jd41
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,756
- 4,849
...huu uzi umenikumbusha siku moja niko barabarani natembea,ilikuwa kama saa 8 mchana hivi,nikapishana na kakikundi cha watoto wa kike wametoka shule (ya msingi), kwa kifupi stori walizokuwa wanapiga wale watoto ni kwamba mmoja anaishi kwenye nyumba ya kupanga,sasa kuna tobo analolitumia kuwachungulia watu wazima wakiwa wanaoga...maneno aliyoongea yule binti,mtu mzima ilibidi niwapite kwanza halafu nikageuka kuwatazama tena,nikafikiria umri wao,na yale waliyokuwa wanayazungumza,nikapata jibu kumbe hamna mtoto mjini,wote watu wazima.!!