Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Namba nimeiweka kwenye post hapo. Hatukuikuta message ya muamala baada ya kushtuka tumeibiwa tukacheck Taarifa ya miamala tukaona namba
Pelekeni polisi hiyo namba
 
System sio rahisi Kama unavodhani.apo Kuna uzembe ulifanyika kwa maza
Nlikuwa nae mkuu alitoa simu kwenye pochi akampa, Alivyomaliza kutumia akamrudishia akairudisha kwenye pochi. Ndo Maana nashidwa kuelewa Nini kilitokea sababu hakuna maongezi ama chochote kilichofanyika Kati yao
 
Hapana nliishia Ubungo. Tulipiga customer care watuambia muda ambao pesa ilitumwa ndio muda ambao Tulikuwa ndani ya bus
Mama ana umri gani?hajasave namba ya siri kwenye simu yake?Na je message iliporudi haikuonyesha pesa zimetolewa akashtuka mapema hadi ulipompigia wew?
 
Huenda kuna wakati mama alinunua mda wa maongezi, alipoweka no ya siri akapiga chabo na kuiweka kichwani.
 
Mama ana umri gani?hajasave namba ya siri kwenye simu yake?Na je message iliporudi haikuonyesha pesa zimetolewa akashtuka mapema hadi ulipompigia wew?
Yuko 50 namba ya Siri hajasave. Sio mzee na Mambo ya simu sio mshamba Sana. Message tapeli aliifuta alipotuma hela
 
Huenda kuna wakati mama alinunua mda wa maongezi, alipoweka no ya siri akapiga chabo na kuiweka kichwani.
Hapana. Muda wa maongezi alinunua tukiwa bado nyumbani. Kwenye Gari hakutoa simu Hadi alipoombwa na huyo mwizi apige
 
Mbona ni rahisi sana kujua namba ya Siri, ila siwez kuweka waz hapa nisije kushiriki dhambi ya wizi
....Hueleweki. Ukiweka wazi hapa ili kuwasaidia watu kujua namna ya kujilinda na hili, unakuwa umeshiriki dhambi ya Wizi???
 
Yuko 50 namba ya Siri hajasave. Sio mzee na Mambo ya simu sio mshamba Sana. Message tapeli aliifuta alipotuma hela
Amenizidi kiduchu tu saaana kumbe wewe ni mtoto,haya niamkie tafadhali mwanangu.Pole kwa kutapeliwa mkuu na asante kutujuza.Lengo halikuwa kukupinga ila kujaribu kuangalia any possible angle ya mwanya wa utapeli huo.
 
Hahaha. Shikamoo mkuu
 
Au wewe ndo ulitoa hiyo hela halafu ukasahau
Mkuu are you serious. Kwani nimepata ugonjwa wa kusahau kiasi gani Yani nishindwe kukumbuka kabisa. Nimeiweka namba ya simu hapo pesa ilipotumwa
 
Ndio nauliza amejuaje namba ya Siri? Wakati hatufahamiani nae tulimkuta tu kwenye bus, na hii inakaa ndio Kazi yake. Kujifanya abiria akitarget kuomba simu then atume miamala. Ni mzoefu wa hii Kazi anajua anachofanya

Itakuwa password ya mama yako ilikuwa mwaka wa kuzaliwa so either aliotea au katika maongezi mama yako alimtajia mwaka aliozaliwa
 
....Hueleweki. Ukiweka wazi hapa ili kuwasaidia watu kujua namna ya kujilinda na hili, unakuwa umeshiriki dhambi ya Wizi???
Njia ya kujilinda usimpe mtu simu yako usie mjua siyo pesa tu atakayo kuibia ila anaweza kuitumia kuwasiliana kwaajili ya uhalifu mkubwa zaidi ya huo , akupe hasara au akuingize kwenye matatzo
 
Kuna namba zasiri ambazo ni common mfano umri wa kuzaliwa mtu akichukeki tuuu akabuni mfano 1987 au anageuza 8719...kuna 1000,,, 2000,,,2580,,,,1234.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hapa kuna kaukweli kidogo umegusia... Mi binafsi kuna jamaa aliokota smartphone sasa kwa bahati nikawaambia wamtafute mwenyewe wampe wakagoma si unajua walevi wa bangi? Sasa mimi nikaangalia picha kwenye screen nikalinganisha umri wake nikapiga mahesabu ya kuweka neno la siri kupitia muonekano ngoma ikakubali. Wakanipa elfu yangu tano ndo nikaifomat.
 
Itakuwa password ya mama yako ilikuwa mwaka wa kuzaliwa so either aliotea au katika maongezi mama yako alimtajia mwaka aliozaliwa
Password yake sio mwaka wa kuzaliwa na hakuwa na maongezi yoyote marefu Hadi kutajiana mwaka wa kuzaliwa. Ilikuwa salamu tu sababu alidhani Ni abiria mwenzake
 
Back
Top Bottom