Utakuwa TEGEMEZI hadi lini best?

Utakuwa TEGEMEZI hadi lini best?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Wasaalamu waungwana,

Leo sina furaha sana kusema yangu machache,
yaliyoujaza moyo wangu na kuleta simanzi upeoni,
nashindwa kuelezea wala kupambanua nini hasa,
kilichowapata waungwana hasa hawa madada zetu.

Napenda nitoe yangu ya moyoni kwani wanaume wa humu jf wamesema kuwa
nawafunda peke yao na wala siwafundi wanawake wenzangu, Sasa leo nimeona
nitoe kadarasa kadogo hapa kwenu nyie madada, wanawake,wenzangu wa humu
naomba msinichukie kwani nimeona nanyi inabidi mfundwe kidogo kwani mmjesihau
na kusahau nafasi/mchango yenu katika jamii. Kwani usipomerimisha mwanamke
hujaelemisha kitu kwani mwanamke ni tegemeo lkwa Taifa na ni kipaumbele cha
TAIIFA.

Wapendwa marafiki zangu wa jf chitchat leo tena nimeingia mjengoni kwa style ya
kushairi zaidi nikiwafunda hasa wanawake wenzangu ambao wao hawana fikra za
kupembua wala kuchuja na wala kutafakari lipi lililo jema kwao. Kazi yao
kubwa wanayowaza ni kuremba na kujionesha kwa wenzao leo wametokelezeaje?
hawana la kutaka kujua watafanya nini hili wajikwamue katika hali walizonazo, kazi yao
kubwa ni kusemanana na kuomba pesa kwa marafiki zao hususani wa jinsia nisiyotaka
kuitaja hapa kwani inani............. jaza hapo

Wanawake wenzangu napenda leo niwape somo yaani niwafunde
kidogo kuhusu maisha kiujumla, wewe rafiki yangu kazi yako kubwa
ni kukaa kibarazani na kusubir mzee alete jioni mahitaji ya hapo kwako
wewe mwenyewe unashindwa nini kutafuta na kuchakarika kwa mikono
yako kutafuta maihitaji ya muhimu ili msaidiane katika familia kutunza
na kulea jamani, yaani wadada wenzangu wa siku hizi sio wote wa humu
mjengoni jf bali wako wachache wanaotuponza na kutufanya tuonekane
si bora si chochote, ni magolikipa tu. Mwanamke mwenzangu inakushinda
nini kutoka na kwenda kutafuta pesa wewe unangoja ukinge tu mikononi
kwanini unakuwa TEGEMEZI kwa kila kitu na wakati akili, ufahamu, ujuzi wa
kutafuta umepewa na Mungu kitu gani kinakushinda usithubutu kufanya lile
unaloweza kufanya kwa mikono yako na Mungu atakusaidia. Kwani
unafikiri mafanikio yako yako kwa Mwanaume au unafikiri kuwa wewe uliumbwa
kkukaa tu na sio kutafuta pesa, acha hiyo dhana ya kuwa tegemezi kwa kila
kitu hadi vitu vya ndani jamani mdada, mwanamke mwenzangu chakarika utaona
matunda ya mikono yako,

Napenda niwaase kidogo kwani kuwa tegemezi sio kuzuri kabisa na kunarudisha
maendeleo yakio nyuma kwani kuna wakati baba atasema leo sina utafanya nini?
Hebu thubutu kuchakarika na kutafuta mpenzi wangu utayaona mafanikio kwako
na raha zaidi ni kutafuta na sio kuwa teegemezi best, achana na hiyo dhana ni
potofu best, tafuta chako ule kwa raha zako bila kugombwa na mtu yeyote.
Fanya kile unachoweza kufanya kiwe ni kusuka, kupika, kuwa na duka, kuwa na
salon, ilimradi tu kinakuingizia kipato chako kwani ukifanya hivyo itakufanya uwe
huru na pesa uliyotafuta kwa mkkono na jasho lako, pesa ya kupewa mara nyingi
haitoshelezi mahitaji yako , tafuta yako nawe utafanikiwa.

Nakupa onyo best rafiki wa moyoni penda kutafuta chako kwani wanaume wa siku
hizi wanachoka haraka kwa wake ambao ni magolikipa wewe jifunze kuanzisha chako
nawe utaffanikiwa na ikiwezekana mwambie mumeo akufungulie mtaji ili uanze biashara
yako hapo atakuona wa maana na mtaenjoy life pamoja bila woga wala mushkeli yeyote
kila la kheri mabest zangu msinikasirikie nishatoa shairi langu lenye fumbo mioyoni mwenu
Nawapenda wote sina kinyongo nanyi nawatakia kila la kheri katika mafanikkio yenu
Nawapenda
 
Wazo zuri kina mama watakuwa wamekuelewa. Mimi kwa upande wangu sipendi kuwalaumu sana akina mama wasiofanya kazi na hili jina la golikipa silipendi hata kidogo. Mama zetu wana kazi nyingi nyumbani zaidi yetu tunaojiona tunafanya kazi. Ikumbukwe toka wakati wa kuumbwa mwanadamu kila jinsia ilipewa majukumu yake na mwanaume alipewa jukumu la kutunza familia kwa hiyo wanaume wasipende kukimbia majukumu kwa kutaka kusaidiwa na wamama. Wengi wa wanawake tunaowaita hayo majina sipendi kutaja hawana kiwango kile cha elimu kuwawezesha kufanya kazi zenye tija, badala ya kuwabeza kwamba ni tegemezi tutoe ushauri wa kuwaendeleza kielimu.
 
sisemi vibaya kuhusu kusema golikipa nina maana nzuri tu besti na wala siwabezi wale wasio na elimu kuwafumbua macho waone mwanga ulioko kwao kwani hata kama hana elimu uwezo/ufanisi/akili anazo za kuwaza ni mbinu zipi afanye ili aweze kuingiza kipato chake yeye mwenyewe na sio kuwa Tegemezi , ninaposema tegemezi sisemei kuwa mwanamke hana la kufanya analo anapika home analinda familia na nyinginezo ila nasemea awe anajishughulisha hata kwa biashara ndogondogo kwani izipo za kufanya kama kuuza chapati, vitafunio mbalimbali na sio kukaa barazani na kuanza kusema hovyo watu wapitao barabarani jamani hukunielewa best

Ila nakumbuka siku1 my husband Mentor aliniwezesha kitu lakini kilikuwa kidogo tuambie wewe namna gani hiyo tena ya kuwezeshwa hebu toa mojawappo tuone,
Ipo namna unawezeshwa. Wewe tu hujajua.
 
Last edited by a moderator:
Nimekuelewa best ila suala la mwanamke kufanya kazi pia linategemea na mila na desturi za sehemu husika mfano kule uarabuni nasikia wanawake hawafanyi kazi
sisemi vibaya kuhusu kusema golikipa nina maana nzuri tu besti na wala siwabezi wale wasio na elimu kuwafumbua macho waone mwanga ulioko kwao kwani hata kama hana elimu uwezo/ufanisi/akili anazo za kuwaza ni mbinu zipi afanye ili aweze kuingiza kipato chake yeye mwenyewe na sio kuwa Tegemezi , ninaposema tegemezi sisemei kuwa mwanamke hana la kufanya analo anapika home analinda familia na nyinginezo ila nasemea awe anajishughulisha hata kwa biashara ndogondogo kwani izipo za kufanya kama kuuza chapati, vitafunio mbalimbali na sio kukaa barazani na kuanza kusema hovyo watu wapitao barabarani jamani hukunielewa best
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom