Elections 2010 Utafiti wa TCIB: Dk. Slaa aongoza

MO-BLOG.jpg

Kutoka kushoto ni Mhadhini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Uchumi Dr.Vicent Leyaro akizungumza na waandishi wa habari katika Hotel ya Courtyard juu ya utafiti wa (TCIB) akiwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa (TCIB) Bw. Steven Msechu.

Na Mwandishi wetu

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutoa utafiti wa taarifa mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha wananchi maamuzi kwa uelewa la Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB) limetoa taarifa ya matokeo ya utafiti wa kura ya maoni kuhusu wagombea urais 2010.

Akizungumza na waadishi wa habari Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam idara ya Uchumi Dr. Vicent Leyaro amesma malengo ya TCIB ni kutoa msukumo kwa wananchi kushiriki katika harakati za kulinda na kendeleza misingi ya Demokrasia, Kutoa fursa kwa wananchi katika kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali katika maisha na kujenga uwezo wa wananchi kwa njia ya tafiti na elimu katika nyanja za serikali, siasa, Mambo ya Kimataifa, ulinzi, elimu na maadili.

Aidha Dr. Vicent Leyaro amesema washiriki katika kura hii ya maoni ni 3047 wenye wasifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto chini ya darasa la saba, elimu ya sekondari na elimu iliyo juu ya sekondari ambapo katika utafiti huo silimia kubwa ya vijana wamonekana kuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA Wllbrod Slaa na asilimia kubwa ya wazee wameonyesha kumuunga mkono mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete.

Amesema Dr. Willbod Slaa ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro 71%, Arusha 60.4%, Manyara79.8%, Iringa58.2% na Dar es salaam 42% ambapo Jakaya Kikwete ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa Dodoma 59.3%, Morogoro 56%, Mbeya50%, Rukwa 54.3% na Ruvuma 55%.

Akihitimisha wakati akijibu maswali kwaa waandishi wa habari Dr. Vicent Reyaro amesema utafiti haukuangalia wala kupendelea sehemu ambazo mtu anapendwa sana kuliko sehemu nyingine na uchambuzi wa matokea kimkoa yanaonyesha kuwa wagombea wawili Jakaya Kikwete na Dr. Willbrod Slaa wanachuana vikali baadhi ya mikoa na mikoa mingine kufanya vibaya.

Hata hivyo utafiti huu wa kura ya maoni kuhusu wagombea urais hauukufanyika kwa upande wa Zanzibar japokuwa wananchi wa Zanzibar wanashiriki katika kupiga kura ya kuchagua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Chanzo:
Changamoto

hapo kwenye red kuna tatizo. ni vyema utafiti ufanywe kwa wale watakaopiga kura na si kuchanganya na watoto wa shule za msingi

na inaonekana hiyo sio random sampling
 
Safi sana kwa kufanya utafiti,tunahitaji tafiti nyingi sana kabla uchaguzi,ili tujue ukweli uko wapi!
 
Now you are talking!!! Katika tafiti zote zilizofanyika huu ndio haujachakachuliwa, kama Slaa au JK atashinda basi itakuwa ni kwa asilimia ndogo (45%-49%) siyo zaidi ya hapo. Nasema hivyo kwa sababu kuna wakulima huko usukumani hawasikii wala kuambiwa kuhusu JK, wananiboa mpaka siku hizi niamua kuwaignore
 
Note, idadi yote ya wapigakura wa Zanzibar, Lindi, Pwani na Mtwara ukijumlisha ni karibu sawa na wapigakura waliopo DSM, hii ina maana kwamba hata kama JK ataongoza katika mikoa hiyo lakini Dr wa Ukweli anapiga bao kwenye mikoa yenye watu wengi kama Shinyanga, Mwanza, Manyara/Arusha, Mara, Knjaro, kigoma, Iringa, Mbeya ambako JK kaongoza kwa Margin Ndogo nadhani walikwenda Rungwe lakini kama wangeenda Mbalali, mbey Mjini/Vijijini, Chunya, Tunduma au Kyela wangeula wa Chuya

