Utahamia lini kijijini?

WAKUU NAOMBA nipewe muongozi wilaya ya mafia huko NDO NAENDA KUWEKA kambi WAKUU. Wenyeji WA hukoo pliz ramani🙏

Kwishaaaaaa
Karibu sana, mi niko karibu na Jibondo, Jibondo iko kusini ya mafia kilometa kidogo tu. Huku ni pwani pacee, amani tele hasa kama utafuata na kufanya kilicho kuleta. Njoo na utafanya biashara zako zote kwa raha zako, hatuna wivu na mtu. Ila usiparamie wake zetu basi, watu ni wakarimu sana.
 
Safi mkuu Bora nmekupata nisaidie mambo yafuataayo.
1. Najihusisha na kuuza MIKOBA ya WADADA. Mabegi ya shule nk JE soko lipo huko.
2. Ardhi bei zake Zina unafuu MANA NAPENDA nikuishi sehemu nijenge.
3. PESA IPO.
4. NAPENDA kujiburudisha weekend JE MAeneO ya Bata mziki nk YAPO? Yamechanganya . MANA kipimo cha WATU kua na HELA sehemu huendana na muamuko WA SEHEM za starehe.
5. Usafiri WA maji ni WA uhakika.

Asante mkuu NMEMPATA RAFIKI WA kudumu

Kwishaaaaaaaaa
 
Naongezea pia
6. Umeme UPO ni WA uhakika
7. Maji
8. Mitandao ya simu inashika VIZURI.
 
Mafia ni makao ya Wilaya, huduma zipo mpaka uwanja wa mbayuwayu upo vizuri sana, ni 24/7 unatoa huduma. Kuna baadhi ya Hotel wewe huwezi kuingia labda baada ya miaka mia ijayo. Watu wa huku ni Muslims na wanafanya Ibada sana, so starehe zisizo na mipaka huku hakuna. Siyo unapiga maji halafu ukakae upenuni kwa shehe. Kwa utalii ndo kwenyewe, mzunguko wa pesa upo sana ktk biashara za mahitaji ya nyumbani. Viwanja vipo, maji na umeme upo.
 
Inamanisha wazungu WAPO WA kutosha huko JE ni kwa season TU au SIKU zote. NIKIWA na LAKI Tano kiwanja naweza PATA hata shambaa huko? Punda mnyama huko WAPO? maana nakazi NAO. Asante mkuu 🙏 🙏
 
Naongezea pia
6. Umeme UPO ni WA uhakika
7. Maji
8. Mitandao ya simu inashika VIZURI.
Biashara za mahitaji ya watoto, vijana na wanawake ziko poa sana. Biashara za mazao ya bahari ipo (samaki, majongoo bahari, mwani, pweza, nk). Vitu vya urembo vinalipa sana huku visiwani.
 
NItahamia mpka kitambaa ifungwe 😅😅😅
 
Inamanisha wazungu WAPO WA kutosha huko JE ni kwa season TU au SIKU zote. NIKIWA na LAKI Tano kiwanja naweza PATA hata shambaa huko? Punda mnyama huko WAPO? maana nakazi NAO. Asante mkuu 🙏 🙏
Wazungu wapo, kuna kipindi wanakuwa wengi sana, Punda hawapo, ila ng`ombe/mbuzi/kondoo wapo. Waarabu wapo pia.
 
Biashara za mahitaji ya watoto, vijana na wanawake ziko poa sana. Biashara za mazao ya bahari ipo (samaki, majongoo bahari, mwani, pweza, nk). Vitu vya urembo vinalipa sana huku visiwani.
SAWA KAKA NMEULIZA KUHUSU VIWANJA bei zake JE NIKIWA na LAKI Tano naweza PATA? Wanyama punda huwa nawatumia KWENYE usafirishaji mali za WATU JE WAPO?
 
SAWA KAKA NMEULIZA KUHUSU VIWANJA bei zake JE NIKIWA na LAKI Tano naweza PATA? Wanyama punda huwa nawatumia KWENYE usafirishaji mali za WATU JE WAPO?
Punda huku hawapo sbb mizigo haipo. Viwanja mpaka wenyeji wakukatie, siyo biashara kama Mkuranga. Kumbuka eneo siyo kubwa kama bara. Ila vipo. Nitauliza.
 
Ohooo ...maji yamelowana huku....
 
Samahani nikisafirisha punda WAWILI kuwaleta huko kwa AJILI ya kubeba mizigo kama mchanga TU vitu kiasi Ina RUKSA au hawaruhusu

Kwishaaaaaaaa
 
Hapa cyo meru kweli make kibarabara cha nkoranga ndo upana huo wa rula😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…