Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Yeye ilikuwa sio kwa ajili ya utajiri,bali ilikuwa ndio mtindo wake kabla hajatoa wimbo/album alikuwa anatambika kwa mizimu ya kwao ambapo alikuwa anajifungia ndani kwenye chumba maalumu hata kwa wiki mbili anakuwa kama kafariki. Kosa lililofanyika ni Mama yake alipokwenda kwake na kuingia humo chumbani ndio akafa moja kwa moja.
Duh....kwahiyo ndugu stori ya KABASELE la MPANYA inaukweli ndani yake!
 
[emoji23] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Ni aina mojawapo ya uchawi wa kupata utajiri ukiacha huu wa ;
kuua ndugu
Kuwafanya wanafamilia ndondocha
Kuwekwa kidonda mwilini
Kupewa masharti ya chakula nguo na magari nk nk
Huu una mambo yake ya ajabu, unapewa dawa ambayo utamshirikisha mkeo tuu....ukishakunywa hiyo dawa unakufa na kuoza kabisa mpaka kutoa funza wengi
Sasa mkeo kazi yake kila siku itabidi awafagie hao funza na kuwaweka kwenye ndio kwa mpaka siku ya saba utakapofufuka..... utajiri wako utategemea na wingi wa funza watakaokusanywa kwa siku
Ukishamaliza siku Saba utafufuka na biashara zako zitaanza kuchanganya
Onyo na tahadhari
-hutakiwi kuwa na mwanamke mwingine
-mkeo hapaswi kushtuka mara ya kwanza akiwaona funza utakufa moja kwa moja
-so wewe wala mkeo mnapaswa kutoa siri hii kwa yeyote hata chini ya mtutu wa bunduki
-Ishu ya kufa wiki nzima na kuoza utaifanya kila biashara zinapoyumba
Kama bado unataka utajiri kwa njia za mkato fikiria mara mbili kabla hujamua
umesema kweli mkuu, namfahamu tajiri mmoja hapa nchini yeye anaoza na kutoa mafunza kila baada ya mwezi na huchukua wiki nzima kurudi kwenye hali ya kawaida huku akisubiri mwisho wa mwez mwangne ufike,yaani muda wte anatembea na begi la manukato..

kweli Kama bado unataka utajiri kwa njia za mkato fikiria mara mbili kabla hujamua
 
Back
Top Bottom