Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa blog hii kupitia kwa mama chanja. Sijawahi kuwa mwanachama hapa. Kuna tabia inanikera ambayo nilimuomba aikemee lakini akakataa kata kata kwa kuogopa kutengwa. Tabia hii ya wake za watu ama waume za watu ambao waliwahi kuandika wamo kwenye ndoa. Hawa wameanzisha tabia ya kujionyesha wamo kwenye mapenzi motomoto na kuitana majina ya kimapenzi na wapenzi wao bila hata kuonyesha woga wa kuwemo kwenye ndoa. Pia baadhi ya marafiki zao huwapongeza hadharani kwa kuwemo kwenye mapenzi motomoto. Sijui kama uongozi wa blog hii unakubaliana na tabia hii ya kuifanya iwe kama danguro kwa waliomo kwenye ndoa kuonyesha mapenzi moto moto hadharani. Kama uongozi wa blog hii unaona athari ya tabia hii chafu ya wake za watu na waume za watu kujianika hadharani na mapenzi ya nje ya ndoa, basi uongozi uzuie tabia hii haraka sana kabla haijawa tatizo kubwa kupita kiasi.