Hata Jana kwenye Nyelele Day pale Karimjee kama ungeenda ungekutana na makatibu wa UVCCM DSM badala ya Wanavyuo, kama ni kuchacha sasa CCM inanuka imeanza kuoza kabsaaaaaa
DR Slaa for Change
 
Matokeo wameyatoa leo?
Kwa vyombo vya habari uu ndo tungoje usiku kwa news manake iyo nayo yaitaji publcity.Angalau samle ni ya zaidi ya watu 3000
 
hapo kwenye red kuna tatizo. ni vyema utafiti ufanywe kwa wale watakaopiga kura na si kuchanganya na watoto wa shule za msingi

na inaonekana hiyo sio random sampling

Yaap hasa ukizingatia kuwa wasiopiga kura mwaka huu ndio wanaomuunga mkono JK.
 
hapo kwenye red kuna tatizo. ni vyema utafiti ufanywe kwa wale watakaopiga kura na si kuchanganya na watoto wa shule za msingi

na inaonekana hiyo sio random sampling

Haya kama maneno ya waandishi wa habari - si mnawajua tena. Yani daktari mzima wa falsafa akamhoji mtoto wa chini ya darasa la saba?
 
Ni dhahiri utafiti uliokuwa haufungamani na upande wowote wa chuo kikuaa cha DSM umesema k weli

some hapa
fullshangwe.blogspot.com/.../tcib-yasema-dr-jakaya-kikwete-na-dr.html

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutoa utafiti wa taarifa mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha wananchi maamuzi kwa uelewa la Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB) limetoa taarifa ya matokeo ya utafiti wa kura ya maoni kuhusu wagombea urais 2010.

Akizungumza na waadishi wa habari Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam idara ya Uchumi DR. Vicent Leyaro amesma malengo ya TCIB ni kutoa msukumo kwa wananchi kushiriki katika harakati za kulinda na kendeleza misingi ya Demokrasia, Kutoa fursa kwa wananchi katika kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali katika maisha na kujenga uwezo wa wananchi kwa njia ya tafiti na elimu katika nyanja za serikali, siasa, Mambo ya Kimataifa, ulinzi, elimu na maadili.

Aidha Dr. Vicent Leyaro amesema washiriki katika kura hii ya maoni ni 3047 wenye wasifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto chini ya darasa la saba, elimu ya sekondari na elimu iliyo juu ya sekondari ambapo katika utafiti huo silimia kubwa ya vijana wamonekana kuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA Wllbrod Slaa na asilimia kubwa ya wazee wameonyesha kumuunga mkono mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete.

Amesema Dr. Willbod Slaa ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro 71%, Arusha 60.4%, Manyara79.8%, Iringa58.2% na Dar es salaam 42% ambapo Jakaya Kikwete ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa Dodoma 59.3%, Morogoro 56%, Mbeya50%, Rukwa54.3% na Ruvuma 55%.

Akihitimisha wakati akijibu maswali kwaa waandishi wa habari Dr. Vicent Reyaro amesema utafiti haukuangalia wala kupendelea sehemu ambazo mtu anapendwa sana kuliko sehemu nyingine na uchambuzi wa matokea kimkoa yanaonyesha kuwa wagombea wawili Jakaya Kikwete na Dr. Willbrod Slaa wanachuana vikali baadhi ya mikoa na mikoa mingine kufanya vibaya.

Hata hivyo utafiti huu wa kura ya maoni kuhusu wagombea urais hauukufanyika kwa upande wa Zanzibar japokuwa wananchi wa Zanziar wanashiriki katika kupiga kura ya kuchagua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Changamoto)

Ngoma inogile
 
REDET na SYNOVATE walishaamua kutofanya tafiti this tyme ili wasimuangushe jamaa yao. lakini nahisi waliposikia kuwa TCIB wanafanya tafiti. basi jamaa wakakurupuka na kuanza kuembaras umma kwa tafiti yao isiyofanyika na kumbe TCIB wamekuja na majibu ya hali halisi.

