waBasila
Senior Member
- Jun 27, 2013
- 168
- 37
ukinijibu maswali yafuatayo, ndipo utajua tatizo ni nini.Hivi kuna grade tofauti za ufaulu kati ya wanafunzi wa dini A na dini B? JE tunapoomba kazi, kuna maswali tofauti ya interview yanayoulizwa kitaaluma kwa kuzingatia dini ya mtu?Je kuna katiba ama sheria yoyote,ama sera yoyote ya serikali imeainisha ukuu wa dini yoyote inchini?je ni sahihi serikali ivipuuze vigezo vya kitaaluma katika kupata ajira na ianzishe uajili kwa kuangalia dini ya mtu?je nisahihi tujiulize top two za nyadhifa nchini zimeshikwa na watu wa thehebu gani?je ni sahihi walioko katika top two hizo,wangepingwa na vyama vyao kwakua sio wadhehebu B?vyuoni kuna SAP ama DISCO za kiislam na za kikristo?Ama ninyi bodi ya mikopo mnazingatia dini katika kuendesha shughuri zenu ili dini fulani ikome ubishi? jamani,jamani,watanzania kwanini twajitia upofu wa misingi ya haki iliyo wazi nchini,na kuanza kukomaa na hoja za uchochezi? tukijibu hayo maaswali yote niliyoainisha nidhahiri kuwa si mkristo ama muislamu au mpagani anahaki zaidi ya mwenzake katika fursa za nchi na hakuna serikali kichaa imeyowahi kuwa madarakani na kuruhusu upuuzi kama huo.Watanzania tusiruhusu watafuta maslahi binafsi kupitia migongo ya utetezi wa dini, watuvishe miwani ya mbao tukajikuta tunakokotwa nao, nakusahau kuulinda mustakabali wa inchi, Serikali na udugu wetu imara.MUNGU IBARIKI TZ