Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi


Mimi hii post naiangalia kwa mtazamo hasi kwakuwa mantiki yake ni kutuaminisha kuwa ni kweli utajiri wa ushirikina upo ila una masharti magumu. Katika kipindi hiki ambacho tuna pambana na imani POTOFU kwamba kumuua albino kunaleta utajiri au bahati, si kipindi cha kuwaeleza watu kuwa ukimuua albino utatajirika isipokuwa masharti yatakuwa magumu zaidi baadae.
Imani hizi huitwa POTOFU kwakuwa si kweli kwamba kumuua albino kutakufanya ufanikiwe ktk mipango yako.
Ndugu mshana, huoni kwamba post yako yaweza kuwahamasisha watu kutafuta utajiri kwa masharti yawayo yoyote yale ilhali si kweli.
Ndugu mshana hujagundua kuwa makabila au jamii zinazosifika kwa utajiri , nyingi husifika kwa ubahili pia???
Angalia WACHAGGA, WAKINGA, WAPARE....Makabila haya yanasifika kwa kufanikiwa ktk biashara, lakini pia yanasifika sana kwa Ubahili.

Ningependa kuwafahamisha wana JF ya kwamba, Hakuna kitu kinaitwa Utajiri wa ushirikina wenye masharti magumu, ila ili uwe tajiri lazima uzingatie "MASHARTI YA UJASILIAMALI" ambayo kimsingi ndiyo huitwa masharti ya kishirikina.

Nakuhakikishia ndugu Mwana JF, Fanya kazi kwa bidii, kuwa mbunifu, usiwe arrogant, fanya matumizi yale ya muhimu tu, epuka anasa, hakika utafanikiwa bila hata kuongeza kiungo cha albino au kumuua mtoto wako.
Acha kuua ndugu, acha kuua mtoto, acha kuua ALBINO. zingatia masharti ya Ujasiliamali, na utafanikiwa.
 

Kuamini sana ushirikina kunaenda sambamba na illiteracy level na umasikini.
Siku zote, jamii inayoamini sana ushirikina kwa kiasi kikubwa huwa haijaelimika na pia huwa ni masikini sana. Huo ndio ukweli, fanya observation utaliona hilo.
 

Kuacha kuongea kitu kilichomo kwenye jamii kwa kisingizio kuwa utahamasisha ni kuukimbia ukweli kitu ambacho ni kibaya kuliko tunavyodhani
Lazima kila jambo lijadiliwe kwa mapana yake watakooelimika ni wengi zaidi ya wataotaka kujaribu!
Dawa ni chungu lakini ni tiba
 

Wana mazezeta ndani kama wahindi......
HAPO KWENYE RED SIO KWELI
 
Utajiri upo kama anaetaka pm hakuna kutoa kafara kabsa ila ni kuvumilia miaka minne na majaribu
 
Oh, ok. Wewe uko category gani kati ya hizo ulizotaja? Je nikitaka zaidi ya hizo inabidi nifanyeje?

Mmh hapana mimi si practice bali nimesomea tu hizi mambo ila makafara hufikia mpaka wakati unahitajika kutoa roho zisizopungua 20!refer ajali za March...!!!
 

Nimekupata aisee mangi! Hata sisi wachaga tunasemwa vibaya sababu ya bidii yetu na kujinyima.
 
post nzuri sema watu wapo kwenye mikutano ya kutangazia nia?



Viungo vya albino kwa sasa kuvipata ni kazi sana. Watangaza nia kwa sasa wako bize sana kujinadi na kutoa dau kubwa kwa viungo vya binadamu ili tu washinde urais na kuchukua nchi kwa nguvu zozote zile.
 
Yaani hapa mangi umeua bendi, uliyoyasema ni ya kweli kwani utakuta mtu ni dereva tu tena si wa maana (kuli wa serikali) ila maisha anayoishi na mali anazo miliki tofauti kabisa na kazi yake. Nina ndugu wa namna hii na kwao wanafahamika kwa kuzima nyota za watu na kuruka na ungo.
 
Kuamini sana ushirikina kunaenda sambamba na illiteracy level na umasikini.
Siku zote, jamii inayoamini sana ushirikina kwa kiasi kikubwa huwa haijaelimika na pia huwa ni masikini sana. Huo ndio ukweli, fanya observation utaliona hilo.
hapa si kweli mkuu, maofisini kumejaa uchawi sana. je hawa sio walioelimika? Adebeyo na kuishi ulaya ana amini mama yake anampiga juju,imani za kichawi zipo sana kwetu ngozi nyeusi.
 
Sasa vipi kuhusu Mjomba.Maana yeye peku peku bila viatu.
Juzi alikuwa BBC London na aliingia Studio bila viatu.
Dunia ameivuruga kwa kutembea Nchi mbali mbali peku
Nasikia anamiliki Ghorofa Refu kuliko Yote London.

View attachment 259053
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…