Habari zenu wakuu.
Jana mama yangu katapeliwa hela kutoka TigoPesa. Nilimsindikiza Ubungo mida ya mchana tukapanda basi kwenye ile seat aliyokaa tukamkuta mkaka amekaa dirishani kwasababu mama siti yake ni dirishani na tulikuwa tumewahi sana, akatupisha akasema nawaacha mkae pamoja kidogo mpige story siti yangu ni ya pembeni akaenda siti ya nyuma.
Baadae kidogo akarudi ikabidi niinuke nimpishe akae siti yake. Akamuuliza mama unasalio naomba nipige mama akijua ni msafiri mwenzake akampa simu, akajifanya nampigia hapokei akarudisha Simu, Mara hiyo hiyo akashuka akasema Naenda kununua vocha.
Jioni mama amefika nampigia ananambia yule mkaka hakurudi kwenye bus. Ile siti haikuwa yake alikuja kukaa mtu mwingine, nawaambia siti Ina mtu Hadi konda akaja akasema hii siti sijaikatia ticket.
Nikas-ense something is wrong nikamwambia mama ameshika simu yako na hakurudi kwenye bus kuna kitu kafanya angalia salio lako la TigoPesa. Kweli kuangalia salio limekombwa loooteeee.
Tuliangalia Taarifa ya miamala pesa imetumwa namba 0719169535 na muda uliyotumwa Ni muda ambao Tulikuwa ndani ya bus. Kweli imetuumiza sana
Usalama wa pesa zetu kwenye mitandao ya simu upoje? Hawa wezi wanajuaje namba zetu za siri?
Mimi nimeogopa kwenye simu saivi siachi zaidi ya elfu 5 na kujifanya mwema kumpa Sim mtu nisiyemjua never.
Update: Wakuu kunamdau comment 109 kaeleza vizuri kilichotokea. Ni maengineer wa mitandao wasiowaaminifu wanashirikiana na wezi Kuwapa USSD jinsi ya kutoa fedha. Ukiweka USSD option ya kuweka namba ya Siri inarukwa unatuma tu hela.
Tuweni makini kuwapa watu tusiowajua simu zetu, kujifanya msamaria mwema sometimes unaishia kulizwa.