Chaos Master

JF-Expert Member
Jul 7, 2021
636
1,304
‌Utajiri wa baharini:Dhahabu imejaa baharini kwa sababu ya kuzama kwa meli kadhaa za kale

‌Kuna mali ya thamani ya mamilioni ya dola inayoharibika katika bahari mbali mbali duniani . Mali hiyo ni pamoja na maelfu ya tani za dhahabu na vito vya thamani ambavyo vilizama pamoja na meli zilizohusika katika ajali miaka mingi iliyopita .

‌Mataifa,taasisi na watu wamekuwa wakiendeleza juhudi za kusaka baadhi ya mali hizo kwa miaka mingi na kuna waliobahatika kuzipata . Inakisiwa kuwa thamani ya dhahabu iliyozama katika mabahari mbali mbali duniniani inatosha kumaliza umaskini wa takriban nusu ya watu duniani wanaoishi maisha ya ufukara .

‌Iwapo una uwezo wa kuyafikia maeneo haya ya bahari ,huu ndio utajiri wa dhahabu na mali iliyozama katika sehemu hizo na iwapo juhudi zako zitafua dafu -utaingia katika historia kama miongoni mwa waliofanikiwa kunufaika na mali hiyo ya baharini .

‌Lakini sio wote wanaopata mali hiyo ya baharini hukubaliwa kuichukua kwani kuna waliojituma maisha yao yote kuzitafuta dhahabu na vito hivyo kwa miaka mingi bila kufanikiwa.

‌Pauni milioni 100 katika bahari Hindi. ‌Kulingana na ripoti za muda mrefu kuna meli ya maharamia iliyozama katika bara Hindi ikiwa na dhahabu yenye thamani ya Pauni milioni 100 katika mojawapo ya visiwa vya bahari hiyo

‌Ingawaje Bahari hiyo inaaminika kuwa na sehemu nyingi yenye mali ya thamani iliyotapakaa kwa sababu ya ajali nyingi za meli na vyombo vya majini ,meli ya maharamia hao inaaminika kuwa ndio iliyozama na kiasi kikubwa cha dhahabu .Eneo lenyewe ni kati ya visiwa vya Ushelisheli na La Reunion.

‌Ingawa wengi wamejaribu - na wameshindwa - kupata dhahabu hiyo , wanaume wawili wamejitolea maisha yao kwenye harakati za kuisaka. Reginald Herbert Cruise-Wilkins, anayejulikana katika eneo la kisiwa cha Ushelisheli cha Mahé kama 'Msaka dhahabu', aliwinda mali hiyo kwa miaka 27 hadi kifo chake mnamo 1977. Mwanawe John alirithi jina lake la utani na kazi hiyo.

‌John alitoa simulizi ya kupendeza ya mali hiyo kwamba mnamo mwaka wa 1716 wakati Mfaransa Olivier Levasseur, anayejulikana kama "La Buse" (The Buzzard) kwa sababu ya kasi ambayo angewashambulia maadui wake, alipopewa barua ya idhini kufanya kazi baharini. Lakini ndani ya miezi michache, Levasseur aligeukia kazi nzuri zaidi ya uharamia.

‌Mnamo 1721, Levasseur na washirika wake - wakati huo wakiwa na maharamia 750 juu ya meli tatu - walipata meli ya Ureno ikipeperusha bendera ya Uingereza kwa jina Nossa Senhora do Cabo, katika bandari ya La Réunion, wakati huo ikiitwa Kisiwa cha Bourbon. Walitua wanaume 250 kwenye meli hiyo na kuwaua wafanyakazi wote.

‌Levasseur, ambaye hakujua ni nini kilichokuwa kwenye meli hiyo, alishangaa na kilichokuwemo. Kulingana na John, mwanahistoria aliielezea kama 'nyumba ya hazina inayoelea, inayoaminika kuwa na vifurushi vya dhahabu na fedha, mawe ya thamani, almasi ambazo hazijakatwa na vitu vingine vyenye thamani

‌Maharamia walikimbia haraka kwenda makao yao makuu huko Madagascar na Jeshi la Wanamaji la Uingereza lilikuwa likiwafuata kwa kasi.

‌Baadaye waligawana mali hiyo huku kila mmoja akipata almasi 42 na vipande 5,000 vya dhahabu. Levasseur alibaki na mali iliyosalia
‌Maharamia hao kisha walitoweka na inaaminika walificha mali yao katika kisiwa cha Ushelisheli cha Mahé.

