Jifunze kusimama na mkeo ndoa yako idumu

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
"Hakuna ndugu na rafiki wa karibu kama mkeo kama utaishi nae vizuri ndio maana wanasema mume na mke ni mwili mmoja kwa maana hii mkeo ni zaidi ya ndugu yako mkiheshimiana mkapendana na kukubaliana katika mapungufu yenu ndoa yenu itadumu kwa furaha".

Anasema Onesmo Emmanuel mtumiaji wa mtandao wa Facebook akieleza namna mke anavyoweza kuwa rafiki bora kwa mume wake iwapo mume ataishi nae vizuri na kuelewa mapungufu yake.

Emmanuel anahusianisha kauli yake na dhana ya ndoa kutoka kwenye kitabu cha biblia inayotambua wana ndoa kuwa mwili mmoja.

Hata hivyo kwenye jamii kuna mambo mengi ambayo wanandoa wanayapitia ambayo muda mwingine hupelekea talaka kutokea.

Wanaume ndio hunyoshewa vidole mara nyingi pale inapotokea ndoa kuvunjika na hutajwa kuwa wao ndio chanzo.

Zipo sababu mbalimbali za wanaume kuhusishwa kuwa chanzo cha ndoa kuvunjika. Miongoni mwa sababu hizo ni mwanaume kushinda kusimama na mke wake katika mambo mbalimbali yanayotokea iwe ndani au nje ya ndoa yake.

Kitendo cha mume kujitenga na mke wake ndicho huzua migogoro na kupelekea ndoa kuvunjika.

Kitendo cha mwanaume kutomsikiliza mke wake na kuwasikiliza zaidi ndugu zake kama dada zake kuhusu mambo ya ndani ya ndoa yake ni kitendo umiza katika ndoa nyingi.

Mke anahitaji mume ambaye anaeweza kumsikiliza na kumuelewa kwanza kabla hajatoka nje ya nyumba na kuwashirikisha wengine.

Iwapo mke atakosa msaada wa mume katika matatizo yake ni rahisi kutoka kwenda kutafuta mwanaume mwingine anayeweza kumsikiliza.

Pia mwanaume unapaswa kufahamu kuwa mkeo ndiye mtu wako wa karibu hivyo kumhukumu kwa sababu ya maneno mabaya ya ndugu zako dhidi yake pasipo kufikiria uhalisia kutamfanya yeye kuhisi kuwa amesalitiwa na kuingiliwa.

"Mkeo anajitolea maisha yake kwa ajili yako kwa kukuzalia watoto na kuendeleza kizazi chako, mkeo ni wewe na wewe ni mkeo hivyo unapaswa kusimama nae kila wakati" anasema Slamah Hamad mtumiaji wa mtandao wa Jamii Forams nchini Tanzania.

Ni wazi kuwa ndugu zako wanaweza kukushawishi uoe na haohao baadae wakaanza kumsema vibaya mke wako ili uachane nae pasipo sababu ya msingi.

Sio hivyo tu dada zako hawatopenda mke wako akutese lakini haohoa pia hawapendi dada yao akiolewa mahali kwingine ateswe na mume wake.

Hivyo unapata picha kuwa ndugu zako ni watu hatari kwenye uhai wa ndoa yako ukishindwa kuchuja maneno yao na ukashindwa kusimama na mke wako basi ndoa yako ipo hatarini kuvinjika.

Ndoa zinazodumu sio kwamba hazina wake wenye mikopo ya riba kubwa kwenye vikoba kausha damu, hapana ila wanaume walio kwenye ndoa hizo wanavumilia na kuwashauri wake zao juu ya matumizi sahihi ya mikopo hiyo sio kuwapa talaka.

Na ukae ukijua mwanamke ni kiumbe anaependa kudekezwa kusikilizwa hata kama anakuambia maneno ya umbea msikilize usimpuuze ila weka chujio kwenye sikio yako naye atafurahi.

Sio kwamba ukubali mkeo akupande kichwani, la hasha baki na misimamo yako itakayo kutambulisha wewe kuwa kichwa cha familia.

Kujifanya nunda kila siku hakuleti heshima kwenye ndoa mfanye mkeo ajisikie kama malkia kwenye kasri la mfalme.

Peter Mwaihola

Photo Courtesy
Photo_1694011069012.jpg
 
View attachment 2741196
Waliooa wakizingatia biblia isemavyo kwa mfano

1 Pet 3:7 "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili" msisitizo kaeni na wake zenu kwa akili na walioolewa wakizingatia
na
Wakolosai 3:18-19 Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana msisitizo watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana na tena msisitzo mkubwa kwenye maneno kama apendavyo bwana, bwana ni nani hapa si ni Mungu/Yesu!

Maneno haya (na maneno mengine ya Mungu as per biblia) yakizingatiwa na wanando basi hakika uwezekano wa ndoa kudumu ni mkubwa sanaaaa. Kinyume cha hayo ndoa hata kama itadumu basi ni ile ambayo ndani haina amani na furaha ipo ipo tu kwa kuwa tayari kuna watoto, na kuivunja ni aibu au pengine kwa sababu za kiuchumi wanandoa wanaona basi na waendelee tu kuishi pamoja.

Kwa kifupi ni heri ukose ndoa nzuri, uende paradiso/mbinguni baada ya kufa/ au unyakuo kuliko kumridhisha mume/mke mtu/watu/jamii then moto wa jehanamu ukakuhusu. Usicompromise neno la Mungu eti unalinda ndoa/unamfurahisha mume/mke/ndugu/jamii.

Adam na Hawa walikuwa wenyewe Eden walikuwa na dunia nzuri sana isiyokuwa na baya lolote. Hakukuwa na ndugu wa mke wala mume! hakukuwa na magonjwa, wala shida yoyote ile ya kiuchumi, walikuwa na Mungu karibu sana. Still wote wakaharibu uhusiano wao na Mungu kwa kumsikiliza shetani na Mungu hakutoa msamaha the rest is history ndo tujue hii neema ya wokovu tuliyo nayo sasa tusiichezee kisa ndoa!

sorry Peter Mwaihola kwa kuongezea mengine nje ya uzi wako ni siku za mwisho hizi tuwe makini tupende sana ndoa/wanandoa wenzetu but tuwe makini kama shetan alimvuruga eva na adam wakakosa kuendelea kuishi eden na kama mkewe Lutu alipotazama nyuma, akawa nguzo ya chumvi basi na na tujuwe Mungu hajabadilika tusichezee neema ya wokovu kisa ndoa, Adam alikuwa na ndoa na alifungishwa na Mungu mwenyewe! na mkewe Lutu alikuwa kwenye ndo lakini wote waliadhibiwa walipoacha kutii neno la Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom