Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Nipo mshana jr, hamna umasikini mbaya kama umasikini wa fikra. Ukiona mtu anataka utajiri kwa njia za ajabu ajabu ujue fikra zake ni masikini mno kiasi kwamba ameshindwa kufanya kwa uwezo wake sasa ameamua kuimport mashetani yamsaidie

au vp bwana
 
Last edited by a moderator:
Hiyo tena ni utumwa usioelezeka. Hela za nini kama huwezi kula vizuri, kuvaa vizuri au kujenga nyumba nzuri. Lisemwalo lipo, niliwahi kuijua familia moja ambayo hela kwao sio tatizo lakini ukibahatika kuwa kwao wakati wa mlo utashangaa wanafokula vyakula visivyofanana na uwezo walionao. Wanyetishaji wakasema eti wamepewa masharti... sheet, hizo hela ni za kutunisha A/C halafu basi!

Mie nna rafiki yangu mkinga, kwao matajiri wakubwa wana maduka mengi ya jymla na nyumba nyingi sana.Watoto wote wamesoma.Wanamiliki simu na vitu vya gharama sana na wanavaa vizuri tu.
Jamani ikifika muda wa kula ni vituko...maharagwe kama yameunguzwa kusudi, mboga za majani mchemsho.Dona gumuu na michumvi kibao.
Kah unawezq jua wanafanya kusudi.
Sioni mantiki ya kufanya biashara ukapata faida afu ukaishi vibaya.Ni uchizi.
Siku wakila nyama utadhani wanajipikilisha ni michuzi na haiivi vizuri
 
Masharti na miiko yana zingatia na ole wake mmojawapo aende nje akale chips kwa siri atazinya kama zilivyo
 
Mie nna rafiki yangu mkinga, kwao matajiri wakubwa wana maduka mengi ya jymla na nyumba nyingi sana.Watoto wote wamesoma.Wanamiliki simu na vitu vya gharama sana na wanavaa vizuri tu.
Jamani ikifika muda wa kula ni vituko...maharagwe kama yameunguzwa kusudi, mboga za majani mchemsho.Dona gumuu na michumvi kibao.
Kah unawezq jua wanafanya kusudi.
Sioni mantiki ya kufanya biashara ukapata faida afu ukaishi vibaya.Ni uchizi.
Siku wakila nyama utadhani wanajipikilisha ni michuzi na haiivi vizuri

sasa huo ni utajir au wendawazim.bora hata kasomesha watt ni mtaj usiofilisika
 
Other things remaining constant, Sioni sababu ya kuishi kama nakosa hvyo vitu vikuu vi 3. Hasa hyo option ya kwanza. Tehe

Tunatafuta utajiri ili tujitosheleze kimaisha na kufurahia kile ulichonacho kama huenjoy na una utajiri basi ni afadhali kubaki fukara
 
Nimewahi sikia eti kuna ule utajiri kuku anatupiwa punje akidonoa moja utaishi mwaka mmoja ila ni full bata akidonoa mbili ivo ivo but baada ya hapo lazima ufe.je kuna ukweli?
Cc. MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Hyo Biblia unayoisoma ww na kusema unaifuata (mafunzo ya Yesu) imeandikwa na nani ??

Wale wale wanadamu na mpango wao wa kumtafuta Mungu unaosema ww hawaja kamilika ndio hao hao waandishi wa Biblia unayoisoma ww na kui amini. (Note: Dini umeletewa na mzungu mwanadamu huyo huyo)

Nikiendelea kuku criticize ki maswali based on ur answers mwisho wa siku utajiona boya sanaaa.

Mpaka hapa nafkiri ushajikaanga tayari na mafuta yako mwenyewe.

Jipange.
Me huu msemo wa imeletwa na nani ndio hapo nachanganyikiwa sasa Kwani huyo Mungu atakuwa amewalenga wakina nani?

Yeah Mungu amewalenga wanadamu na hao wanadamu wema ndio Mungu anawatumia kwenye maagizo yake sio kama wanadamu wote ni wauwaji na waovu japo hao ndio waliolengwa na imani.

Na unatakiwa utambue Ukristo ni imani sio dini na hakuna race wala taifa lenye hatimiliki na imani ya Ukristo.
 
Ahsante. Umeeleweka.
 
Utajiri ni ile hali ya kumiliki mapesa mengi na kuwa na mali nyingi, utajiri ni mzuri kwa kuwa unakupa uwezo, nguvu, mamlaka, sifa na umaarufu! Kwa kifupi Utajiri ni kitu chema.

Watu wengi hutafuta utajiri kwa njia mbalimbali halali na haramu wao wanachotaka ni utajiri ili waweze kutimiza ndoto zao nyingi.

Sasa kuna wakati mtu hutafuta utajiri kwa njia za mkato hapa nazungumzia kwa njia za ushirikina na uchawi.

Utajiri huu ni mzuri na huja haraka lakini ukiwa na masharti mengi lakini kubwa likiwa ni kutoa kafara la damu kwa kuangamiza roho.

Unapoingia kwenye utajiri huu mwanzoni utafurahia na masharti utayaona mepesi lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo hubadilika na tabu huanzia hapo.

Mwanzoni utaambiwa toa kafara la damu ya kuku baadae itakuja mbuzi, halafu itafuatia ng'ombe na mwishowe itakuja binadamu mmoja na hatimaye kwa makundi.

Hii yote ni kutaka kulinda utajiri wako usiporomoke na ukivunja masharti kila kitu kinaharibika .

Kuna pia masharti ya kujisaidia, kulala, kula, kuvaa na hata matumizi ya vitu mbalimbali. Mwanzoni inakuwa ni rahisi tu kwenda sambamba nayo lakini mbeleni mambo hubadilika hasa pale watu wanapoanza kuhoji hiki au kile.

Wote tunajua jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inavyoteketea kutokana na waganga wa kienyeji kuwaaminisha wateja wao kuwa viungo hivyo vikichanganywa na dawa nyingine huleta utajiri, bahati, nguvu na uwezo! Kuna zaidi ya waganga 300 kwenye mahabusu na Magereza mbalimbali wenye kesi zinazowahusisha na mauaji ya albino.

Jamani utajiri wa masharti ya namna hii haufai na mwishowe huwa na anguko kuu tunashuhudia visa vya kila aina kuhusiana na utajiri wa namna hii lakini kila uchao watu hawakomi kuendelea kuutafuta.

Hakika dunia inaumwa

😎🙁:banghead:😎
 
just imagine, lengo sasa linabaki kuwa una hela ili watu wakuone/wakujue, lakini kufaidi hufaidi ng'ooo
 
Back
Top Bottom