‌"Aliwawatawanya wafanyakazi wake katika vikundi vya wanaume 20, baba yangu alifikiria. Wafanyakazi hawakujua wapi chumba cha kuweka dhahabu hiyo kitakuwa. [Hazina] iliwekwa kwenye pango, iliyowekwa kwa muda mfupi, halafu wakati wa mazishi ulipofika, ni wafanyakazi tu wa mazishi ambao walifunga pango na kisha wakauawa, "John alisema. Hakuna mtu isipokuwa Levasseur sasa alijua mahali ilipo.

‌Baadaye Levasseur alitekwa na kuuawa mnamo Julai 7, 1730 huko La Réunion, inaonekana alijua kulikuwa na washirika wake waliokuwa maharamia katika umati. Alitupa kipande cha ngozi hewani, akipiga kelele 'Hazina yangu kwa yule anayeweza kuelewa'.
‌Kipande hicho cha ngozi kilikuwa ramani ya hazina hiyo ‌Dola bilioni 20 katika bahari ya Caribbean

‌Kwa karne nyingi, Meli ya San José ililala chini kwenye sakafu ya bahari, lakini sasa iko katikati ya mzozo wa umiliki, na watu kadhaa wakidai utajiri wake.

‌Ilikuwa mnamo Juni 8, 1708 ambapo meli ya Uhispania San José ililipuka moto kutoka pwani ya Cartagena, Colombia. Meli hiyo ilikuwa ikipigana na Waingereza tangu alasiri, na usiku, meli hiyo ya mizinga 62 ilikuwa imepotea katika Bahari ya Caribbean. Nayo, ilizama ikiwa na karibu watu 600 na dhahabu, fedha na vito vya thamani ya $ 20bn.

‌Kwa karne nyingi, meli ya San José ilipotea kwenye sakafu ya bahari. Lakini siri iliyozunguka meli hiyo ilianza kufichuka mnamo 2015, wakati serikali ya Colombia ilipotangaza kuwa imepatikana rasmi. Miaka minne baadayem,meli hiyo bado iko mita 600 chini katika maji ya Colombia.

‌Serikali ya Colombia haijafichua eneo halisi la meli hiyo Lakini San José inasemekana iko karibu na visiwa vya Rosario, visiwa vya kitropiki na hifadhi ya kitaifa kilomita 40 kutoka Cartagena.

‌Msururu wa boti ndogo hupita juu ya maji wakati zinaposafirisha watalii wanaokwenda pwani kwenda visiwani kila siku. Wakati unabebwa kuvuka bahari, ni vigumu kutofikiria San José na hazina yake, chini nani ya bahari .

‌CHANZO CHA PICHA, LUIZ RIBEIRO/ALAMY‌
‌Meli ya San José iliondoka katika mji wa bandari wa Panama wa Portobelo mwishoni mwa Mei 1708. Ilikuwa imesheheni dhahabu, fedha na mawe ya thamani yaliyotolewa kutoka nchi iliyokuwa ikidhibitiwa na Uhispania,Peru ambayo inakadiriwa kuwa na thamani kati ya $ 10bn na $ 20bn leo.

‌Utajiri huo ulikusudiwa Mfalme Philip V wa Uhispania, ambaye alitegemea rasilimali kutoka kwa makoloni yake kufadhili vita vya urithi wa Uhispania.

‌Nahodha wa meli hiyo, Jose Fernandez de Santillan, alijua kwamba Waingereza, ambao walihusika katika vita, wanaweza kuwa na meli zinazosubiri kuishambulia huko Cartagena; mji huo ulilenga tu kuwa kituo cha haraka cha kukarabati San José kabla ya safari yao ndefu kwenda Havana, Cuba, na kisha kwenda Uhispania. Lakini nahodha aliendelea mbele na safari.

‌Na kufikia jioni ya tarehe 8 Juni, vita vya hazina ya San José vilikuwa vimeanza. Jeshi la Wanamaji la Uingereza - lililokuwa na bastola, panga na visu - lilijaribu mara tatu kupanda boti na kuichukua kama yao, alisema Gonzalo Zuñiga, msimamizi wa Jumba la kumbukumbu la wanamaji la Caribbean huko Cartagena
 
Ngoja nijitoe muhanga sasa nikasake huo utajiri aisee , maana bongo nyoso aisee na hizi tozo balaa tu
 
Unatafuta kitu usichokiweka
Kuna mambo mengine tunaamua kuacha tu
 
Back
Top Bottom