Utachagua kipi kati ya mume/mke na pesa?

Utachagua kipi kati ya mume/mke na pesa?

Hapo lazima nichague pesa mkuu. Kwani wanawake noma siku hizi. Labda kama umeongelea wa zamani! Uhangaike utafute, zote zichukuliwe kesho akwambie bila hela, no love! Utakuwa mgeni wa nani? Pesa kwanza
 
Mume wangu ndo furaha yangu ,cwezi chagua pesa nkamuacha Mume wangu.
Wabebe kila kitu ila waniachie tu Mume wangu ,
 
Shikamooni wakubwa wadogo marahaba na wa rika langu mambo zenu habari zenu mwajionaje na hali

Haya leo naombeni tulijadili hili wote wanawake kwa wanaume,leo hii ukiambiwa uchague kati ya pesa na mume/mke utachagua nini.Nitatoa scenario kadhaa ili tuone application ya hili.

1. Mmevamiwa na majambazi yakakupa choice waue mke/mume ubaki na pesa au pesa zote zichukuliwe ubaki na mumeo mkeo unachagua nini?

2. Una mali nyingi lakini ghafla unayumba kiuchumi mtu fulani mwenye pesa zake anakwambia uchague akusaidie uchumi wako urudi kama zamani ila umpe mkeo au azidi kukuyumbisha kiuchumi ubaki na mkeo/mmeo unachagua nini?

3. Leo umepewa nafasi moja tu uchague kati ya vitu hivi viwili mke/mume mzuri soulmate wako mnayematch anayechangia furaha yako kwa kiasi kikubwa au pesa na kila kitu cha fahari unachagua nini?

4. Mkeo/Mmeo anaumwa yupo hoi na uwezekano wa kupona kwake upo ila matibabu yake ndo almost mali na pesa zenu zote tena mmezipata kwa shida mno na kwa muda mrefu, ukiamua atibiwe maanake pesa hamna unabaki na mume/mke ukimwacha maana yake unabaki na pesa zako ila hakuna mke au mume unachagua nini?

NB: Hapa naomba ieleweke kabisa siongelei wale wenzangu na mimi wa hit and run au cheap and quick sex naongelea zile hisia ambazo mtu aliyebahatika kuwahi kukutana nazo zile hisia za ukweli za upendo kati ya mume na mke wanaopendana katika shida na raha ambao watafanya wanachoweza kuhakikisha wenzi wao wana furaha kikweli kama mifano ya picha kadhaa hapa.

th

th

th

th


Narudia tena topIc yetu haihusiani na easy and quick sex. Nipo tayari kusahihishwa na kuelimishwa.

Karibuni wadau tujadili kwa pamoja.
Kwangu mke
 
Me napenda kusema msiwaamin wanawake kbs ktk maisha yenu lbd mama tu.utakuj kujuta hawa viumbe dhaif sn kukusaliti n km kuuwa mbu kwa jiwe[
Mkuu mbona tuna aminika sana tu? Hivi kama wewe ni mwaminifu mi naanzaje kutokua mwaminifu?

Ni swala la kukariri tu kwamba wanawake sio waaminifu au wanaume sio waaminifu.

Au ndio ile kwakua wewe mwizi basi unahisi na mwenzio mwizi... Yani mwizi sikuzote ye anahisi kuibiwa tu.

Ninaacho amini tupo wanawake waaminifu na wapo wanaume waaminifu.
 
