Utapeli mkubwa DSM: Beware

Kuna rafiki yangu mmoja (binti) wamempiga milioni moja na laki tisa.. alisubiri hapo Airport mpaka amekoma hakuna cha mzungu kutokea wala nini... na hela yenyewe alikua amekopa.
...Nini uvivu wa kufanya kazi au???
 
Hivi, mtu akikuambia anakufahamu anakutajia na majina ya watu wako wa karibu sijui ndugu zako, birthday yako, ya baba yako, jina la mbwa na paka wenu, na nyumba yenu, on top of that ni "mzungu", halafu wewe HUMJUI na wala maishani mwako hujawahi kumsikia, hii yenyewe tayari inatosha kabisa kuwa na wasi wasi.
 

Hii kali, au jamaa wanatumia na nguvu za giza?
 

Ni kweli kabisa, mara nyingi kama si zote "shortcuts are wrong". Tutumie vyema elimu zetu, akili zetu na nguvu zetu kufanyakazi kwa bidii kujiletea maisha bora.
 
Hii kali, au jamaa wanatumia na nguvu za giza?
Ndivyo inavyosemekana. Ila kufanikisha hii sanaa kupitia simu napata shaka.
Inawezekana mhanga ni mtu aliyewahi kupelekwa kwa waganga? (Kuchanjwa hivi na mambo kama hayo?)
 
Ndivyo inavyosemekana. Ila kufanikisha hii sanaa kupitia simu napata shaka.
Inawezekana mhanga ni mtu aliyewahi kupelekwa kwa waganga? (Kuchanjwa hivi na mambo kama hayo?)

Mkuu mbwa mvivu... hakuna cha waganga wala nini! yaani wanakutafuta tu kama una tamaa ya pesa lazima uingie kingi! Mi mtu nnayemfahamu wakati anaingizwa kingi ungemuona anavyojitapa kuwa kaukwaa utajiri wa ghafla ungesikia wivu
 
Waungwana huu ni mtandao mkubwa sana,wako smart kimavazi,wanatumia magari mazuri mfano GX 110,mie walitaka kunipiga kwa kuniuzia MERCURY.kabla ya kununua nikaona bora nipate soko kwanza,nikakutanishwa na mnunuzi maeneo ya Lugaro jeshini ambaye alikuwa mzungu Mr Steve toka Ujerumani ambaye pia ni mwezao.Aiyeniokoa ni Mr wangu kwani nilikuwa ninaomba aniongezee cash.Mtandao huu una lugha zao,mfano anayetaka kupigwa wanamwita ZOBA,zoba mjanja mjanja anaitwa Man'gaa,Ukigundua kuwa anataka kupigwa wanasema Zoba limepata MASEKE!!,Wameibiwa wengi sana hata viongozi ambao hawawezi kusema kwa kuona aibu!!!
 
Hivi sijaelewa kitu kimoja wakuu, mtu akikwambia taarifa zako zooote hadi siku uliyopata tohara ndio unatakiwa ukubali kumuamini au ni vipi? kwani kufanya biashara na mtu ni lazima awe anakujua sanaaaaaaa? Uvivu wa kufikiri tu na woga wa kuuliza maswali.
 


Yale yale ya ile deal ya kutoa dola 300 upatiwe kazi, ni kutumia akili tu kama mtu anakwambia atakulipia tiketi kwenda huko kazi iliko na atalipia gharama za visa lakini utangulize dola 300, you dont need to have a PhD kuelewa kwamba hapa unaingizwa mkenge. It is clear that once they get the money they are gone!
 


Hii ya viongozi na wakuu wa mashirika ya umma imetokea sana, sema wanaona aibu kusema! Hawa matapeli mara nyingi wanawapigia wakuu wa mashirika ya umma ama wafanyabiashara kwa kujifanya mawaziri (wanaiga sauti) na kuwatoa upepo. Sometimes wanadai wameishiwa vocha na wako remote areas kama vile njiani kutoka Dodoma ama jimboni!.watumiwe kama laki mmoja, na kwa sababu unajua ni Mheshimiwa anapiga huhitaji kuhoji sana, ni kuzama mfukoni tu!

Walishawahi kutaka kumliza Tido Mhando wa TBC kwa kudai mpigaji ni waziri yulko Dodoma wakati Tido alirudi jioni hiyo na waziri toka Dodoma, hapo ndo akajua kanyaboya!!!!
 

Mkuu ulimpoteza mwizi tapeli hivihivi??? Yaani ungeandaa kabisa police au kwa haraka unakamata namba za gari, au unamwambia subiri ukachukue cash kumbe cash yenyewe ni askari kanzu. Siku nyingine usifanye kosa, fanya kweli.
 

Umesahau kuwa alilizwa makongoro Mahanga?
 
Ni suala la kufuatilia habari tu mkuu na interest! Habari ya Tido Mhando ilirushwa TBC na kuelezea mkasa mzima.


Wanawaibia mazoba na mafala tu. Watu wajanja hawaibiwi.

Nyie woote mlioibiwa ni sawa na wale wanachama wa Deci. Hivi Deci imeishia wapi?

Mitanzania mijinga sana!!
 
kweli hii ni bongo tambarare- watuhumiwa wanajulikana kwanini awakamatwi??
 
Wanawaibia mazoba na mafala tu. Watu wajanja hawaibiwi.

Nyie woote mlioibiwa ni sawa na wale wanachama wa Deci. Hivi Deci imeishia wapi?

Mitanzania mijinga sana!!



Mkuu ungejua watu waliopigwa kwenye hili dili hata usingesema haya... wamepigwa watu na akili zao kisa wameongea na Mzungu kwenye simu!
 
Tunashukuru kwa information kama shule tumeipata ni sisi sasa kuwa makini na hizi deal za harakaharaka na kushilikiana na police inapowekana
 
duh! huu utapeli wa hali ya juu!
ila hapa ile post ya Yo Yo inakuwa direct applied kabisa. Wabongo tunapenda mijipesa mingi pasipo kuvuja jasho sasa ndio haya. By the way hapana sababu ya kuwaona waliotapeliwa kuwa ni mazoba la hasha, haya ni mambo yanayotokea na kupitia these experiences tuna learn ambao bado hatujakumbwa na zahama hili.
Asante mtoa hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…