Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Hakuna namna mtu anaweza kuiba salio bila kujua password
Ndio nauliza amejuaje namba ya Siri? Wakati hatufahamiani nae tulimkuta tu kwenye bus, na hii inakaa ndio Kazi yake. Kujifanya abiria akitarget kuomba simu then atume miamala. Ni mzoefu wa hii Kazi anajua anachofanya
 
Haiingii akilini mtu tu kushika simu aweze kuwa na uwezo wa kuhamisha salio, bila kupata taarifa zingine kutoka kwa mwenye simu.
Hilo ndio swali langu pia. Amejuaje namba ya Siri? Na inaonekana si Mara ya Kwanza hiyo ndio kazi yake, kujifanya abiria, kuomba apige simu na kuiba miamala.
 
Hapo Mama atakuwa anajua zaidi yako kuhusu hili tukio.

Kumfuatilia ni rahisi kama mkitaka
 
Ndio nauliza amejuaje namba ya Siri? Wakati hatufahamiani nae tulimkuta tu kwenye bus, na hii inakaa ndio Kazi yake. Kujifanya abiria akitarget kuomba simu then atume miamala. Ni mzoefu wa hii Kazi anajua anachofanya
Yawezekana kuna kitu mama anaficha
 
Mbona ni rahisi sana kujua namba ya Siri, ila siwez kuweka waz hapa nisije kushiriki dhambi ya wizi
 
Hapo Mama atakuwa anajua zaidi yako kuhusu hili tukio.

Kumfuatilia ni rahisi kama mkitaka
Mkuu nlikuwepo wakati wote wa tukio, Hawakuongea Cha zaidi. Alitoa simu kwenye pochi akampa then akamrudishia akisema anayempigia hapatikani.

Muongozo tafadhali jinsi ya kumfatilia
 
Habari zenu wakuu.

Jana mama yangu katapeliwa hela kutoka TigoPesa. Nilimsindikiza Ubungo mida ya mchana tukapanda basi kwenye ile seat aliyokaa tukamkuta mkaka amekaa dirishani kwasababu mama siti yake ni dirishani na tulikuwa tumewahi sana, akatupisha akasema nawaacha mkae pamoja kidogo mpige story siti yangu ni ya pembeni akaenda siti ya nyuma.

Baadae kidogo akarudi ikabidi niinuke nimpishe akae siti yake. Akamuuliza mama unasalio naomba nipige mama akijua ni msafiri mwenzake akampa simu, akajifanya nampigia hapokei akarudisha Simu, Mara hiyo hiyo akashuka akasema Naenda kununua vocha.

Jioni mama amefika nampigia ananambia yule mkaka hakurudi kwenye bus. Ile siti haikuwa yake alikuja kukaa mtu mwingine, nawaambia siti Ina mtu Hadi konda akaja akasema hii siti sijaikatia ticket.

Nikas-ense something is wrong nikamwambia mama ameshika simu yako na hakurudi kwenye bus kuna kitu kafanya angalia salio lako la TigoPesa. Kweli kuangalia salio limekombwa loooteeee. Kweli imetuumiza sana

Usalama wa pesa zetu kwenye mitandao ya simu upoje? Hawa wezi wanajuaje namba zetu za siri?

Mimi nimeogopa kwenye simu saivi siachi zaidi ya elfu 5 na kujifanya mwema kumpa Sim mtu nisiyemjua never.
Luck to ndio ilimwezesha jambazi huyo. LAZMA MAMA ALIFANYA MUAMALA JAMAA AKAONA PASSWORD.. Inawezekana aliwafuatilia tokea muda na akaona hio Pin number. Au wako zaidi ya mmoja. Au watu wa basi nao WALIHUSIKA. Huwezi toa hela bila password. Aliipata hio password.
Watu tunajisahau sana na kufanya miamala sehemu za wazi. TUACHE
 
Luck to ndio ilimwezesha jambazi huyo. LAZMA MAMA ALIFANYA MUAMALA JAMAA AKAONA PASSWORD.
Hakufanya muamala wowote. Simu ilikuwa kwenye pochi muda wote, aliitoa alipooombwa apige simu.
 
Mkuu toa elimu inavyokuwa, watu wanalizwa Sana.
Njia ya kujua password ipo ila kutokana na maelezo yako chunguza ni sangap huo muamala ulifanyika labda Kuna mtu alimuibia mama yako kabla hata ya kukutana na jamaa, huwenda Jamaa hajashiriki uwizi huo
 
Mkuu nlikuwepo wakati wote wa tukio, Hawakuongea Cha zaidi. Alitoa simu kwenye pochi akampa then akamrudishia akisema anayempigia hapatikani.

Muongozo tafadhali jinsi ya kumfatilia

Kama ni pesa nyingi, nenda polisi, huyo mwizi hachukui siku mbili atakuwa mikononi mwako, utapiga pesa yako na polisi itapata pesa yake ikiwezekana na serikali
 
Kama ni pesa nyingi, nenda polisi, huyo mwizi hachukui siku mbili atakuwa mikononi mwako, utapiga pesa yako na polisi itapata pesa yake ikiwezekana na serikali
Asante kwa muongozo mkuu
 
Back
Top Bottom