Kuongezea Kwenye Point ya Alibakari, Ukweli ni kwamba unatakiwa kuwa muangalifu sana watengenezaji wa simu feki wameshajua kuwa watu wengi wanangalia simu fake kwa kutumia code hizo hivyo zipo simu fake zenye kuonyesha code hizo lakini kwa kuangalia tu kwa macho yako pamoja na kuongezea na test alizotaja Alibakari unaweza kupata simu original.
Kwa mfano ukiangalia kwenye picha hapo juu utaona utafauti ambao unaweza kuona kwa haraka kwa kuangalia namba zilizo wekwa kwenye picha.
1. Kioo kinakuwa na mwanga hafifu na kinakuwa kimetengenezwa kwa plastick au glass ya bei rahisi.
2. Upana wa kutoka kioo mpaka ukingo kwenye simu feki unakuwa ni mkubwa sana
3. Kioo kinakuwa akina mwanga wa kuosha au kinakuwa na mwanga hafifu
4. Utakuta kuna baadhi ya Sensor ambazo hazifany kazi (hivyo ni vizuri kufuata hatua za alibakari ili kujua kama senseor zote zinafanya kazi)
5. Kibonyezo cha katikati (home botton) kwenye simu feki kinakuwa hakiko mahali kinapotakiwa
6. Logo ya samsung unapoigusa kwa kidole kwenye simu feki utaisikia kabisa ikikwaruza kidole yani haitakuwa smooth
Hayo tu ni machache ni vyema kuwa makini kwani njia hizi sio kwamba ndio zinaonyesha moja kwa moja hivyo ni vyema kuwa makini. Pia unaweza kuingia
kwenye ukurasa huu wa TCRA kisah weka imei namba na utapata jina la simu kama itakuletea tofauti basi hiyo simu ni feki.
NATUMAINI ITAKUWA IMEKUSAIDIA