Utabiri wa Hali ya Hewa: TMA ipewe maua yake

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,016
144,373
Sipendi sana kutumia huo msemo, ila kwakuwa ndio uko kwenye chati, wacha niutumie kuwapongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kwa kutoa utabiri wenye viwango.

Wote ni mashuhuda wa utabiri wa mvua za mafuriko kutoka TMA japo wako watu waliobeza ila muda umethibitisha.

Waliochukua tahadhari watakuwa wameepuka mengi ikiwemo usalama wao na wa mali zao na waliopuuza bila shaka itakuwa imekula kwao.

Endeleeni kufuatilia utabiri kutoka TMA.

Hongereni sana TMA

NB: Weather Forecasting is a science and not otherwise.
 
Hii kitu imepiga usiku kucha haikutosheka, bado imepiga kutwa nzima na inaendelea kupiga🙆🙆🙆
 
Iko hivi, TMA wanasadiwa na EU kupitia The European Organisation for the Exploitation of Meteorological Satellites (EUMTSAT)

EUMTSAT wana-monitor hali ya hewa hapa Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupitia hiyo satellite niliyotaja hapo juu

EUMTSAT wao ni service provider wa TMA

Ikumbukwe awali TMA walikuwa wanatumia mfumo wa zamani ambao haukuwa sahihi sana (2nd Generation Satellite)

Mfumo mpya wa satellite ya EUMTSAT ni wa kisasa (3rd Generation Satellite) umeanza kutumika mwaka huu na matokeo yake ndio haya tunayoyaona
 
Iko hivi, TMA wanasadiwa na EU kupitia The European Organisation for the Exploitation of Meteorological Sayellites (EUMTSAT)

Hao jamaa wana-monitor hali ya hewa hapa Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupitia hiyo satellite niliyotaja hapo juu

EUMTSAT wao ni service provider wa TMA

Ikumbukwe awali TMA walikuwa wanatumia mfumo wa zamani ambao haukuwa sahihi sana (2nd Generation Satellite)

Mfumo mpya wa satellite ya EUMTSAT ni wa kisasa (3rd Generation Satellite) umeanza kutumika mwaka huu na matokeo yake ndio haya tunayoyaona
Kwa kuongezea tu.zamani kidogo, data za hali ya hewa zilikua zinatumia netwek za serikali tu.na zinachukua muda kusoma ukweli kutoka katika eneo husika.lakin kwasasa data zao zimeunganishwa moja kwa moja kupitia na mitandao ya simu.
Yaani kwenye kila netwek ya simu na data za hali ya hewa zinasoma ndani ya dakika 5, na baada ya nusu saa zinasoma kidunia.
 
Mbeya huku vipi aisee, mbona mvua hamna kabisa.

Especially, hii wilaya ya mbarali, yani ni joto balaa, nyie mnaolima vitunguu pande za igawa hapa acheni uchawi.
 
Sipendi sana kutumia huo msemo, ila kwakuwa ndio uko kwenye chati, wacha niutumie kuwapongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kwa kutoa utabiri wenye viwango.

Wote ni mashuhuda wa utabiri wa mvua za mafuriko kutoka TMA japo wako watu waliobeza ila muda umethibitisha.

Waliochukua tahadhari watakuwa wameepuka mengi ikiwemo usalama wao na wa mali zao na waliopuuza bila shaka itakuwa imekula kwao.

Endeleeni kufuatilia utabiri kutoka TMA.

Hongereni sana TMA

NB: Weather Forecasting is a science and not otherwise.
Si mlipuuza? Ngoja muogelee kwenye vinyesi vyenu huko Dar
 
Back
Top Bottom