Uswis yatoa Masharti kuwataja walioficha Mabilioni...

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
Siku chache baada ya Mbunge wa K/Kaskazini Z.Z.Kabwe kutoa hoja binafsi bungeni juu ya uwepo wa Watanzania kuficha mabilioni nchini Uswisi ili serikali ifanye uchunguzi na kuwabaini,serikali ya Uswis imetoa masharti kadhaa ili jambo hilo lifanyike.

Masharti hayo ni pamoja na serikali ya Tanzania inatakiwa iwataje wahusika wanaotuhumiwa, pia itaje na makampuni ya utafutaji wa Mafuta yanayodaiwa kuhonga ili yapatiwe maeneo ya uchimbaji.

Pia Tanzania imetakiwa izithibitishie mamlaka za Uswis kuwa pesa/mabilioni hayo yametokana na rushwa au "Fraud", pia waeleze nani alimuhonga nani na namna fedha hizo zilipofanyiwa "Transactions"

...kwa masharti hayo na mengine, Serikali ya Uswis itakuwa tayari kutoa ushirikiano na si vinginevyo....

Je, masharti hayo ni msaada kwa Watanzania kupata "Offshore Billions" au ndo kinyume chake?
 
Siku chache baada ya Mbunge wa K/Kaskazini Z.Z.Kabwe kutoa hoja binafsi bungeni juu ya uwepo wa Watanzania kuficha mabilioni nchini Uswisi ili serikali ifanye uchunguzi na kuwabaini,serikali ya Uswis imetoa masharti kadhaa ili jambo hilo lifanyike. Masharti hayo ni pamoja na serikali ya Tanzania inatakiwa iwataje wahusika wanaotuhumiwa,pia itaje na makampuni ya utafutaji wa Mafuta yanayodaiwa kuhonga ili yapatiwe maeneo ya uchimbaji..pia Tanzania imetakiwa izithibitishie mamlaka za Uswis kuwa pesa/mabilioni hayo yametokana na rushwa au "Fraud",pia waeleze nani alimuhonga nani na namna fedha hizo zilipofanyiwa "Transactions"...kwa masharti hayo na mengine,Serikali ya Uswis itakuwa tayali kutoa ushirikiano na si vinginevyo....Je masharti hayo ni msaada kwa Watanzania kupata "Offshore Billions" au ndo kinyume chake?

Haya masharti ni favour kwa wanaohusika na hili sagga!
 
Hayo masharti ni magumu sana kwa serikali hii, kukubaliana nayo ina maana ya kuizika rasmi CCM na serikali yake,tusitarajie lolote hapo.
 
Kwa serikali hii tuliyonayo hayo mambo ni ndoto kutekelezwa.na ndiyo utakuwa mwisho rasmi wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kutawala.
 
Hapo hawatusaidii ila pia ikumbukwe kuwa kinachofanyika kuwataja hawa ni jambo la kumfichua adui sasa ni vita. Hivyo kunauwezekano mkubwa wamekwisha kuwasiliana nao kusudi wawakingie vifua mafisad hao. Ila vilevile ikumbukwe kuwa mabenk hayo yako kibiashara ivyo wakiruhusu mabilion hayo ghafla wanakwenda kupata mtikisiko wa kifweza. Hapo ni nguvu ya sheria ichukue mkondo wake. Ingawa nasikitika ni sheria ipi Tanzania inayokumbatia mafisad itakwenda kuchukuliwa dhidi ya hao mafisad kama sio kiini macho na danadan itaenda kupigwa na mwisho kes iyo itupwe kapun. Ee Mungu ibariki Tanzania wape kuwafungua macho na akili ya kuwaongoza katika kulikomboa taifa letu. Ameen
 
Source ya hizi habari ni wapi ili tuanzie hapo, lakini pia msisahau hawa wazungu ni watu washenzi sana, ingalikua ni nch ya Kiafrika inakua kapu na mtunzaji wa fedha haramu hawa magaidi wa Ulaya na US wangeshalazimisha kile kituko cha UN kuanzisha sheria ya kuzuia kutunza pesa chafu hizo, ila kwa kuwa wao ndio majizi kwa kushirikiana na hawa watawala wa Afrika wenye njaa basi wanaona ni sawa...
 
Mtu yeyote anaweza kuzuka na habari kama hii ili kuanza kupoteza lengo la awali la kurudishwa hizi hela kwa Sisi walalahoi, masikini wa Tanzania. Tupe source ya habari yako ili tujue kuwa wewe si Mwanasheria Mkuu, au hauko kwenye list ya watuhumiwa.
 
Siku chache baada ya Mbunge wa K/Kaskazini Z.Z.Kabwe kutoa hoja binafsi bungeni juu ya uwepo wa Watanzania kuficha mabilioni nchini Uswisi ili serikali ifanye uchunguzi na kuwabaini,serikali ya Uswis imetoa masharti kadhaa ili jambo hilo lifanyike.

