Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Hapana namba yake ya Siri sio 0000
Ni wizi mraisi sana.Kinachofanyika ni hiki:Anatokea ndugu wa karibu na Mama ambae anajua password ya Mama kisha anamtafuta mtu wa mbali anampa mchongo kuwa Mama siku fulani atasafiri kwa hiyo pande nae kwenye bus moja na kisha omba simu yake then toa hela kwa password hii!Kikulacho ki nguoni mwako.

Ova!
 
Siamini Sana Hilo. Hatukumwambia mtu yoyote Basi tunalopanda, Siti tulikatia palepale Ubungo Tena tulipewa ya Kwanza tukaikataa tukabadilishiwa ya pili ndo tukampata huyo tapeli amekaa hapo.

Naamini huu mchezo Matapeli wanajifanya wasafiri wanaomba simu wapige then wanaiba. Kuna jinsi wanacheza na system kujua password
 
Unataka nikwambie ili na ww ukaibie watu au ? Siwez kukueleza kwa shinikizo la mihemko yako we endelea kutokuamini
Hauna jipya ww. Watu tuko hapa kuelimishana. Kama ungekuwa unajua kitu ungesema ili watu wote wajue hio njia ili waji-protect. Mjinga sana halafu unataka kiki kwa kujifanya unajua kitu.
 
Ulisafiri na mama safari yote?Njiani hakupigiwa simu na castomer care fake?
Hapana nliishia Ubungo. Tulipiga customer care watuambia muda ambao pesa ilitumwa ndio muda ambao Tulikuwa ndani ya bus
 
Mkuu walimlia njaro vipi. Hatumjui tulikata siti hapohapo Ubungo akapewa siti namba. Kwenye hiyo siti ndo tukamkuta huyo Kaka amekaa.
Muamala wa mwisho aliufanya asubuhi kabla tutoke alinunua salio kupitia tigopesa
Angalia statement ili mjue Ni muda gani exactly muamala ulifanyika. Isiwe ikawa kuna njia siju hizi mtu akiwa na simu yako akapata password kwa kutumia gadget fulani labda anaichomeka tu kwa mini usb/ charging port .

Kama muamala ulifanyika mida hio mkiwa kwa basi, itakuwa alitumia simu ya mama kutoa $$$. Kama ulifanyika baadaye itakuwa alikuwa na kitu cha kuibia password nk. Halafu unatoajae bila SIM card? Hata app, lazima isajiliwe na sim card. duh! Kasheshe kweli kweli.
 
Sijaelewa. Kama ni hivyo huyo Kaka alijuaje tunapanda Hilo bus , alijuaje tunasafari hiyo siku, Alijuaje seat namba?? Nadhani Ni mchezo unaofanyika kivingine Hawa wanalenga wasafiri
Ndiyo maana mimi naamini kuna ndugu wa karibu alihusika kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma.Mtu pekee ambae anaweza kuwa na hizo data za safari hadi seat number ni ndugu wa karibu!
 
Angalia statement ili mjue Ni muda gani exactly muamala ulifanyika. Isiwe ikawa kuna njia siju hizi mtu akiwa na simu yako akapata password kwa kutumia gadget fulani labda anaichomeka tu kwa mini usb/ charging port .

Kama muamala ulifanyika mida hio mkiwa kwa basi, itakuwa akipata password
Muda muamala ulifanyika Ni muda Tulikuwa ndani ya bus
 
Ndiyo maana mimi naamini kuna ndugu wa karibu alihusika kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma.Mtu pekee ambae anaweza kuwa na hizo data za safari hadi seat number ni ndugu wa karibu!
Mkuu hakuna mtu alijua bus tunalopanda. Tulichagua bus tukiwa stand na mtu mwenye namba ya Siri ya mama Ni mdogo wangu Yuko shule. Hakuna mwingine that's why siamini Mambo ya Mtu kutufanyia mchongo. Hii ni game jipya la utapeli
 
Habari zenu wakuu.

Jana mama yangu katapeliwa hela kutoka TigoPesa. Nilimsindikiza Ubungo mida ya mchana tukapanda basi kwenye ile seat aliyokaa tukamkuta mkaka amekaa dirishani kwasababu mama siti yake ni dirishani na tulikuwa tumewahi sana, akatupisha akasema nawaacha mkae pamoja kidogo mpige story siti yangu ni ya pembeni akaenda siti ya nyuma.

Baadae kidogo akarudi ikabidi niinuke nimpishe akae siti yake. Akamuuliza mama unasalio naomba nipige mama akijua ni msafiri mwenzake akampa simu, akajifanya nampigia hapokei akarudisha Simu, Mara hiyo hiyo akashuka akasema Naenda kununua vocha.

Jioni mama amefika nampigia ananambia yule mkaka hakurudi kwenye bus. Ile siti haikuwa yake alikuja kukaa mtu mwingine, nawaambia siti Ina mtu Hadi konda akaja akasema hii siti sijaikatia ticket.

