Utahamia lini kijijini?

Mkuu Equation x , hongera, kama haya umeandika ni kweli , lakini TO ME ,this life is real. NIMERUDI NYUMBANI.
BAada ya kumalizana na masuala ya talaka na ndoa kuvunjika, nikaamua kuacha kila kitu na kuamua kurudi mkoani (nyanda za juu kusini).
Hapa ndipo nimezaliwa na kusoma toka chekechea mpaka nahitimu high school Tosa boys miaka 15 iliopita.
Sikutaka kukaa mjini kati, nikasogea pembezoni kabisa mwa mji huko mashambani.
I live a very peaceful life considering the fact kwamba umeme upo, maji ya mamlaka ya maji mkoa pia yapo ya kotosha.

Nilichokifanya ni

  • ku establish my local gym, kwakua ninapenda weight lifting.
  • nimefungua mradi wa kufuga nguruwe, nilianza na nguruwe 7, huu bado naukuza haujaanza ku pay out
  • nikafungua pia mradi wa ufugaji kuku chotara na wa kienyeji. Nina average ya kuku 400 ambao hawapungui mabandani all the time maana hawa tayari nilishaanza kuwauza na for every 3 weeks sikosi kuuza kuku wa wastani wa shilling 800,000/.

Sio mashamba yangu bali ni maeneo ya wazee wangu, ambayo niliona wanayatumia kwa kiasi kidogo sana, nikaona acha niyatumie ipasavyo.

By proffesion, mimi mi software developer na "software As Service" ndio biashara yangu so i continue coding during night to support my clients technically. So am getting paid while being right here , regardless nimelala or what!!

KIukwel ,maisha haya so far yananipa utulivu sana ,niii tafakari my come back (japo najiona kabisa siwezi tena rudi jijini).

I take few trips kusafiri pale ambapo nahitaji kuonana na clients wangu mikoani na jijini lakin most of the time napatikana shambani kijijini, huku ndiko maisha yangu yame base kwasasa..

Napata muda wa kutosha kulala sanaaaa.
Kufanya mazoezi sana pia.
 
Umefaulu sana kuwafanya watu wajadili ubuyu wako wasahau kidogo mipasho ya kula tunda kimasihara
Ardhi huku kijijini bei rahisi sana, kuna sehemu unaweza kupata ata kwa 80,000 tu; kwa mtu yeyote at mwenye kipato cha chini akiwa na maleno ya muda mrefu, ndani ya miaka 5 atakula mema ya dunia.​
 
Hakuna uhalisi. Uhalisi gani wa kufuga mbuzi, nguruwe, kuku, ng'ombe idadi yote hiyo kwa ajili ya kitoweo, mayai na maziwa kwa mke na mume?
Inawezekana, wakipatikana wanunuzi unauza.
 
Mkuu haya ndo maisha, town unaenda kutembea tembea tu unarudi kambini.


Safi mkuu
 
  • Hongera sana, na pole kwa changamoto ulizopitia.​
  • Kama bado utakuwa na salio, boresha eneo lako kwa kuchimba kisima kirefu, au kama bili haikusumbui unaweza kutumia maji ya idara, na pandisha minara miwili ya lita 10 juu, fanya kilimo cha umwagiliaji wa bustani, nkimaanisha mazingira yako miaka yote yawe kijani.​
  • Jenga/tenga ofisi ndogo hapo nyumbani kwa ajili ya kazi yako.​
  • Fungua chaneli ya Youtube, onyesha shughuli unazofanya.​
  • Baada ya miaka 2 tupe mrejesho pamoja na mke mgeni/mzungu utakayempata.​
  • Utakuwa ni milionea kama sio bilionea 'in town'​
  • Na aliyekukimbia, atakutafuta kwa kila namna ingawa haitasaidia atakuwa amechelewa.​
 
Nipo kijijini.
Nso mana nawaanua wana kuwa idadi ya wanyama na man power ulonayo ni tembo na sisimizi.

Ko hilo wazo lako ni ngumu hata kuwa ndoto.
Ngoja nikamate mbuzi nichome
 
Hapo sio Tanzania ni UK au South Africa,sasa story yako ipange upya
 
Ahahahaha.. kuhusu You tube channel, ninkama ulikua kwenye mawazo yangu. I was about to do that ila katika masuala mengine. I am about to start kilimo cha bustan ,ninafanya kama pilot phase so far kwa matumizi ya nyumban tu kwakua niko na vijana kadhaa hapa maeneo so tunakula mboga mboga za shambani ukiachana na kutumia vyuku kama kitoweo 😂
 
Huyu anafurahisha genge.
Kupambana na Hao wanyama ni shughuli pevu.
Hata hizo sauti za ndege anazosema, ingekuwa nadra sana kweke kuzisikia....mziki wake wa kila siku ungekuwa ni sauti za kitimoto.
 
Ni vizuri, maisha ni kuishi namna wewe unavyotaka, na katika kulifanikisha hilo ni lazima kujiwekea misingi pamoja na kuitekeleza.​
 
Huyu anafurahisha genge.
Kupambana na Hao wanyama ni shughuli pevu.
Hata hizo sauti za ndege anazosema, ingekuwa nadra sana kweke kuzisikia....mziki wake wa kila siku ungekuwa ni sauti za kitimoto.
Mkuu, karibu huku shambani nipo hapa nanyonyoa kuku niweze kula nyama choma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…