Utamwambia nini Rais JK?

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Mwana fikra pevu!! Assume umepata nafasi ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete faragha na umepewa dakika mbili tu za kuongea nae. Ni kitu gani utapenda kumwambia kwa maslahi ya Umma wa Tanzania??
 
Nitamwambia "rais nch imekushnda". Itisha uchaguz upya upumzke salama.
 
Tanzania ina mabilionea wengi . Acha kwenda kuomba omba washauri hawa mabillionea warudishe kiasi kwa jamii na Tanzania ya kufikilika utaipata.
 
vunja baraza la mawaziri, unda upya kama umejifunza kitu katika udhaifu walioonesha. Ngeleja afunguliwe mashataka
 
JK, umekuwa mpole sana na muoga wa kuchukua maamuzi. Awamu yako ya kwanza ulijaza rafiki zako, ukawa unawaonea aibu kuwachukulia hatua pindi wanapokosea. Awamu yako ya pili umejaza maadui zako ambao unawaogopa kuwambia chochote.
 
Mh. Jakaya Kikwete, CCM kujivua gamba, suala lisiwe kujisafisha tu bali kuleta maendeleo kwa wananchi

*Kama ni kweli kauli yako kuhusu kujivua gamba kama nyoka ulimaanisha CCM ni kama nyoka, ujumbe huo
utakuwa na maana kuwa tumeshang'atwa sana na nyoka (CCM) huyu na sasa utakuwa umetambua kile
kinacholalamikiwa muda mrefu na wananchi kuhusu IPTL, Deep Green, Meremeta, Richmond/DOWANS, EPA na
mengine kibao. Hivyo gamba jipya litusaidie kumwona nyoka huyo hata kama atajificha gizani.

*Kama kweli wewe na Chama Cha Mapinduzi mna nia ya dhati kujivua gamba na kuwatumikia wananchi,
mnapaswa muanze sasa kuwekeza katika kuhakikisha kunakuwepo uwiano sawa kwenye mgawanyo wa rasilimali
ili kwenda sawa na kaulimbiu yako ya "Maisha bora kwa kila Mtanzania".

*Najua unalewa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini kwa kutegemea jembe la mkono,
kipato wanachopata kutokana na kilimo cha aina hiyo hakiwasaidii kukidhi mahitaji yao muhimu ya kila siku. Ile kauli
ya mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ingekuwa na ukweli, wananchi wa Tanzania wangekuwa matajiri.

*Rais, wananchi wanalalamika kuwa wakija mijini hali bado ni ngumu wakati nyinyi tuliowapa dhamana ya kuweka
mazingira hayo mmelala usingizi na kufikiria jinsi ya kutengeneza mikataba feki ili mchote fungu mnaloliona lipo 'idle' .

*Ni wakati sasa uelewe kuwa Watanzania siyo wavivu kama unavyofikiria, uchumi siyo kutoa takwimu tu bali
kuwawezesha Watanzania kuwa na matumaini ya kuuza mazao yao kwa wakati kutoka mashambani. Kwa hiyo kujivua
gamba kwa chama chako kusiishie kwenye kubadilisha uongozi tu, unapaswa uyaone haya na kuyatekeleza kivitendo.

Naomba kuwasilisha...
 
hivi mkuu unasikiaje kudharauliwa kuhusu utendaji wako wa kazi,na mkuu naona uvunje ule mtandao wako wa mabest zako iwe chapa kazi au chapa lapa...
 
mie ningepewa dakika 2 tu za kukaa naye .............ngoja nisiseme, nina hasira naye.
 
Mh. Jakaya Kikwete, CCM kujivua gamba, suala lisiwe kujisafisha tu bali kuleta maendeleo kwa wananchi

*Kama ni kweli kauli yako kuhusu kujivua gamba kama nyoka ulimaanisha CCM ni kama nyoka, ujumbe huo
utakuwa na maana kuwa tumeshang'atwa sana na nyoka (CCM) huyu na sasa utakuwa umetambua kile
kinacholalamikiwa muda mrefu na wananchi kuhusu IPTL, Deep Green, Meremeta, Richmond/DOWANS, EPA na
mengine kibao. Hivyo gamba jipya litusaidie kumwona nyoka huyo hata kama atajificha gizani.

*Kama kweli wewe na Chama Cha Mapinduzi mna nia ya dhati kujivua gamba na kuwatumikia wananchi,
mnapaswa muanze sasa kuwekeza katika kuhakikisha kunakuwepo uwiano sawa kwenye mgawanyo wa rasilimali
ili kwenda sawa na kaulimbiu yako ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania”.

