Uswis yatoa Masharti kuwataja walioficha Mabilioni...

Source Mkuu!

Siku chache baada ya Mbunge wa K/Kaskazini Z.Z.Kabwe kutoa hoja binafsi bungeni juu ya uwezo wa Watanzania kuficha mabilioni nchini Uswisi ili serikali ifanye uchunguzi na kuwabaini,serikali ya Uswis imetoa masharti kadhaa ili jambo hilo lifanyike.

Masharti hayo ni pamoja na serikali ya Tanzania inatakiwa iwataje wahusika wanaotuhumiwa, pia itaje na makampuni ya utafutaji wa Mafuta yanayodaiwa kuhonga ili yapatiwe maeneo ya uchimbaji.

Pia Tanzania imetakiwa izithibitishie mamlaka za Uswis kuwa pesa/mabilioni hayo yametokana na rushwa au "Fraud", pia waeleze nani alimuhonga nani na namna fedha hizo zilipofanyiwa "Transactions"

...kwa masharti hayo na mengine, Serikali ya Uswis itakuwa tayari kutoa ushirikiano na si vinginevyo....

Je, masharti hayo ni msaada kwa Watanzania kupata "Offshore Billions" au ndo kinyume chake?
 
Usishangae kukuta huo ni mpango mkakati wa makusudi kati ya watawala wetu wakishirikiana na serikali ya Uswis ili ionekane kuwa upo ugumu wa kulifuatilia jambo hili.
 
Siku chache baada ya Mbunge wa K/Kaskazini Z.Z.Kabwe kutoa hoja binafsi bungeni juu ya uwepo wa Watanzania kuficha mabilioni nchini Uswisi ili serikali ifanye uchunguzi na kuwabaini,serikali ya Uswis imetoa masharti kadhaa ili jambo hilo lifanyike.

Masharti hayo ni pamoja na serikali ya Tanzania inatakiwa iwataje wahusika wanaotuhumiwa, pia itaje na makampuni ya utafutaji wa Mafuta yanayodaiwa kuhonga ili yapatiwe maeneo ya uchimbaji.

Pia Tanzania imetakiwa izithibitishie mamlaka za Uswis kuwa pesa/mabilioni hayo yametokana na rushwa au "Fraud", pia waeleze nani alimuhonga nani na namna fedha hizo zilipofanyiwa "Transactions"

...kwa masharti hayo na mengine, Serikali ya Uswis itakuwa tayari kutoa ushirikiano na si vinginevyo....

Je, masharti hayo ni msaada kwa Watanzania kupata "Offshore Billions" au ndo kinyume chake?

hii ndio double standard. Ingekuwa ni hela ya Al Qaeda saa hizi kila kitu kingeshaanikwa wazi na hizo accounts zingekuwa frozen up siku nyingi. Lakini sababu ni hela ya stupid Africans hawajali
 
hii ndio double standard. Ingekuwa ni hela ya Al Qaeda saa hizi kila kitu kingeshaanikwa wazi na hizo accounts zingekuwa frozen up siku nyingi. Lakini sababu ni hela ya stupid Africans hawajali

wanaangalia masirahi ya mataifa yao kwanza tofauti na sisi tunaangalia matumbo yetu..
 
Kama mkuu wa kaya mwenyewe analiogopa hiyo issue na hivyo hana ubavu wa kulizungumzia, unategemea kweli serikali yake itimize masharti ya Uswisi (iwapo ni kweli masharti hayo yametolewa).

Kikubwa JK na mafisadi wenzake wanachokifanya ni kutafuta namna ya kulifunika suala zima la mapesa ya Uswisi.

Watanzania, tusiwe na akili za samaki kama za CCM -- hili ninalosema limeshatokea. Mnakumbuka jinsi serikali ya JK ilivyokuwa ikihaha kufunika wizi wa EPA? Ikashindikana!!!!! na hivyo ikawa hamna namna -- mambo yakawa hadharani. kilicxhobakia ni kutumia nk katika namna ya kulishuighulikia!
 
Kwa serikali yetu hii full of impunity basi suala hilo limefungwa rasmi!!! Manake hayo mashariti hayatekelezeki katika mfumo huu tulionao!!!!
 
kwa masharti haya kwa vilazi wetu na chama cha ujambazi ccm tusitegemee kitu hapo maana AG ni kilazi ile mbaya na hela walioficha wengi ni walio kwenye nyadhifa za juu. kwa hiyo hakuna jipya bali ni kuumia kimya kimya
 
kama tukiwa serious hayo masharti mbona ni marahisi tu? Idara ya usalama wa taifa na kile kitengo cha wizara ya fedha kinachoshugikia uharamia huu wafanye kazi, pia sasa zitto awataje ili sasa wachunguzwe! kwa sababu kama huna majina hata ya speculation unaanzia upelelezi wapi??
 
Iwe ni taarifa ya kweli au uongo mimi binafsi naichukulia hali hii kama drama nyingine tena. Linapokuja suala la kuwachukulia mafisadi hatua lazima vikwazo vizuke kwa lengo la kuwalinda. Hakuna kizuizi cha kuwashughulikia mafisadi kwa viongozi wenye dhamira ya kweli. Haiwezekani wezi wawe na sheria ya kuwalinda wao na mali zao siku zote. Hii ni nchi yetu wote jamani, wachache wasitufikishe mahali pa sisi kufanya maamuzi magumu. Hatuhitaji dola wala silaha ni sisi wenyewe ndio silaha itakayomaliza madhila haya. Hadithi za utawala wa sheria tusisikie tena linapokuja suala la kudhibiti mafisadi papa na manyangumi!
 
Hatujui iwapo uamuzi huu wa waswisi umetokana na lobby ya aina fulani au ni kufuatana na taratibu zao, kwa mwendo huu, tusitarajie lolote la maana kutokea; Pole Zitto, ulijaribu kuokoa watanzania katika janga hili, lakini itabidi tu suala hili ulimalizie majukwaani kisiasa (sio kwenye magazeti) kwani kisheria, dirisha ndio linafungwa hivyo..; Ni umma wa watanzania tu ndio utaweza kutatua tatizo hili iwapo Siasa za majukwaani zitatumika kikamilifu; Ushirikiano wa Zitto, Membe, na wana ccm wengine wazalendo wenye ushahidi pia ni muhimu towards that end;
 
hao hao walioko kwenye serekali na chama ndio hao hao waliofija hizo pesa uswisi na ndio hao hao wanasidi kufisadi hii nji, tunategemea nini
 
Kuna uwezekano Mh. Zitto alilijua hili ndiyo maana alishidwa kutaja majina ya wahusika bungeni ?
 
Kama Uswiss inakubali kuwa kuna walioweka hela chafu nchini kwake kwa nini serikali ya Tanzania ndio iwataje. Nilidhani ungesema wao wakiwataja serikali yetu isiwafiche iamplify hayo majina na kuahidi kufanya kazi ya ziada kuwa itatafuta wapi walikozipata
 
Tunisia, Libya Misri and other Arab countries, the only solution to end this brutality leadership.
 
Hapana, Uswis imerahisisha kazi. Kama ni kweli, cha msingi ni kule kukubali kuwa ina hizo accounts. Kama serikali itaamua, ni rahisi kwani kwa kawaida benki hulazimishwa na mahakama kufanya hivyo kama ilivyofanyika Nigeria, DRC na kwingineko.
Hayo masharti ni magumu sana kwa serikali hii, kukubaliana nayo ina maana ya kuizika rasmi CCM na serikali yake,tusitarajie lolote hapo.
 
Back
Top Bottom