Sasa tuwasubiri akina rwekaza wakiikandia ripoti hii ya TCIB maana yao ilikandwa na wasomi kama wao.

Jamaa wa TCIB wametumia vigezo murua ktk kutafiti na kuwakilisha.
 
Ninachofahamu utafiti unapingwa kwa kufanya utafiti. Sipingi huu utafiti ila nimeshindwa kuelewa kwa nini awashirikishe watoto wa chini ya darasa la saba? Hawa tunajua hawaruhusiwi kupiga kura na bado ni watoto. Naomba mwenye ufahamu atueleze yasije kuwa yale yale....
 
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Tanzania Citizen's Information Bureau (TCIB) na kutolewa leo umeonyesha Dk Slaa anaongoza kwa asilimia 45, JK asilimia 41,Prof. Lipumba asilimia 10, Hashim Rungwe 2, Peter Mziray 1 na Mutamwega 1.

Utafiti huu umefanyika kwenye mikoa 15 iliyochaguliwa kwa njia ya kinasibu (random sampling ) na kwenye jimbo moja katika kila mkoa wananchi kati ya 60 na 100 walihojiwa. Utafiti umefanywa ndani ya mwezi huu na kutolewa leo Jijini Dar es Salaam.

Kwenye Gazeti la mwananchi pia wanayo online polls, na mpaka sasa Dr. anaongoza kwa zaidi ya 70%.
 
Huo ni utafiti usiokubalika kwa jamii. Yaani jamani mtu anajiita Dokta lakini mambo yanayofanyika ni tofauti kabisa na elimu yake. Utawezaje kufanyia utafiti watu 3000 kuwakilisha milioni 16 watakaopiga kura.
Eti watoto wa shule ya msingi nao unawajuisha utafikiri ni wapiga kura. Hivi hawa madaktari wa chuo kikuu wana matatizo gani?

I don't care hata kama Slaa anaongoza but this utafiti is full of Banalism too. Kwenye ukweli lazima tuusimamie, hapa huyu Dr. Leyaro naye katokota.
 
Kuwahoji watoto wa shule si kosa katika tafiti kuna kundi la watu ambalo unaweza kulihoji ili kukupa jawabu linganifu katika utafiti mzima unaofanya kwa mfano ukitaka kutafiti maswala fulani kwa wafanyakazi wa kada fulani katika jambo fulani unaweza ukawahoji watoto kwa sababu wananufaika na kile wafanyakazi wanachokipata kama ulinganifu katika jamii ni njia moja wapo tuu ya kupata maoni mengi zaidi katika makundi mbalimbali ya kijamii,watafiti wanayafahamu haya
 
Huo ni utafiti usiokubalika kwa jamii. Yaani jamani mtu anajiita Dokta lakini mambo yanayofanyika ni tofauti kabisa na elimu yake. Utawezaje kufanyia utafiti watu 3000 kuwakilisha milioni 16 watakaopiga kura.
Eti watoto wa shule ya msingi nao unawajuisha utafikiri ni wapiga kura. Hivi hawa madaktari wa chuo kikuu wana matatizo gani?

I don't care hata kama Slaa anaongoza but this utafiti is full of Banalism too. Kwenye ukweli lazima tuusimamie, hapa huyu Dr. Leyaro naye katokota.

Hiii ina tofauti gani na watu wazima wasiojiandikisha?????????????? All in all tafiti zote zina mapungufu lakini mimi nafurahia zinapozidi kuwa nyingi na tofauti zinaondoa ile Psychological effect na kuacaha watz kufanya maamuzi bila interference ya propaganda!!!!!!
 
Dr Slaa anastahili apate 60-70% Jk 10% etc labda sampling ilikuwa ndogo

Udogo wa sampple size hau-affect percentage. Tuliona jamvini humu kura zilizopigwa Kagera kijijini kwenye msiba ambapo Dr Slaa alipata kura 48/60 (80%). To me, the results reported poll in this thread sounds very realistic
 
Back
Top Bottom