Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 34,611
- 59,734
Mkuu nishafanya research mpaka nimeamua kupoteza tu cz design nimeona nikifatilia sana such stuff naweza nikawa tempted to try it. Lol
You know i dont wanna do that shit. Tehe... Patience and working smart is the talent. Hela za ndago sio issue Joh. Muamini Mungu.
Issue inakuja unajilinda vp na mafirauni kama hawa ??? Inabdi uwe fit kiimani pia. Imagine Mangi kakuficha ki mazingara kwenye store ya hardware. Noma sanaa Joh. Hahahaha
Ila wangetoka kaskazini ndo matajiri halali wakitoka kusini sio halali toa evidence ya uchawi kwa Wakinga
Mwaka we neema huu kwa wanahabari,wapambe na WAGANGAwanasiasa muda huu wapo karibu kinoma na waganga na wagaguzi
Siamini katika uchawi.
Aaaah bwana wewe acha ibishi bwana, wakinga wengi walipata utajiri kwa njia za majoka.... unajua nini kuhusu mwakipande
kwani wewe umeleta hoja gani zaidi ya kupiga porojo za vijiweni?
Utajiri ni mmoja tu ndugu,hakuna wa ushirikina wala wa nini...umeshafatilia maaharti mengine wanayopewa hao watafuta utajiri kwa waganga,mwisho utakuta masharti hayo yanawarudisha kulekule kwenye kufanya kazi kwa bidii na si kwenda kulala miguu juu kusubiri hela zitoke hewani...waganga ni wajanja..hutakiwi kuamini wanachosema hata waseme wangapi
kujiuliza tu huyo mganga yeye mbona maskini? ila mwisho wa utajiri wa hivyo ni mbaya mpaka tena unaona huruma
Ua ryt mdau kabisa,,,,,,,,,,,,,,,,MAJINI yametajwa sana kwenye QUR'ANBulldog mapepo na majini Vipo na ni roho zinazotangatanga unaweza usiamini lakini kumbuka hata kwenye misahafu haya mambo yameongelewa kwa mapana yake
Kuna ile habari ya Bwana Yesu kuwaamuru mapepo wamtoke yule mtu nayo yakamuuluza tukitoka twende wapi? Akayaelekeza kwenda kwenye kundi la nguruwe ambao walitimka na kuingia baharini
Kiyoya hili jambo la kutafuta utajiri wa haraka limeitafuna jamii vibaya sana asilimia kubwa sana ya wafanyabiashara wanafanya haya mambo
Kuna hili kundi lingine ambalo watu hawalijui lakini nalo linafanya uchafu mwingi sana kwa maagizo ya waganga MAMA NTILIE NA WAUZA VYAKULA watu wanalishwa uchafu mwingi sana kwenye hii sekta epuka sana chakula cha mamantilie ambaye kamwe hali alichopika mwenyewe
Biashara ndogo nyingi kama saluni maduka ya nguo mafundi mbalimbali na hata kwenye mabar wote hawa ni mabingwa wa kwenda kwa waganga kusaka utajiri!tusivae miwani ya mbao wakati haya mambo yapo live kabisa kwenye jamii yetu
Umesahau ile wanawavalisha watoto wadogo vitu vyeusi wanaita eti dawa. Yaani mtoto akizaliwa wanatafta tambara jeusi wanafunga hayo madawa na kitovu cha mtoto eti dawa ili asidhurike na wachawi. Kwangu mimi naona ni upungufu wa Imani kabisa!Mbona mimi binafsi sijawahi wavalisha watoto wangu hizo kitu na wamekuwa na wanakua vizuri tu bila shida? Kinachonishangaza hata watu ambao wamesoma na kuelimika bado wanaizo imani!!Jirani yangu Daktari wa Ocean Road kamfunga mwanae hizo kitu, dah!!!Ni shida
boss hiyo ni imani yako tu.
wakinga wanatafuta hela mahali popote na wanaishi maisha ya kujibana ndio maana wanakuwa na mali pale wanapozipata.
matumizi mabaya ya kile kidogo unachopata yanakufanya usifanikiwe hata kidogo.
mkinga asubuhi anakunywa chai nyumbani, mchana analetewa chakula kutoka nyumbani, jioni anaenda kula nyumbani kwa nini asiwe na hela?
dukani kwake yupo yeye na mkewe ndio wauzaji akiweka msaidizi basi ni ndugu yake.
kwani wangapi wameenda kwa waganga na bado biashara zikagoma/kuanguka?
siku zote hata kwa anayetegemea mshahara, matumizi mazuri ya anachopata ndio mafanikio yake.
sio mtu kila siku asubuhi anaamkia supu ya kuku, mchana nyama choma na jioni kitimoto na bia juu.
huyu hawezi kufanikiwa.
