Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

MSHANA UNA FIX SANA UJUE BASI TU NAKUHESHIMU. HAKUNA UTAJIRI WA KICHAWI KAMA ULIVOELEZA MKUU

Wale wenye utajiri ambao unakuta hawana uhuru wa kufanya kitu fulani; mfano kuvaa nguo nzuri, au kuendesha gari nzuri n.k. unadhani inatokana na nini?!
 
Utajiri ni ile hali ya kumiliki mapesa mengi na kuwa na mali nyingi, utajiri ni mzuri kwa kuwa unakupa uwezo, nguvu, mamlaka, sifa na umaarufu! Kwa kifupi Utajiri ni kitu chema.

Watu wengi hutafuta utajiri kwa njia mbalimbali halali na haramu wao wanachotaka ni utajiri ili waweze kutimiza ndoto zao nyingi.

Sasa kuna wakati mtu hutafuta utajiri kwa njia za mkato hapa nazungumzia kwa njia za ushirikina na uchawi.

Utajiri huu ni mzuri na huja haraka lakini ukiwa na masharti mengi lakini kubwa likiwa ni kutoa kafara la damu kwa kuangamiza roho.

Unapoingia kwenye utajiri huu mwanzoni utafurahia na masharti utayaona mepesi lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo hubadilika na tabu huanzia hapo.

Mwanzoni utaambiwa toa kafara la damu ya kuku baadae itakuja mbuzi, halafu itafuatia ng'ombe na mwishowe itakuja binadamu mmoja na hatimaye kwa makundi.

Hii yote ni kutaka kulinda utajiri wako usiporomoke na ukivunja masharti kila kitu kinaharibika .

Kuna pia masharti ya kujisaidia, kulala, kula, kuvaa na hata matumizi ya vitu mbalimbali. Mwanzoni inakuwa ni rahisi tu kwenda sambamba nayo lakini mbeleni mambo hubadilika hasa pale watu wanapoanza kuhoji hiki au kile.

Wote tunajua jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inavyoteketea kutokana na waganga wa kienyeji kuwaaminisha wateja wao kuwa viungo hivyo vikichanganywa na dawa nyingine huleta utajiri, bahati, nguvu na uwezo! Kuna zaidi ya waganga 300 kwenye mahabusu na Magereza mbalimbali wenye kesi zinazowahusisha na mauaji ya albino.

Jamani utajiri wa masharti ya namna hii haufai na mwishowe huwa na anguko kuu tunashuhudia visa vya kila aina kuhusiana na utajiri wa namna hii lakini kila uchao watu hawakomi kuendelea kuutafuta.

Hakika dunia inaumwa
Pop of the pop salute
 
Pamija
 
Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    54.6 KB · Views: 56

Kama mganga anakaa mahabusu kashindwa kujisaidia mwenyewe nini kikufanye umuamini,wengine wakiugua uenda hospital.
 
watu wengi wameongea lakini bado cjaridhika ..nilidhani kwamba nitapata mtu mmoja ambaye ameshawahi kupata hizo Mali kwanjia hizo akiwa anatoa ushuhuda katk huu uzi ...

okay ngoja niendelee kusubiri
 
Hutopata hata mmoja zaidi watajitokeza waliotapeliwa
 
Back
Top Bottom