Sikatai wapo hao wanawake wa shoka!! I believe they still exist. But wachache mno. But asilimia kubwa ni materialistic!! Iko wazi. Ukifulia your women may not leave you the first day ulipofulia but the count down begins.
Lakini kabla hujaoa/kuolewa inamana utashindwa kujua huyu mtu wangu ni watabia gani?
 
yapo sana mkuu Eli79 nazunguka maeneo mbalimbali haya mambo yapo kabisa yaani kuna ndoa nyingi zina furaha ya kudumu na kamwe hautosikia mtafaruku wao nje,
wanavumiliana kwa hali zote,
Hivi kama watu wanahudumiana kipindi cha ugonjwa mtu hawezi hata kujisaidia mwenyewe watashindwa kuvumiliana kipindi cha kukosa pesa?
Tatizo ni hii mitandao ya kijamii wengi wachangiaji utakuta haijui ndoa wala maana yake, uboyfriend na ugirlfriend anaubadili katika ndoa.
hapo anaanza kulalamika ndoa hazifai ndoa ni machungu
kwa kipimo hicho hata wewe msomaji utaona ndoa hazifai.
Ilhali kuna watu chungu nzima tunazifurahia ndoa zetu zilizojengwa katika msingi wa upendo bila kigezo.
Na hao wa pesa ndiyo wanaharibu hii sekta kwa kuwa hawaridhiki na ni walalamishi katika kila jambo.
Tatizo watu tumechagua kwenda na mawazo hasi

Badala ya kwenda na mawazo chanya. Wakati wala haina gharama
 
Kwa kweli my jolly bebee comes first, hapana kitu ina thamani kama nafsi ya mpenzi wangu siwezi muacha in any of the potrayed scenarios above...
 
Mm mkuu ni pesa tu. pesa, pesa, pesa, pesa,

Nilishawahi kumfumania nikamsamehe, nilishabaniwa papuch sana, pesa zake ni zake. Za kwangu ni za wote. Ni mkali matusi kila kukicha amani hakuna. Bora nitafute pesa tu huenda zitaniongezea furaha.
Halafu hawa viumbe bila pesa huwez kuwamiliki.
Pesa kwanza vingine vitafuata
 
Mkuu pesa hutafutwa, lakini mke huwezi pata kama Wa kwanza hata ukitafuta.!
Mi binafsi nachagua mke, namba mbili mke pia na tatu mke!

i.e
Mke!
Mke!
Mke!
 
MUME kama pesa ata mimi napaswa kutafta.
 
Mbona madem wanapenda wanaume wenye pesa sasa bcz kama umekuwa billionaire bas utakula madem.
Kuna mchiz wang alizungushwa na demu miez kwa miez but aliponunua kijigar tu akangoa ndan ya mwezi.
Mm pesa zang first thing. Mapenz ni assumptions tu hayameki sense in search mbele ya pesa.
Kila kitu kina price even mama yako mzaz ikifika bei atakuuza.
Ukitaka kuendelea usieke mbele mapenzi bcz it is something unstable.
Kuwa na dem but usimfanye kuwa ndo every thing.
Pesa inaweza kumfanya dem akupenda na tajir anaweza kununua mke wa maskin.
 
hakuna namna ambavyo utachagua pesa over mwenzi wa maisha, never...pesa zinatafutwa na mkizisaka kwa pamoja mtapata tu.

mi ningechagua tu kubaki na mume wangu izo pesa ntaziacha tu zipite.

unaweza chagua pesa na kamwe usizifurahie pale unapokumbuka umemwacha mwenzio kwa ajili hiyo.

pesa zinapatikana tu ila furaha na upendo haureplasiwi na pesa
 
Pesa ni kwa ajili ya watu lakini watu sio kwa ajili ya pesa. Pesa isipotatua matatizo ya familia kama magonjwa ni ya kazi gani? Starehe hufanyika kama hali ni shwari nyumbani. Wadada wanaochagua pesa wengi ni kabla ya ndoa. Ni haki yao maana hawawezi kutabiri kuwa huyo mume to be atakuwa mume bora au kichomi shingoni. Lakini ukishakuwa kwenye nfoa iliyo njema obvious mume/mke (familia) ni zaidi ya pesa na actually pesa unayoitafuta ni kwa ajili ya familia
 
Mleta mada unafananisha mke na vitu vya kijinga.
 
Back
Top Bottom