*Najua unalewa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini kwa kutegemea jembe la mkono,
kipato wanachopata kutokana na kilimo cha aina hiyo hakiwasaidii kukidhi mahitaji yao muhimu ya kila siku. Ile kauli
ya mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ingekuwa na ukweli, wananchi wa Tanzania wangekuwa matajiri.

*Rais, wananchi wanalalamika kuwa wakija mijini hali bado ni ngumu wakati nyinyi tuliowapa dhamana ya kuweka
mazingira hayo mmelala usingizi na kufikiria jinsi ya kutengeneza mikataba feki ili mchote fungu mnaloliona lipo 'idle' .

*Ni wakati sasa uelewe kuwa Watanzania siyo wavivu kama unavyofikiria, uchumi siyo kutoa takwimu tu bali
kuwawezesha Watanzania kuwa na matumaini ya kuuza mazao yao kwa wakati kutoka mashambani. Kwa hiyo kujivua
gamba kwa chama chako kusiishie kwenye kubadilisha uongozi tu, unapaswa uyaone haya na kuyatekeleza kivitendo.

Naomba kuwasilisha...

Baada ya kujivua gamba, unapaswa kuwaomba radhi Watanzania ukifuata mfano wa aliyekuwa
Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Yohane Paulo II aliyeomba msamaha mwaka 2000 kwa
niaba ya Kanisa Katoliki kwa makosa yaliyofanywa miaka mingi sana iliyopita na watendaji wa
kanisa hilo.

Ili wewe na CCM yako mmeremete na muaminike tena kwenye jamii kuwa mnachokifanya si
propaganda, tuombeni radhi haraka.
 
Ushikaji/marafiki...ume/wameku'cost,,,,,yani hauwezi kumfukuza mtu kwenye nafasi uliyompa mwenyewe?.......Una'manage mambo by crisis!Badala ya MBO(Management by Objective)......ovyo kabisa.
 
Mh JK, kuna power vacuum tangu uingie madarakani, watz walizoea ubabe wa Mkapa, sasa kuwa mbabe na wewe.
 
Mh. Jakaya Kikwete, CCM kujivua gamba, suala lisiwe kujisafisha tu bali kuleta maendeleo kwa wananchi

*Kama ni kweli kauli yako kuhusu kujivua gamba kama nyoka ulimaanisha CCM ni kama nyoka, ujumbe huo
utakuwa na maana kuwa tumeshang'atwa sana na nyoka (CCM) huyu na sasa utakuwa umetambua kile
kinacholalamikiwa muda mrefu na wananchi kuhusu IPTL, Deep Green, Meremeta, Richmond/DOWANS, EPA na
mengine kibao. Hivyo gamba jipya litusaidie kumwona nyoka huyo hata kama atajificha gizani.

*Kama kweli wewe na Chama Cha Mapinduzi mna nia ya dhati kujivua gamba na kuwatumikia wananchi,
mnapaswa muanze sasa kuwekeza katika kuhakikisha kunakuwepo uwiano sawa kwenye mgawanyo wa rasilimali
ili kwenda sawa na kaulimbiu yako ya "Maisha bora kwa kila Mtanzania".

*Najua unaleewa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini kwa kutegemea jembe la mkono,
kipato wanachopata kutokana na kilimo cha aina hiyo hakiwasaidii kukidhi mahitaji yao muhimu ya kila siku. Ile kauli
ya mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ingekuwa na ukweli, wananchi wa Tanzania wangekuwa matajiri.

*Rais, wananchi wanalalamika kuwa wakija mijini hali bado ni ngumu wakati nyinyi tuliowapa dhamana ya kuweka
mazingira hayo mmelala usingizi na kufikiria jinsi ya kutengeneza mikataba feki ili mchote fungu mnaloliona lipo 'idle' .

*Ni wakati sasa uelewe kuwa Watanzania siyo wavivu kama unavyofikiria, uchumi siyo kutoa takwimu tu bali
kuwawezesha Watanzania kuwa na matumaini ya kuuza mazao yao kwa wakati kutoka mashambani. Kwa hiyo kujivua
gamba kwa chama chako kusiishie kwenye kubadilisha uongozi tu, unapaswa uyaone haya na kuyatekeleza kivitendo.

Naomba kuwasilisha...

Maneno yote haya na alivyo mvivu na kila*a sidhani kama atakusikiliza!!
 
yule jamaa naona ni aina ya 'charismatic' na si ajabu ukajikuta na wewe uaanza kuwa na fikira kama zake!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom