Hapo ndio unasikia kwa uwezo wa kibinadamu unakuwa umefika mwisho, lakini kwa uwezo wa Kimungu hakuna lisilowezekana, muujiza wa Mungu pekee waweza kumnusuru kutoka hapo alipo, jibu ni kujikabidhi kwa Mungu ili apate kutenda kadri ya mapenzi yake.
Kuna mwandishi mmoja wa kitabu kiitwacho stop worrying and start living katika moja ya andiko lake katika tafsiri ya kiswahili isiyo rasmi anasema "Mungu nijalie hekima ya kuweza kuelewa mambo ambayo naweza kuyabadilisha na yale ambayo siwezi, na unijalie kujua tofauti kati ya mambo hayo".(mwisho wa nukuu).
Mtu ukiwa katika hali kama hiyo huna budi kukubaliana na usemi huo na kumwachia Mungu nafasi yake maana kwa uweza wa kibinadamu inakuwa ngumu sana.