Utafiti: Shule za msingi zakithiri kwa ngono

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,693
1,701
Wanajamii

katika pitapita yangu nimekutana na hii taarifa ya utafiti:

Source: UTAFITI: Wanafunzi shule za msingi wakithiri kwa ngono


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UTAFITI uliofanywa na mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono, umebainisha elimu ya afya ya uzazi bado inahitajika ili kuwakinga na tabia hatarishi.

Akitoa matokeo ya awali ya utafiti huo, mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili, kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula, alisema kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 14 ambao ni wanafunzi wa darasa la tano na sita wameshawahi kufanya ngono.

Alisema ngono hiyo kwa asilimia kubwa hufanywa na wanafunzi hao kinyume na maumbile.

Kajula alisema vijana wengi wamebainika kufanya ngono ya kawaida na ya mdomo, ikifuatiwa na ngono ya kinyume na maumbile.

Alisema kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono, asilimia 6.3 wamefanya kinyume na maumbile wakati asilimia 93.7 hawajawahi kufanya.

Alisema utumiaji wa kondomu umebainika kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao wameanza kufanya ngono.

“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawahi kutumia kondomu kabisa, wakati asilimia 32 wamewahi kutumia,” alisema.

Alisema hiyo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini, Bergen na Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha Uingereza.

Katika utekelezaji wa utafiti huo, wanafunzi 5,099 walichaguliwa mwanzoni mwa mradi kufanyiwa utafiti huo, ambapo 4,783 (asilimia 93.9) walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4,370 (asilimia 85.8) kwa miezi 12.

Mradi huo wa PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka Manispaa ya Kinondoni zilizochaguliwa, kwa kutumia sampuli mtawanyiko, zilizopangwa katika makundi mawili ya shule.

“Kimsingi tunataka kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya mradi wa PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa kiume na wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Kajula.

Matokeo yaliyotathminiwa ni mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono) na kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwishaanza vitendo hivyo.

Kajula alisema kwa wastani mradi wa PREPARE umefanikiwa kupunguza uwezekano wa vijana wadogo hasa wavulana na wasichana kuanza ngono na kuongeza matumizi ya kondomu kwa wale walioanza.

Hata hivyo, katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa hatua yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio ukilinganisha na wale ambao hawakupata.

Alisema uchukuaji wa hatua ulisababisha kuwapo tabia ya kutumia kondomu kwa wanafunzi wa jinsia zote na taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu miongoni mwa vijana wa kiume.

Kajula alisema ili kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa, mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watano wakufunzi wa wakufunzi.

Alisema mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji 76, na waelimishaji rika wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa afya katika kliniki za huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza mwingiliano.

Mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, ambapo programu ya utafiti wa afya imelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya utamaduni na jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya uzazi miongoni mwa vijana wenye umri miaka 12-14 kwa kutumia shule kama njia ya kufundishia.

Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo, alisema utafiti umeonyesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa mfumo wa kisaikolojia kama njia ya kufanya wajitambue.


Huko marekani nako je?

Source: American Teens' Sexual and Reproductive Health



SEXUAL ACTIVITY

  • Miaka 12: 2% Wamefanya ngono
  • Miaka 15: 16% Wamefanya Ngono
  • Miaka 16: 33% Wamefanya Ngono
  • Miaka 17: 48% Wamefanya Ngono
  • Miaka 18: 61% Wamefanya Ngono
  • Miaka 19: 71% Wamefanya Ngono
Je nini nini sababu zinazochochea hali hii? Na nini kifanyike ili vijana waache ngono za umri mdogo?
 
Inasikitisha sana..Utadai mtoto anaaribika shuleni au huko nje kumbe wala! ni houseboy ndio anakuaribia mtoto

Watumishi wa ndani uwezekano ni mkubwa sana kwani kuna wazazi wote wawili ni wafanyakazi hivyo muda mwingi huyu mtumishi hubaki na watoto wakisharudi shuleni. Wengine na ambao ni wabaya sana ni watu wazima wanaodai mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzako. Hela za kuwashawishi kwa chips na simu wanazo.
 
Inasikitisha sana..Utadai mtoto anaaribika shuleni au huko nje kumbe wala! ni houseboy ndio anakuaribia mtoto

Thats true. Kwa hiyo nyumbani hakuna nafuu na shuleni nako Shida.
Nini unafikiri kinachangia hali hii?
 
Watumishi wa ndani uwezekano ni mkubwa sana kwani kuna wazazi wote wawili ni wafanyakazi hivyo muda mwingi huyu mtumishi hubaki na watoto wakisharudi shuleni. Wengine na ambao ni wabaya sana ni watu wazima wanaodai mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzako. Hela za kuwashawishi kwa chips na simu wanazo.
Daaah yaani inasikitisha sana.

Nina mpwa wangu anafanya field ya sheria katika moja ya mahakama. Sasa kuna mtu mzima yuko kwenye 40+ years alimlawiti binti wakati huo akiwa ana miaka 7 sasa ana miaka 14. Kwanza kesi imechukua muda mrefu, jamaa anaambiwa jitetee anasema anaonewa tu, lakini vipimo vyote na DNS vinaonyesha ni yeye.

The big question ni: Nini hasa kinasababisha hali hii na nini kifanyike kuzuia au kupunguza? Tafiti inaonyesha hali hii ni mbaya. I wonder kama kuna idara maalumu Serikalini inashughulika na hili.
 
huko ndiko bikra zilipo pekee

Ni vijana wadogo sana. Under 14. Sasa Umri huo hata hiyo Bikra si ni majangazi tu.

Hebu pitia hii statement uone pia hatari ya Ukimwi:

“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawahi kutumia kondomu kabisa, wakati asilimia 32 wamewahi kutumia,” alisema.
 
Hapa Wazazi wanachukua nafasi kubwa.
Ingawa sample yao wanachukua maeneo yale ambayo kilio cha matendo hayo kimekuwa cha Muda mrefu lakini kwa utafiti wangu nilio ufanya baada ya kukutana na kesi kadhaa usiwi wa jamii inaonekana nyumba za kupanga zimekuwa kichochezi kikubwa sana katika hilo especially maeneo ya Magomeni na Mwananyamala
 
Wanajamii

SEXUAL ACTIVITY

  • Miaka 18: 61% Wamefanya Ngono
  • Miaka 19: 71% Wamefanya Ngono
Je nini nini sababu zinazochochea hali hii? Na nini kifanyike ili vijana waache ngono za umri mdogo?
Majanga!
 
Utndawazi umechangia bongo movie pia haikwepi hapa hata sisi wakubwa zao tumechangia pia
Utakuta mtu na mpenzi wake kwa shobo tu anambusu mtu mbele ya watoto na watoto ni wadadisi sana wanapenda kujaribu.

Nyumba za kupanga hapa mjini ni majanga, baba ana watoto wawiliwakike na wakiume miaka 6/ 9 wanalala chumba kimoja kilichokatwa kwa pazia la kanga.

Kila kitu watoto wanashuhudia na wanajaribu pia.
 
Back
Top Bottom