Masharti hayo ni pamoja na serikali ya Tanzania inatakiwa iwataje wahusika wanaotuhumiwa, pia itaje na makampuni ya utafutaji wa Mafuta yanayodaiwa kuhonga ili yapatiwe maeneo ya uchimbaji.

Pia Tanzania imetakiwa izithibitishie mamlaka za Uswis kuwa pesa/mabilioni hayo yametokana na rushwa au "Fraud", pia waeleze nani alimuhonga nani na namna fedha hizo zilipofanyiwa "Transactions"

...kwa masharti hayo na mengine, Serikali ya Uswis itakuwa tayari kutoa ushirikiano na si vinginevyo....

Je, masharti hayo ni msaada kwa Watanzania kupata "Offshore Billions" au ndo kinyume chake?

tuwekee sorce ya hii habari yako.
 
Kama hii habari ni kweli basi huu ni mwanzo wa kuanza kuwalinda wahusika kama ilivyokuwa kwenye rada.
 
Waswizi, hiki ni moja ya vyanzo mhimu vya mapato kkwao,hivyo lazima wakilinde. Wanaogopa watu watahamisha hela over night na kuzipeleka America, Asia na kwingineko. Kwahiyo tusidhani Waswiz ni malaika wanaotuhurumia sisi wanyonge NO.
 
Imekula kwetu watanzania, tusubiri 2015

Mimi sioni kama 2015 kutakuwa na mabadiliko yoyote....!!!!! yatakuwa yale yale ya 2010 kura kuchakachuliwa.....

Watanzania tumekuwa cool mno.... na Viongozi wa dini watatumika tena waseme amani amani amani.

Amani hii ya kupumbaza watanzania ili wapora mali asili ni wonder of world....

Kodi za watanzania zinaibwa, wanapeleka uswisi halafu eti madaraja na maendeleo ni pesa za mkopo Worldbank na michango ya NSSP. ........ Shame!!!!!

Wanapita pita na kuzindua miradi ya maendeleo pesa za mikopo worldbank na NSSF. Watanzania tutaendelea kupata mateso miaka na miaka kwa sababu tutalipa hii mikopo.

Anyway wacha tuteseke vizuri ili ifike mahali tuwatoe hawa Mafisadi kwa nguvu na wala sio sanduku la kura....
 
Serikali ya JK haiwezi kuwataja kamwe!!mchezo mwingine wa kuigiza!tumechoka nayo tufanye mambo mengine sasa hayo ma drama tumeyachoka!
 
Tangu suala hilo limeletwa serikali iliamua kuziba masikio na kuruhusu muda mwingi kupotea, lazima wahusika walitumia muda huo kulobby na kutishia hizo taasis kisheria. Mnakumbuka EL alizusha safari ya ghafla mara tu aliposikia hayo mabilioni yakitajwa bungeni? Hata Membe akapata wasiwasi kuwa ni safari gani hizo za ghafla wakati vikao vya bunge vinaendelea? Alijibiwa ni utaratibu wa kawaida. Anyway, bungeni walituambia Kenya, USA, India, Germany wamefanikiwa kutatua taizo hilo. Je wao walitumia kigezo gani katika kurejesha pesa zao?
 
Siku chache baada ya Mbunge wa K/Kaskazini Z.Z.Kabwe kutoa hoja binafsi bungeni juu ya uwepo wa Watanzania kuficha mabilioni nchini Uswisi ili serikali ifanye uchunguzi na kuwabaini,serikali ya Uswis imetoa masharti kadhaa ili jambo hilo lifanyike.

Masharti hayo ni pamoja na serikali ya Tanzania inatakiwa iwataje wahusika wanaotuhumiwa, pia itaje na makampuni ya utafutaji wa Mafuta yanayodaiwa kuhonga ili yapatiwe maeneo ya uchimbaji.

Pia Tanzania imetakiwa izithibitishie mamlaka za Uswis kuwa pesa/mabilioni hayo yametokana na rushwa au "Fraud", pia waeleze nani alimuhonga nani na namna fedha hizo zilipofanyiwa "Transactions"

...kwa masharti hayo na mengine, Serikali ya Uswis itakuwa tayari kutoa ushirikiano na si vinginevyo....

Je, masharti hayo ni msaada kwa Watanzania kupata "Offshore Billions" au ndo kinyume chake?

Hizo ndizo POLICIES kali za MABENKI USWIS; Ndio Maana ni taabu sana kuzipata PESA USWIS au Kutajwa WAMILIKI
LIBYA bado haijapata PESA za GADAFFI alizoficha USWIS; au PESA za BEN ALI wa TUNISIA

ROMNEY mwenyewe wachunguzi wa USA wanajua pesa ziliko Carribean; ENGLAND; AUSTRALIA lakini USWIS hawajui
Sasa ANGALIA HAPO... ni kazi haswa sio LELEMAMA; Wakifanya kosa DOGO sahau hizo pesa kuzijua...
 
Back
Top Bottom