Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,640
- 697,999
Binadamu pamoja na maarifa yake yote kashindwa kujua kitu kimoja!...kesho yake si waamini Mungu, miungu wala wapagani si wanazuoni mahiri wala wanasayansi waliobobea wote maarifa yao yamegota kwenye leo na sasa hivi zaidi ya hapo ni upofu na giza.
Hali hii imesababisha kutokea kwa elimu ya utabiri na unajimu kwamba wewe kesho yako itakuwa hivi au vile
Hii elimu ni pana na kongwe sana na imegawanyika katika makundi haya;
-kwa kutumia nyota
-kwa kutumia viganja vya mikono
-kwa kutumia majira ya mwaka, miezi na tarehe za kuzaliwa
-kwa kutumia herufi na majina
-Na kutumia hii ya karata za tarot
Katika zote hizo ni hii ya kutumia karata za tarot ambayo hutoa majibu ya uhakika na uhalisia zaidi na uchezaji wake ni rahisi Tarot yaweza kuwa ndio elimu ya utabiri na unajimu kongwe zaidi duniani ikiwa na zaidi ya miaka 500
Kwenye kusoma karata za tarot huwa kuna mafungu yaani karata tatu sita tisa kumi na mbili na kuendelea lakini iliyo maarufu ni tatu na sita ni katika uchezaji huo karata utakazochagua ukija kulinganisha majibu yake na ukafananisha na mambo yako utapata majibu ya kushangaza mno
Hebu jaribu kuingia kwenye mtandao sasa ugonge tarot card reading halafu utaniambia...na baada ya hapo hutahangaika tena na tabiri zingine zisizotoa majibu ya uhakika!!! jaribu sasa