Nikas-ense something is wrong nikamwambia mama ameshika simu yako na hakurudi kwenye bus kuna kitu kafanya angalia salio lako la TigoPesa. Kweli kuangalia salio limekombwa loooteeee.
Tuliangalia Taarifa ya miamala pesa imetumwa namba 0719169535 na muda uliyotumwa Ni muda ambao Tulikuwa ndani ya bus. Kweli imetuumiza sana

Usalama wa pesa zetu kwenye mitandao ya simu upoje? Hawa wezi wanajuaje namba zetu za siri?

Mimi nimeogopa kwenye simu saivi siachi zaidi ya elfu 5 na kujifanya mwema kumpa Sim mtu nisiyemjua never.
kuna njia 2 za kutoa hela kwenye simu ya mtu hata kama hujuani nae au hujui password zake,njia moja unaweza kuvhkua hela simple kuptia app ya tgo pesa,na nyingine bila tgo pesa kwa kuptia, na mwsho ni kuptia bank account yako usirogwe narudia tena usirogwe kumpa mtu au kuacha hovyo card yako ya bank ni ndani ya dakika 10 tu zinarltosha kuhamisha kila cent ndani ya account yko.

All in all
njia zote hizo zinarisk hasa kama mwizi huyo atanogewa kwani anakozirusha hela kama aliyeibiwa ataamua kuzfatilia lazma watakudaka baadae
 
Mpumbavu sana. Hakuna cha maana ulicho-post hapa. Hebu USITUHARIBIE JUKWAA. Pita hivi
Nisikuharibie jukwaa wewe na nani? Mtt wa kiume unakiherehere kama demu au we ni mchele coca unapakuliwa?
 
Muda muamala ulifanyika Ni muda Tulikuwa ndani ya bus
Basi kwisha habari jambo lilifanyika, sasa na msg ya muamala mliikuta? Na je ilitumwa kwenye namba gani hiyo namba ndiyo ya kuifutilia
 
Basi kwisha habari jambo lilifanyika, sasa na msg ya muamala mliikuta? Na je ilitumwa kwenye namba gani hiyo namba ndiyo ya kuifutilia
Namba nimeiweka kwenye post hapo. Hatukuikuta message ya muamala baada ya kushtuka tumeibiwa tukacheck Taarifa ya miamala tukaona namba
 
Sijaelewa. Kama ni hivyo huyo Kaka alijuaje tunapanda Hilo bus , alijuaje tunasafari hiyo siku, Alijuaje seat namba?? Nadhani Ni mchezo unaofanyika kivingine Hawa wanalenga wasafiri
Hutakaa uelewe kwasababu hujaunganisha angalau codes zangu,nimezungumzia kusafiri pia ila kunakitu ngoja nikupe tofauti na hii mbinu yetu Mpya
Unaanzaje kumtumia mtu pesa halafu badae unajua umetaperiwa iko hivi mfano ww unafanya biashara ya dukani na unarafiki yako anaitwa john mnaaminiana Sana kwenye biashara anatokea taperi anakupigia oya niambie boss nimepewa namba yako na john kuna sukari kubwa 20 hapa za dili vipi unahitaji utamwambia poa nahitaji ili kuhakiki utampigia john kinachofanyika tunahack namba ya john kupitia divert na hapo ni ishu ya dakika 10 tu kuna mtu atakuwa na simu ya john ukishapiga anapokea taper anayejua kukopi sauti ya john anakwambia freshi fanya nae kazi ukiwa huna hela ndakwambia sasa tuma elfu 50 ili nizifikishe kwako ukituma unakuwa umeisha
Kama bado hujapata code hadi hapo utakuwa mgumu kuelewa
 
Siamini Sana Hilo. Hatukumwambia mtu yoyote Basi tunalopanda, Siti tulikatia palepale Ubungo Tena tulipewa ya Kwanza tukaikataa tukabadilishiwa ya pili ndo tukampata huyo tapeli amekaa hapo.

Naamini huu mchezo Matapeli wanajifanya wasafiri wanaomba simu wapige then wanaiba. Kuna jinsi wanacheza na system kujua password
System sio rahisi Kama unavodhani.apo Kuna uzembe ulifanyika kwa maza
 
Hutakaa uelewe kwasababu hujaunganisha angalau codes zangu,nimezungumzia kusafiri pia ila kunakitu ngoja nikupe tofauti na hii mbinu yetu Mpya
Unaanzaje kumtumia mtu pesa halafu badae unajua umetaperiwa iko hivi mfano ww unafanya biashara ya dukani na unarafiki yako anaitwa john mnaaminiana Sana kwenye biashara anatokea taperi anakupigia oya niambie boss nimepewa namba yako na john kuna sukari kubwa 20 hapa za dili vipi unahitaji utamwambia poa nahitaji ili kuhakiki utampigia john kinachofanyika tunahack namba ya john kupitia divert na hapo ni ishu ya dakika 10 tu kuna mtu atakuwa na simu ya john ukishapiga anapokea taper anayejua kukopi sauti ya john anakwambia freshi fanya nae kazi ukiwa huna hela ndakwambia sasa tuma elfu 50 ili nizifikishe kwako ukituma unakuwa umeisha
Kama bado hujapata code hadi hapo utakuwa mgumu kuelewa
Naelewa unachozongumzia Mkuu, Lakini kwa kesi yetu si hiyo story. Huu Ni utapeli Aina nyingine, watu kila siku wanakuja na mbinu mpya.
 
Back
Top Bottom