuandalie Jambo Fulani. Mkakubaliana siku kumi zijazo utakuja kuchukua. Inafika siku ya 9 unapiga simu kuwa umeghairi na unamuambia huwezi kulipia Kwa sababu hujachukua. Hujali mwenzako amehangaika kushughulikia Oda yako. Hapo umemtapeli mwenzako Muda wake na pia baadhi ya gharama alizotumia.

Utapeli katika masuala ya Uchumba, upo Kwenye mahusiano na binti au kijana wa watu, kumbe hauna Future naye, huo ni utapeli wa Muda.

Serikali inaweza kushughulikia utapeli karibia wote lakini utapeli wa kwenye makanisa ya siku hizi umeufumbia macho.

Sijajua Kwa nini serikali imefumbia macho utapeli unaoendelea kwenye makanisa haya ya siku hizi.

Matapeli wamejiimarisha mpaka imefikia hatua wanalipia vipindi Redioni na kwenye Luninga ili kutapeli watu. Wapo ambao wamebarikiwa mpaka kufungua Media ili wazidi kutapeli watu.

Baadhi ya matapeli ni rafiki zangu Wakubwa, wanawaita Manabii na mitume, huwaga nikiongea nao wanabakia kuniambia niokoke huku wakitabasamu.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anatibu UKIMWI Kwa maombi wakati ni uongo wa wazi Kabisa, inafumbia macho wakati msemaji Hana hata cheti cha Udaktari, Hana Uelewa wa kina wa ugonjwa huo.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anafufua wafu inakaa kimya badala ya kumpa mtu huyo karipio la kuacha kuirubuni jamii.

SERIKALI inasikia kabisa mtu akiwadanganya watu kuwa anatoa Utajiri na inajua ni uongo kabisa lakini inafumbia macho. Kama hawa manabii wangekuwa wanatoa Utajiri Kwa nini wasiisaidie Nchi kuwa Tajiri mpaka tunakopa mikopo nchi za zingine.

Hao manabii hivi wanajua nchi yetu inakopa? Hao manabii hivi wanajua kuwa nchi hii kila siku watu wanakufa? Kama sio utapeli Kwa nini washindwe kutoa Suluhu la matatizo ya nchi yetu. Hawa manabii wanajua nchi yetu kuna watu ni Watumwa wanalipwa mishahara ya laki na ishirini Kwa mwezi na wanafamilia?

Yupo mtume mmoja alinipigia siku mwaka Juzi kunitishia, nikamwambia asifikiri kila mtu ni Mpumbavu.

Pendekezo;

1. Serikali iunde sheria zinazozibana taasisi za Kidini kuhusu kutapeli wananchi hasa katika kutoa mafundisho ya uongo yanayoingilia fani na taaluma za watu wengine Kama Madaktari, waalimu n.k.
Unakuta mchungaji anaongea uongo kabisa alafu anapigiwa Makofi ukimuuliza atakuambia ni mambo ya kiroho. Hakuna mambo ya hivyo.

2. Kwa vile dini ni biashara, serikali itoze Kodi kutoka Kwa taasisi za Kidini.
Wafanyakazi wa dini husika wasajiliwe kuanzia Wachungaji, wapiga kinanda na waimba kwaya. Nilishawahi kusema, wapo watu wanatumika bure Kanisani pasipo kulipwa, kuanzia Wana kwaya mpaka mashemasi walipwe mishahara sio wadanganywe wanamtumikia Mungu Bure. Hakuna Mungu WA bure.

3. Iundwe sheria kuwa wachungaji sharti wawe wamesomea uchungaji na wanacheti. Na wahubiri kulingana na vyeti vyao. Sio mtu Hana Uelewa wowote wa Dunia na mambo ya Zama hizi anapewa kipaza sauti anahutubia taifa zima mambo ya kizamani ambayo baadhi ni irrelevant Kwa Zama hizi.

Mtu WA Darasa la Saba au Kidato cha nne azungumzie mambo ya kawaida Kwa kiwango cha elimu yake, sio aongee mambo yaliyomzidi uwezo, mambo complicated mwishowe apotoshe jamii.

4. Sheria za Miradi ya Kanisa iundwe kuwa waumini wa Kanisa husika watalipiwa Nusu ya Ada na Kanisa alafu nusu nyingine watatoa wenyewe. Sio waumini wajenge mashule na Hospitali ya Kanisa alafu bado muwaumize kwenye Ada kubwa Kwa watoto wao wajapo kusoma. Huo ni uhuni na utapeli. Kama shule au Hospital niya Kanisa Acha watoto wa waumini wafaidi Miradi Yao. Ninaongea Kwa uzoefu.

5. Mafundisho yajikite zaidi kutatua matatizo ya Zama hizi za wanajamii na sio kujikita katika ulimwengu ujao ambao hakuna mwenye ushahidi nao. Mafundisho ya ulimwengu ujao yanatengeneza kizazi cha uvivu wa fikra na kuona hapa Duniani tunapita. Hivyo kukifanya kukosa Ari ya kufanya maendeleo.

6. Mapato ya wachungaji yaendane na Hali halisi ya waumini.

7. Serikali ijihusishe na dini Kama haijihusishi ni Bora izifute zote, tuongozwe na utanzania na sheria za nchi.
Dini na madhehebu ya Dini ni Kama Club za Simba na yanga tuu, ni Kama taasisi zingine lazima ziingiliwe na kuwekewa sheria Kali.

8. Iundwe sheria ambazo zitasimamiwa na Baraza la dini litakaloundwa kuhusu vyeo vya majina ya viongozi WA dini. Rank ya juu Kama itakuwa ni Kuitwa Nabii. Ambaye atathibitishwa Kwa maajabu ayafanyayo mubashara, kutabiri na ikatokea, na kufanya mambo makubwa Kama kufufua.

Nabii atajaribiwa unabii wake mbele ya halaiki Kwa kupewa atoe miujiza kadhaa ya kumthibitisha, na sio mdomo wake umthibitishe.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM
Umeandika gazeti halafu pumba tupu
 
Back
Top Bottom