yapo sana mkuu
Eli79 nazunguka maeneo mbalimbali haya mambo yapo kabisa yaani kuna ndoa nyingi zina furaha ya kudumu na kamwe hautosikia mtafaruku wao nje,
wanavumiliana kwa hali zote,
Hivi kama watu wanahudumiana kipindi cha ugonjwa mtu hawezi hata kujisaidia mwenyewe watashindwa kuvumiliana kipindi cha kukosa pesa?
Tatizo ni hii mitandao ya kijamii wengi wachangiaji utakuta haijui ndoa wala maana yake, uboyfriend na ugirlfriend anaubadili katika ndoa.
hapo anaanza kulalamika ndoa hazifai ndoa ni machungu
kwa kipimo hicho hata wewe msomaji utaona ndoa hazifai.
Ilhali kuna watu chungu nzima tunazifurahia ndoa zetu zilizojengwa katika msingi wa upendo bila kigezo.
Na hao wa pesa ndiyo wanaharibu hii sekta kwa kuwa hawaridhiki na ni walalamishi katika kila jambo.