Utajiri ni ile hali ya kumiliki mapesa mengi na kuwa na mali nyingi, utajiri ni mzuri kwa kuwa unakupa uwezo nguvu mamlaka sifa na umaarufu!kwa kifupi Utajiri ni kitu chema.
Watu wengi hutafuta utajiri kwa njia mbalimbali halali na haramu wao wanachotaka ni utajiri ili waweze kutimiza ndoto zao nyingi.
Sasa kuna wakati mtu hutafuta utajiri kwa njia za mkato hapa nazungumzia kwa njia za ushirikina na uchawi.
Utajiri huu ni mzuri na huja haraka lakini ukiwa na masharti mengi lakini kubwa likiwa ni kutoa kafara la damu kwa kuangamiza roho.
Unapoingia kwenye utajiri huu mwanzoni utafurahia na masharti utayaona mepesi lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo hubadilika na tabu huanzia hapo.
Mwanzoni utaambiwa toa kafara la damu ya kuku baadae itakuja mbuzi, halafu itafuatia ng'ombe na mwishowe itakuja binadamu mmoja na hatimaye kwa makundi.
Hii yote ni kutaka kulinda utajiri wako usiporomoke na ukivunja masharti kila kitu kinaharibika .
Kuna pia masharti ya kujisaidia kulala kula kuvaa na hata matumizi ya vitu mbalimbali. Mwanzoni inakuwa ni rahisi tu kwenda sambamba nayo lakini mbeleni mambo hubadilika hasa pale watu wanapoanza kuhoji hiki au kile.
Wote tunajua jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inavyoteketea kutokana na waganga wa kienyeji kuwaaminisha wateja wao kuwa viungo hivyo vikichanganywa na dawa nyingine huleta utajiri bahati nguvu na uwezo! Kuna zaidi ya waganga 300 kwenye mahabusu na Magereza mbalimbali wenye kesi zinazowahusisha na mauaji ya albino.
Jamani utajiri wa masharti ya namna hii haufai na mwishowe huwa na anguko kuu tunashuhudia visa vya kila aina kuhusiana na utajiri wa namna hii lakini kila uchao watu hawakomi kuendelea kuutafuta.
Hakika dunia inaumwa.
mshana jr
Mimi nachojiulizaga hizo kafara huwa zina uhusiano gani na utajiri? yani ni process gani inafanya mtu apate hayo mahela baada ya kumuua ndugu/jamaa yake.
Mkuu palipo na damu kuna agano!!
Hili somo pana.
Sasa basi hakuna chochote kinachokamilisha agano/mkataba isipokua damu.na kumbuka kwenye hayo maagano/mikataba huwa kuna mashart!....
Sasa basi kinachofanyika kwa waganga baada ya msaka huo utajiri kuwekeana mkataba/agano,mashart pamoja na yote huambiwa leta kuku,mbuzi,ng'ombe, mtu kulingana na level ya utajiri though kwa kuanza wengi wanaanzia hapa chini yaani kuchinja kuku,mbuzi nk
Sasa hapa mganga anachofanya ni kidogo tu kuyaita hayo majini/mapepo ya utajiri na kuyaambatanisha na mhusika,so hizo roho au majini yanatii na kumfanyia kila kitu huyu mhusika anachotaka kulingana na mashart husika aliyopewa huko!!
Sasa kadri utajiri unapokua,ujue na kafara zinatofautiana ndo hufikia mahali zinatakiwa damu za watu!!!ss hapa ndo kasheshe ilipo!
Na pia inategemea mashart yenu mliyopeana Kule mwanzo!
Baadhi ya mashart unaweza kuta kila mzaliwa 1 kwny hiyo family anatolewa kafara,au kufanywa zezeta au hakuna kuoa/kuolewa,hakuna kufanikiwa ht ufanyaje,au kifafa kwa mtt 1 yaani mengi mno!!!
Nb,ubaya wa mashart hayo huwa yanabeba ukoo/familia nzima na hapa ndo shida!